Usajili wa laini mchawi ni NIDA

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Leo nilitembelea Ofisi za Nida Wilaya ya Ilemela ili kuona zoezi la upatikanaji wa namba za vitambulisho vya Nida linavyoendelea baada ya kupata taarifa kuna msongamano wa watu wengi.

Kwanza niwapongeze Ofisi zetu zote za Nida wakushirikiana na Ofisi ya Uhamiaji wanajitahidi Kwa kasi kubwa kuwahudumia wananchi ndio sababu Ofisi za Uhamiaji zimesogea hapo hapo Nida ili kurahisisha zoezi hilo, ila kuna changamoto moja kubwa ambayo nimeibaini watu wengi simu zao zitazimwa ifikapo tarehe 20/1/2020 kwa sababu tatizo liko Nida makao Makuu hawatoi namba za usajili Kwa wakati.

Leo nimeshuudia wananchi wengi waliosajili mapema tena mwanzoni kabisa lakini wakiangaliwa kwenye mfumo namba zao za usajili bado azijaandaliwa huko makao Makuu ya Nida ambako kuna mlundikano wa Majina ya Watu wengi ambao hawajapata namba zao.

Hii inaonesha mfumo uko taratibu sana kwa hiyo Kwa wale ambao awajapata namba zao na Nida wanakubali kwamba tatizo liko Makao Makuu kosa sio la Wananchi bali ni mfumo wa Nida wenyewe huko makao Makuu.

Hili jambo niiombe Serikali inayoongozwa na Rais wa Wanyonge Dkt.John Pombe Magufuli litazamwe upya kwani mpaka sasa watu zaidi ya Nusu ya watumiaji wa simu Nchi nzima hawana namba zao.

Ukweli ni kwamba haziko tayari wanaambiwa wasubiri kule Nida makao Makuu kuna Majina mengi yanaendelea kupewa namba. Kwa unyeti wa zoezi hili nashauri tuongeze muda kwani pia serikali itapoteza kodi kwa kiasi kikubwa sana kwani mpaka sasa kuna idadi inayokadiriwa zaidi ya watu milioni 17 hawajasajili kodi yao kwa siku au wiki kwa kutumia simu sio mchezo serikali itayakosa haya mapato. Utaratibu uwekwe upya mpaka Juni mwaka huu..

BY: DENNIS NYAMLEKELA KANKONO KATIBU WA SIASA NA UENEZI WA CCM WILAYA YA ILEMELA
IMG-20200116-WA0094.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani mwenye shida wa Kwanza ni yule aliyemteua Mkuu wa NIDA Tanzania nzima na kama ni lawama zetu basi zote tuzipeleke Kwake na tuacheni Unafiki wa Kuwalamu NIDA kwani yawezekana walishaomba mambo mengi tu yenye Tija yafanyiwe Kazi au yaangaliwe kwa Umakini wake ila Mtanzania Mmoja tu mwenye Kiburi nchi hii akawadharau na kutowasikiliza Ushari wao.

Upumbavu namba Moja unaanzia tu pale unapoweka Ukomo wa Jambo ambalo Kiuhalisia kila baada ya Saa 24 kuna Mtu mwingine Kiumri anakidhi Vigezo hivyo kufanya Suala la NIDA kuwa ni la Mwendelezo na kamwe siyo linalotakiwa kuwa na Ukomo.

Najua ili Kuficha Madhaifu ya huyo Mtanzania Mmoja Bosi Mkuu wa NIDA namwomba kuanzia sasa aanze Kujiandaa Kisaikolojia kwani nampa kama 5% tu za Yeye kuendelea kuwa Bosi Mkuu hapo.
 
Walikuwa wapi muda wote mpaka zimebaki siku tatu? TCRA zimeni line saa sita usiku ya tarehe 19 January 2020. Msiongeze hata sekunde moja. Na ole wenu msogeze tena muda mbele. Nitawafungulia kesi ya kumhujumu Mheshimiwa Rais ambayo ni uhaini.
 
cleverbright,
Usajili line hauna kikomo. Ukinunua line mpya unaweza kuitumia mpaka miezi mitatu bila kuisajili ndipo itafungwa.

Kigezo cha kitambulisho cha nida nao ni ujinga wa watanzania tu. Kwani mzungu au mchina au mturuki akija Tanzania kufanya kazi ya mkataba anapewa kitambulisho cha NIDA?

Tuache mambo ya kipuuzi watanzania. Tuishi kwenye uhalisia wa mambo.
 
Hakuna ukomo kwenye suala la uandikishaji ili kupata kitambulisho cha taifa, ukomo uliowekwa ni wa lain zilizo active ambazo hazijasajiliwa kwa kitambulisho cha utaifa.

Mi mwenyewe ni muhanga wa hilo lakini nasema #wafunge tu! Maana kila nishapoteza siku 2 kila nikienda nikiweka foreni nakaribia kufika ili nipigwe picha na alama za vidole zichukuliwe anatoka mtu anasema mtandao umekata..! Kwakweli wanachosha shubamiti.
 
Usajili line hauna kikomo. Ukinunua line mpya unaweza kuitumia mpaka miezi mitatu bila kuisajili ndipo itafungwa.

Kigezo cha kitambulisho cha nida nao ni ujinga wa watanzania tu. Kwani mzungu au mchina au mturuki akija Tanzania kufanya kazi ya mkataba anapewa kitambulisho cha NIDA?

Tuache mambo ya kipuuzi watanzania. Tuishi kwenye uhalisia wa mambo.
Kumbe Ndio maana wenzetu wakienda Ulaya kila baada ya miezi kadhaa anakuwa na line mpya
 
Back
Top Bottom