Usafiri wa TAZARA

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
attachment.php

Usafiri huu kwa njia ya reli ya TAZARA ndio usafiri niliotumia mara nyingi sana kutoka Mbeya hadi Dar es Salaam. Lakini usafiri kwa njia ya reli hii hautabiliki sana hasa kuhusu ratiba ya treni ya abiria. Hapo zamani usafiri huu ulikuwa wa uhakika hasa kwa kufuata ratiba kwa mfano treni ikiondoka Dar saa 9:50 alasiri hufika Mbeya saa 7:08 mchana. Lakini siku hizi acha kabisa, kwa mfano jana treni kutoka Dar kwenda Zambia iliingia Mbeya saa 2:00 usiku bada ya saa 7:08 mchana,

Pia treni ya kutoka Zambia kwenda Dar ambayo kwa mujibu wa ratiba inatakiwa kuiingia Mbeya saa 8:10 mchana kinyume na hapo iliingia saa nne usiku na hivyo kuleta usumbufu wa abiria ambao wakati mwingine huingia katika gharama zingine na kupoteza muda mwingi.

Kuna sababu kadhaa ambazo husababisha treni kuchelewa ambazo baadhi yake ni Ubovu wa vichwa vya treni (Locomotive), ajali za kuanguka kwa treni za mizigo na kuzuia njia na wakati fulani uzembe wa wafanyakazi.

Pichani ni mojawapo ya sababu iliyosababisha treni kuchelewa iliyosababishwa na kichwa cha treni kushindwa kuvuta mabehewa hayo kutokana na utelezi wa mvua mvua katika eneo hilo. HIvyo tulikaa eneo hilo takribani masaa manne mpaka ilipoagizwa Locomotive nyingine ili zisaidiane kuivuta. Na mimi nilikuwa msafiri mmojawapo katika treni hii.
 

Attachments

  • Image109.jpg
    Image109.jpg
    122.2 KB · Views: 568
enzi zangu nilishawahi kukwama karibia na mzenga porini hakuna hata kijiji, tulianza kununua mihogo na ndizi zilizokuwa zinaenda kuuzwa Dar, tukakoka moto porini kwasababu njaa ilikuwa kali hadi migahawa ya ndani ya treni iliishiwa chakula...tulikula mihogo ya kuchoma na ndizi za kuchoma hadi tulikoma...kati ya usafiri unaosumbua huu ni mmojawapo, pamoja na kwamba hauwezi kuufikia ule wa wenzetu wa reli ya kati...huwezi amini inaunganisha nchi mbili toka dar hadi zambia..
 
Tatizo hapo wala siyo utelezi ni injini haina nguvu
Dereva wa treni hiyo ndiyo alisema ilikuwa ikislip halafu na sehemu yenyewe ni mwinuko, japo siamini sana sababu hizo lakini kubwa zaidi ni ubovu.
 
hapo ni wapi ndugu, na pia hiyo milima ni kama nusu jangwa vile...washakata miti bila kupanda mingine eeh?
 
Back
Top Bottom