Usain Bolt kufanyiwa majaribio ligi ya Australia

sky walker

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
1,160
824
_102557076_79768292-c53e-47de-a5e0-61079b0b77f3.jpg




Bingwa mara nane wa Olimpiki Usain Bolt ameanza mazungumzo ya majaribio ya kusakata soka nchini Australia , klabu moja imesema.

Mwanariadha huyo wa jamaica , 31, anafanya mazungumzo ya kiusaini kandarasi ya wiki sita n klabu yaCentral Coast Mariners, klabu inayoshindana katika ligi ya dara la A nchini humo.

Afisa mkuu wa klabu ya Mariners Shaun Mielekamp amesema kuwa klabu hiyo ilitumia miezi minne kumsaka Bolt na mkataba wa muda mrefu huenda ukafuata baadaye.

Bwana Rallis ambaye amehusika na mkataba huo aliambia Sky Sports kwamba mazungumzo yanaendelea kuhusu mshahara wa Bolt.

''Mmiliki wa Central Coast Mariners ameamua kutafuta fedha zaidi na kuhakikisha asilimia 70 ya mshahara wake'' , bwana Rallis alisema.

Chombo cha habari cha News Corp Australia kiliripoti kwamba makubaliano ya mamilioni ya madola yameafikiwa.

Awali Bolt amekuwa akifanya mazoezi na klabu nchini Ujerumani , Norway na Afrika Kusini.

_102564940_2b766e00-d49a-4a16-b01a-48715a30bff8.jpg

Bingwa huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mita 100 na 200 , ambaye alistaafu katika riadha mwaka uliopita amezungumzia kuhusu hamu yake ya kutaka kucheza soka na kuwa mchezaji wa kulipwa.

Bolt ni shabiki wa Manchester United na naibu mkufunzi wa klabu hiyo Mike Phelan sasa yuko katika klabu hiyo ya Mariners.
Shirikisho la soka nchini Australia limeambia BBC kwamba halitahusika katika kufadhili majaribio ya Bolt.

Bwana Mielekamp amesema kuwa anatumai kwamba majaribio hayo yataongezewa muda.

''Iwapo kila kitu kitakuwa sawa, huwezi kujua? huenda akachezea ligi ya daraja la A msimu huu, aliambia chombo cha habari chaSeven Network siku ya Jumanne.

Bwana Mielkamp alisema kuwa klabu hiyo imepokea ripoti nzuri kuhusu mchezo wa Bolt wakati alipofanya majaribio na klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund na timu ya Norway ya Stromsgodset.

"Kitu muhimu nadhani ni kusubiri kujua iwapo ni mchezaji mzuri wa kiwango gani'', bwana Mielekamp alisema

"Wakati utasema yupo katika kiwango gani na iwapo anaweza kucheza katika ligi ya daraja la A''.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom