Usahaulifu ndio udhaifu wetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usahaulifu ndio udhaifu wetu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by uporoto01, Mar 13, 2012.

 1. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kila ukikaribia uchaguzi mkuu na miezi kadhaa baada yake kunakuwa na kelele nyingi kuhusu ubovu wa tume ya uchaguzi, lakini kelele hizi hupotea kabisa na kutokupewa tena umuhimu mpaka wakati wa uchaguzi ambapo tunakuwa tumechelewa.Bila tume huru ya uchaguzi malalamiko hayataisha,tume iliyopo inachaguliwa na Rais aliyopo madarakani ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala na katika mazingira haya tusitegemee watatenda haki kwa vyama vyote kwa usawa.
  Baada ya mapungufu yaliyotokea kwenye uchaguzi uliyopita Kenya imeunda tume huru ya uchaguzi ambayo imepitishwa na bunge,na pia tumeona bunge likihusika katika kila nyanja kama uundwaji wa majimbo,uchaguzi wa majaji na pia nyadhifa nyingi kutangazwa na waombaji kuhojiwa na washindi kupatikana kwa uwazi kabisa.
  Bila msukumo mkubwa kuwekwa sasa kwenye suala hili hata uchaguzi wa mwaka 2015 tusitegemee miujiza kutoka tume ileile iliyoboronga 2010.
   
Loading...