Usahihi: VAT kwenye escrow

Halafu nimegundua humu watu linapokuja swala kumwajibisha mtu wa kabila lake hupoteza ufahamu Sangalala ww ni wakutetea wezi leo?
Acheni ukabila bwana mbona wengine tunatoka na pinda sehemu moja lakini tuko front line kusema the man must go
Mambo gani haya vijana wa Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Kuongea ni haki ya kila mmoja wetu, lakini kuongea ktk jambo usilo na ufahamu nalo ni kujitia aibu. Pesa za ESCROW hazikupaswa kulipwa mwaka jana. Mosi kwa sababu kulikuwa na shauri juu ya namna ya kukokotoa ''capacity charge'' kwenye mahakama ya kimataifa ya usuruhishi. ''Capasity charge'' ndio msingi mkubwa wa kujua ipi hela ni ya UMMA (TANESCO) na ipi sio. Pili ndani ya pesa hiyo kuna kodi (vat), kanuni za ukusanyaji kodi zinataka kodi ilipwe ndani ya muda muafaka. Kwa kanuni hii mfanyakazi hukatwa kodi moja kwa moja na si kupewa hela ''then'' akalipe TRA. Tatu TZ ni nchi yenye kufuata utawara bora, je ktk malipo hayo SHERIA, TARATIBU NA KANUNI zilifuatwa. Jambo hili ni muhimu kujibiwa kwa sbb ndani ya nchi tunaamini hakuna alie juu ya sheria.
 

I totally agree with you. Kuna upotoshaji mkubwa sana katika hili jambo. Kila kitu kimechukuliwa kisiasa na kupakana matope. Ni aibu sana kwa watu wazima wanaosema eti ni wachambuzi kupotosha mambo kwa kusema maneno mengi amabyo hayafungi mtumba. Kinachotaliwa sasa ni IPTL kulipa hizo pesa za VAT au kufilisiwa kwa kufuata sheria zilizopo, kama zinasema hivyo.
 

Ni kweli kabisa TRA walitakiwa kulipwa VAT kama inavyofanywa na kampuni nyingine yeyote ile. Kama wanakataa kufanya hivyo basi ni lazima wachukuliwe hatua kama wadaiwa wengine wowote.
 
Hivi hii IPTL bafo inaendelea kufanya kazi?? yan tangu 95 tunazungumzia IPTL tu.. Hii ni kampun ya wizi kabisa na ni uchochoro wa mafisa kufuja pesa zake


nimemsikiliza lusinde.. Sijaona cha maana alichoongea.. Na elimu yake darasa la sita

profesa mhongo naye kama kawaida propaganda za gas kahamishia IPTL

kiukweli hapa hakuna mjadala


WAZIRI mhongo.. Werema... Waziri pinda na wenzake wawajibishwe


mtoa mada naye alivyokuwa mwehu ameona ni sahihi hela zilipwe then kodi ndo ikatwe... Kwa mfumo wa nchi gani????


IPTL wafukuzwe.. Na aliyeileta hii kampun hana tofauti na aliyeileta dowans..... Ufike wakati na yy ajiuzulu kwa kulitia hasara taifa
 
TANESCO kama shirika la UMMA ilitakiwa wakati wanalipa IPTL ilibidi wa WITHOLD TAX husika na kuipeleka TRA.
Hawakutakiwa walipe kiwango chote IPTL kikiwa na VAT.

Maajabu haya. Ndivyo sheria ya VAT Tanzania inavyosema kuwa mnunuzi ndiye anayekusanya pesa ya VAT? Una uhakika gani hiyo pesa itafika? kwani kila mnunuzi ni msajiliwa wa VAT?
 
Naona kuna mkuu East African Eagle amegusia withholding tax,je ingekuwa sahihi TANESCO wangefanya hivyo.

Ndio maana nashauri, tufuate maelekezo ya lusinde "TUSEME UKWELI ILI TUTENDE HAKI"

Tusitafute sababu za kulazimisha, haitowezekana, ukweli ukiibuka utatuumbua tuu.

Kama kuna hela iliyotakiwa kuwa with held ingekuwa with held wakati malipo yanapelekwa kwenda escrow, watanzania tukumbuke kwamba kama hizo hela zisingepelekwa escrow, zote zingekwenda IPTL na huu mjadala usingekuwapo.

sasa tunapoanza kuleta na mambo ya withholding tax kwenye eneo ambalo haihusiki, hiyo inakuwa sio HAKI.
 
Maajabu haya. Ndivyo sheria ya VAT Tanzania inavyosema kuwa mnunuzi ndiye anayekusanya pesa ya VAT? Una uhakika gani hiyo pesa itafika? kwani kila mnunuzi ni msajiliwa wa VAT?

TANESCO KASAJILIWA.
Si tu ni mnunuzi mkubwa bali pia ni muuzaji mkubwa wa Umeme.Alitakiwa a-withold tax na kupeleka TRA
 
Unachoongelea hapa katika hali ya kawaida upo sahihi kwenye upande wa VAT. Usichokijua hapa ni kuwa ni lazima uongelee mambo matatu kwa pamoja.

Kwanza kuna uuzaji wa makampuni, sheria inatamka wazi kuwa mauzo ya kampuni hayakamiliki mpaka kodi zote zinazodaiwa na serikali zimelipwa. Na hapo ndipo unakuja ule umuhimu wa ukokotoaji ili ifahamike ipi ilikuwa ni hela ya umma na ipi ilikuwa ya IPTL. Baada ya ule ukokotoaji kufahamika, na hela ya IPTL kufahamika, ile hela ya IPTL ilitakiwa kulipiwa kodi zote kabla ya mauzo ya mauzo ya hisa za wanahisa, ndipo Wizara waridhie/waidhinishe uuzwaji wa hisa za VIP na Mechnan. Swali uuzwaji uliwezaje kufanyika bila ukokotoaji kufanyika, na kodi zote kulipwa? Kwenye uuzwaji wa kampuni, kodi zote hulipwa kabla na siyo baada ya kuiuza kampuni.

