Usalama Uwanja mpya (Terminal) 3, Unatia Mashaka.

Usalama Uwanja mpya (Terminal) 3, Unatia Mashaka.

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2018
Posts
336
Reaction score
567
Wiki iliyopita nilifanikiwa kurudi Kibaruani Ng'ambo baada ya kuwa nchini kumuuguza Mzazi wangu kwa muda mrefu.

Wakati wa kuondoka nikitumia Uwanja mpya "Terminal 3" kusema kweli Uko poa sana. International Standards!

Ila kuna vitu kadhaa nilifanikiwa kuobserve.

1.) Usalama kuanzia unakata kona kuingia uwanjani hadi unaingia uwanjani hakuna Askari niliyemuona (Labda kama wapo Kanzu ambao hata mtu ukipata shida ni ngumu kuamini kama ni askari kutokana na 'Wasiojikana'.

2.) Msafiri anaweza kuingia hadi kufika check in point na mzigo wake hadi kukabidhi bila kukaguliwa. (Hakuna Scanner yoyote kukagua mzigo unaoingia hadi kukabidhiwa.)

Kama ipo itakuwa ndani kabla ya kupakia (baada ya kukabidhi na msafiri kuwa ameshatoweka eneo hilo kuelekea waiting lounge)

Hii ni hatari iwapo mtu anataka kufanya tukio, anaweza kuingia na silaha na kushambulia watu ndani ya uwanja( Sehemu ya Check in)

...au hata Kuweka kitu hatari ambacho kinaweza kusababisha madhara (Mf. Kilipuzi au hata Silaha ya Kibaiolijia-kumbuka enzi za Kimeta nk.)

3.)Wasindikizaji wana access ya kuingia hadi ndani sehemu ya ku check in na kutoka (Sio jambo baya) ila ni muhimu tukiangalia usalama kwa yeyote anayeingia kuwa scanned.

Hii itasaidia kulinda usalama wa Wasafiri na Rasilimali yetu.

NB: Nashauri kuwekwe Scanner ya ukaguzi wa awali wa mizigo na wasafiri pamoja na kuwa na Askari wanaotambulika ili kusaidia usalama panapotokea tatizo.( Sina maana wawe wanazunguka na silaha muda wote pale ndani ) wenye Silaha wanaweza kuwa sehemu maalum, na walinzi wa kawaida wakawa Hata Suma JKT kuangalia usalama wa awali

Pia Kuwe na sehemu/chumba maalum ndani hii itasaidia kwa ukaguzi binafsi zaidi iwapo utahitajika bila kudhalilisha mtu yeyote hadharani.

Naomba kuwasilisha!
 
Genuine concern nitajaribu ku observe next month tena nitaingia na mock kilipuzi kutest the security
 
Waweke scanner Kama ya pale Kigali Int. Airport
 
Sawa hoja imefika mahali panapostahili maoni yako tutayashughulikia
 
Genuine concern nitajaribu ku observe next month tena nitaingia na mock kilipuzi kutest the security
Kuna mashambulizi ya aina nyingi, ingia hata na mkasi kwenye begi utest nao ( Ofcourse kama unasafiri utauacha uwanjani check in ya pili juu ambapo kuna scanner ya usalama) hata knife crime inaweza kutokea.
 
Wamewaachia wananchi muone mpige selfie, kisha mkasimulie.

Sipendi ulinzi wa askari wetu wala rushwa na wasumbufu, watumie camera na hizo scanners hizi haziombi rushwa, na hazisumbui wananchi.
 
No offense, askari wa suma JKT ni tatizo, wapo arrogant na hawanyumbuliki (sio waelewa). Binafsi sipendekezwi wawekwe hapo.
 
Back
Top Bottom