Usalama wa Taifa haujadiliwi

Mkuu nimeelewa muktadha wako ila bado inaonyesha bado hujaujua ukubwa wa agency nlizotaja,ni matusi kuishindanisha TISS na CIA,umesahau kipindi cha mauji ya wachungaji zenji mliwaomba wao msaada,how come TISS walishindwa kukabiliana na ishu ndogo tu ya homicide.TISS wanachojua ni kungoa watu kucha tu na kuteka watu pamoja na eavesdroping tena eavsdroping ya kizamani sana.
Wapo kwa maslahi ya watawala na sio wananchi,kiteknolojia ndo wako nyuma kabisaa
 
Kwa mwendo huu wa kuhusishwa na Utekaji wa Raia LAZIMA TISS WAJADILIWE.
Unanikumbusha bwana mmoja aliyeitwa MALIYAMUNGU, huyu aliongoza kitengo ndani ya taasisi ya kijasusi ya Uganda(STATE RESEARCH BUREAU) ya kipindi kile cha nduli idi amin dada.

MALIYAMUNGU aliratibu utekaji, utesaji na mauaji ya wale wote walionekana ni hatari kwa serikali ya idi amin.
 
Usalama wa taifa lipi? Hawa watekwao?
 
Eti spies? Wakati makontena ya udongo wa madini yakivushwa kwa Kipindi cha miaka 20, wao walikuwa wapi?
 
[QUOTE="gkutta, post: 20646646, member: 7

KITENDO CHA KUNYANYASA RAIA HAKITAFUMBIWA MACHO MAANA NI RAIA WANAIPA UMUHIMA TAASISI HIYO KUWA YA KIPEKEE PALE TU INAPOJIHESHIMU KUHESHIMU RAIA NA HAKI ZAO KAMA WANANCHI NA KSIA, AMANI, NA USALAMA WA NCHI.[/QUOTE]Hii taasisi ipo imara sana ila tatizo haijapewa meno ya kutosha na kingine wanasiasa ndiyo wanaiharbu wanapenda iende kisiasa siasa ila bado ninaimani nakupa hawa watu
 
Mleta mada yuko sahihi mia ya mia. Huwezi jadili usalama wa taifa jf wala facebook wala twita.
Kama CIA wanapo tesa na kunyanyasa watu wanajadiliwa na kuundiwa tume za kuwachunguza itakuwa majambazi na wabakaji hawa?
Wacheni woga wa kijinga na kujipendekeza kitoto toto.
 
Wale twiga walisafirishwa vipi?
 
Mkuu nimeelewa muktadha wako ila bado inaonyesha bado hujaujua ukubwa wa agency nlizotaja,ni matusi kuishindanisha ....
Nina wasiwasi mkubwa kuwa yawezekana haujaelewa muktadha wangu! Mimi sijashindanisha mtoa huduma yeyote. Nilichokifanya ni kueleza ukweli juu ya vitu muhimu vitumikavyo kutoa huduma hii. Nikasisitiza umuhimu wa kuwa na rasilimali watu maalum katika utoaji huduma. Ebu fuatilia kwenye vyanzo vyako mbalimbali vya habari juu ya umuhimu wa rasilimali nilizotaja katika kutoa huduma hii, nina hakika utauelewa muktadha wangu sawia
 
Sasa kama mkuu/ nosi wa kipindi hicho alikuwa ameruhusu unadhani wangeenda kukamata kinyume na maelekezo....na ulijuaje kama taarifa zao zilikuwa wakitipoti hazifanyiwi utekelezaji ?
Anyway unaweza dhihaki kuwa hawafanyi kazi ni maoni yako pia na una Uhuru wa kuandika kabisa....
 
Sijapingana na wewe kuhusu rasilimali watu,na rasilimali nyengine mtambuka.Ila sidhani kuwa wanarasilimali watu wanaofaa,kama yule alemtishia nape bastola ni wakwao basi inaonyesha wazi bado wako nyuma sana. agency inayotumika kisiasa na kuminya haki za wananchi haiwezi kuwa agency nzuri.
 
Sijapingana na wewe kuhusu rasilimali watu,na rasilimali nyengine mtambuka.Ila sidhani kuwa wanarasilimali watu wanaofaa.....
Mkuu mapungufu yapo sehemu nyingi tu. Na kuna utaratibu unaofaa kurekebesha mapungufu hayo.

Ngoja ni kukumbushe kuwa hao watoa huduma wanaosifika nao wanamapungufu makubwa mno kuliko unavyodhani. Waliwahi kumtuhumu kiongozi fulani wa nchi fulani kuwa ana silaha za mahangamizi, wapi! Walisababisha maafa makubwa kwa kupotosha jeshi la nchi yao kwenda kuziharibu silaha hizo. Hawakuzipata silaha, walimuua kiongozi yule na raia wake wengi pamoja na kusababisha vifo vya baadhi ya askari wa jeshi lao.
------
Mkuu mambo haya niyakutazama kwa kutumia jicho la vipimo vinne (4 dimensions)! Vinginevyo unaweza kupandwa na hasira bila sababu.
 
Mkuu hakuna shirika jema la ujasusi hata moja,CIA wameshasababisha vifo vya zaidi ya watu milioni kumi mpaka leo,kuanzia cuba,el salvador,congo na kwengineko.ila wenzetu wanadeal zaid na external sabotage,kupigania interest zao nje ya nchi sisi,wakwetu wanadili na internal sabotage.
Ninachopinga mimi ni hii kauli ya kusema eti TISS hawapaswi kuchunguzwa na bunge,eti kisa wao ni shirika nyeti.hilo ndilo nalopinga.
 
....
Ninachopinga mimi ni hii kauli ya kusema eti hawapaswi kuchunguzwa. ...
Nimekuelewa mkuu.

Lakini ukipata muda fuatilia utendaji watoa huduma hao maarufu wanachowafanyia wananchi wake wenye asili za Asia, Latino, na Afrika.

Jioni njema.
 
Usalama wa taifa haujadiliwi kwa sababu ni sehemu za siri za taifa.
 
Okay u
Umeeleweka mkuu,,,kumbe wana majukum Makubwa muda mwingine kuliko hata police,,,nimegundua wao ndio wanajukumu kubwa hadi kudhibiti huujumu uchumi ikiwemo Wa maliasili zetu kama kudhibiti wanyama wasitoroshwe na kadhalika,
na ufisadi ukiacha usalama wa nchi, ,
 
Nimekuelewa mkuu.

Lakini ukipata muda fuatilia utendaji watoa huduma hao maarufu wanachowafanyia wananchi wake wenye asili za Asia, Latino, na Afrika.

Jioni njema.
Mbona nayafahamu mkuu,kuanzia oparation PAPERCLIP,MKULTRA mpaka MOCKINGBIRD,hawa jamaa ni mafia kuliko wale wa sicily.ila ishu ni modus operandi ya agency yetu ni mbaya.

A Timeline of CIA Atrocities
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…