Pili, inaonekana wazi Wizara ya Fedha na Wizara ya Madini na Nishati walikuwa wanalijua sharti hili, ndiyo maana unaona kulikuwa na mawasiliano mengi juu ya VAT. Mwanasheria Mkuu hata bila kuwa na haki za kisheria (aliegemea zaidi ruhusa aliyoitoa Rais) akaielekeza Wizara ya Fedha kuwa VAT isilipwe lakini Wizara ya fedha ilijua kuwa siyo sahihi, ikaamua kuchelewesha malipo (bila shaka kuna jitihada zilizokuwa zikifanywa na TRA kutaka kodi ilipwe), lakini Mwanasheria Mkuu akazidi kulazimisha kuwa pesa yote itolewe wapewe IPTL na itolewe bila ya kulipa VAT.

Jambo la tatu, kama VIP waliouza hisa 3 (30%) walilipa TZS 38 bilioni kama kodi kutokana na mapato ya mauzo, kwa nini aliyeuza 70% hakulipa kodi inayoendana na hiyo 70%?
 

Aliyekuwa akiweka fedha kwenye account ya ESCROW ni TANNESCO na TANNESCO ni shirika la umma na hadi fedha zinachukuliwa mgogolo uliokuwepo ulikuwa haujatatuliwa hivyo basi fedha hizo zilikuwa bado za TANNESCO hadi pale mgogolo ungeisha ndipo ingeweza kuwa vinginevyo.
 
Mkuu, imekuwa vema umelileta hili katika namna hii. Ni vizuri pia kwa sababu kwa maelezo yako naona unao utaalamu wa kutosha kuweza kujadiliana suala hili katika mrengo wa kikodi (VAT).

Maelezo yako kwa sehemu kubwa yapo sawa kabisa. Lakini hapo mwishoni, kwa uelewa wangu, naona unapotosha.

Kwanza, ni kweli kuwa IPTL ndiye mwenye wajibu wa kukusanya VAT kutoka Tanesco (kwa niaba ya serikali/TRA) na kuiwasilisha kodi hiyo kwa TRA. Swali la msingi ni je pesa zilizowekwa escrow zilikuwa na VAT ndani yake. Kama jibu ni ndiyo, basi VAT hiyo ni mali ya serikali/TRA na siyo mali ya IPTL. Kwa misingi ya VAT, IPTL ni wakala wa serikali katika kukusanya kodi ya VAT. Labda kabla sijaendelea kuonesha ni kwa vipi Muhongo, AG and BOT pengine walivunja sheria, nataka uniambie kwanza mpaka hapa kama tunakubaliana kuwa pesa hizo ni mali ya umma.
 
Utalinganishaje 321 billion na swala la local purchase (cement) au kisa unataka kujustify uwizi wa hao majambazi
 

Mkuu.

Labda haunielewi vizuri.

Mimi nachukuia rushwa na kuliko kawaida, na siwapendi CCM mpaka nashangaa, lakini hiyo sio sababu ya kupotosha mambo.

Taifa linaibiwa katika biashara kati ya Tanesco na IPTL, kwa muda mrefu sana, na hata leo kama kuna malipo yanafanyika tunaibiwa pia, sababu ujio wa IPTL uligubikwa na rushwa na maslahi binafsi ya kiwango cha juu sana.

Ukiuliza pesa ambazo IPTL imelipwa na Tanesco mpaka leo, naamini ni trilions of shillings, achana na hizi bilioni mia ngapi sijui.

Hizi pesa na zile ambazo Tanesco walikuwa wanawalipa kwa madai kwamba hawana ubishi nazo zote ni wizi, hasa sababu valuation ya bei ni subjected to some models ambazo hazina market benchmarks. Tanesco na serikali inawezekana kabisa walijiingiza kwenye usanii wa kulalamikia capacity charges na kuja kutuambia kwamba imepunguzwa ili kutupoza watanzania, sababu kelele juu ya hawa watu zimeanza kupigwa muda mrefu sana.

The model used, na hata namna walivyofikia kwenye Internal rate of return ya 22% ni wizi, biashara inayooperate kwa capital structure ya Debt to Equit ya 7:3 haiwezi kugenerate retun kubwa namna hiyo katika nchi hii, hata kama wangeenda kukopa wapi haiwezekani.

Malipo ya pesa kutoka kwenye escrow ni wizi kama malipo mengine ambayo tunaambiwa hayakuwa na ulalamishi, na ni wizi ambao tumeishakubaliana nao siku nyingi, sasa kwa nini leo tunakataa IPTL asipewe hizo hela? kivipi?
 
Fugwe umemuelewa vizuri Lusinde ila hujasema kuwa Lusinde anataka zigo lote abebeshwe Mwasheria mkuu na watendaji na siyo viongozi wa kisiasa
 
Last edited by a moderator:

Hakuna fedha za umma kwenye escrow account. Hata ripoti ya CAG ilikuwa na kigugumizi, ukweli mshaambiwa kama hamtaki mnaacha, fedha za escrow siyo mali ya umma na TANESCO bado inadaiwa.
 

Mpuuzi mwingine huyu hapa!
 

Hakuna fedha za umma kwenye escrow, IPTL kama ni wakala wa kodi basi kodi itatolewa full stop.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…