USAILI WA CLUB RAHA SHOW JIJINI MWANZA

USAILI WA CLUB RAHA SHOW JIJINI MWANZA

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Jana nilibahabika kuangalia usaili huu wa Vijana wetu kupitia klabu hii. Vijana wengi waliojitokeza ni wa kidato cha nne na ninatumaini hawana shughuli maalum za kufanya. Asilimia 90% ya waliosailiwa walikuwa wanataka kuimba nyimbo za Bongo Fleva. Asilimia 99% ya wale walioimba waliimba hovyo hovyo. Siyo kuwa ninapinga usaili huu LAKINI wito kwa Vijana wetu kuweni na shughuli za kufanya hata kulima mbogamboga, kupiga viatu rangi n.k kuliko kukimbilia usanii ambao wengi hamuiwezi. Vijana wengi wanadhani kuwa usanii ndo unaolipa kwa sasa, hapana ninaomba mjishughulishe na shughuli za kuwaingizia mapato kuliko kufikiri kuwa usanii unalipa.
 
Back
Top Bottom