Usafiri wa daladala Kigamboni ni kero tupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafiri wa daladala Kigamboni ni kero tupu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MVAA GWANDA, May 10, 2012.

 1. MVAA GWANDA

  MVAA GWANDA Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani usafiri wa daladala za kigamboni hasa za kutoka feri kwenda kibada na kongowe una kero vibaya mno, asubuhi daladala zinakatisha route toka Kongowe zinaishia Toangoma na Mikwambe CCM, tuendao feri tunabaki kubahatisha chache sana zikiwa zimejaa! Imagine asubuhi umedamka uwahi job unakaa kituoni muda mrefu ukipata usafiri ni ki-hiace mnabanana vby mno bora kufika.

  Mchana daladala zinabembeleza abiria kupanda. Jioni ndio kuna balaa kwani kituoni pale feri unakuta daladala kama kumi hivi zimepaki pembeni wanatangaza mwisho mji mwema au ungindoni, wakifika kibada piga makofi kushangilia! Hizo daladala zina leseni ya kwenda zaidi ya hapo lakini ndio hvyo tena hawataki kwenda kongowe, tunajikuta abiria 40 tunagombea kuingia kwenye hiace ya kutosha watu 15, ni vichekesho na uchungu, bora hata kugombea kwenye coaster au dcm sio ki-hiace coz kuna wagonjwa, wazee, wajawazito na watoto wasioweza kugombea gari.

  Kama hamna usimamizi ili magari yasikatishe ruti basi toeni leseni kwa coaster na dcm kuliko vipanya vinavyopaki kuota jua stendi huku tunateseka na usafiri!

  Nimekereka kiasi cha kutosha, sijui kama kuna wengine pia mnaliexpierence hilo tupeane taarifa ofisi ya Ndugulile ilipo nikamvalishe GWANDA afanye kazi yake sio kutuhubiria mradi wa mji mpya wa kigamboni kila siku.
   
 2. M

  Moony JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hamia kwingine
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  pole sana ukisikia mtu nae anaekukopa gari ni sababu ya hiyo miyeyusho mkuu pole sana..
   
 4. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Piga mbizi!
   
 5. MVAA GWANDA

  MVAA GWANDA Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla hujachangia uwe unaelewa topic kwanza, mi sijazungumzia kivuko bali daladala. Kwenye issue siriaz wengine mnaleta utani, mara hamia kwingine siwezi hama ndio nna kamjengo kangu huko nshakamalizia, aliyesema kukopa au kununua gari ni sawa lakini kwa njia moja au nyingine nawakilisha kilio cha wengine ambao hawana uwezo wa kununua hayo magari maisha yenyewe haya! Cha msingi ni kupata suluhisho ktk tatizo hili, wahusika wasimamie ipasavyo kwani wenye daladala hawatendi haki kwa wakazi wa huko. Ambaye hawezi kufuata sheria anyang'anywe leseni wapewe wanaoweza, au ndio za kwao hao wahusika hawawezi kujinyang'anya leseni!?
   
 6. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli wanaudhi sana, .. tatizo ni kwamba hakuna ukaguzi na usimamizi.
  Mbali na hilo tatizo la kukatiza route, tatizo jengine ni usalama wa abiria, magari mengi yanayotoa huduma Kigamboni ni mikweche na baadhi ya madereva hawana hata leseni za udereva.
   
 7. Chimama

  Chimama Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni tatizo sana hasa jioni..ikifika saa moja jioni kosa..wanabadili route au wanapaki pembeni wanawasubiri mnajaa halafu wanaongeza bei na kuwataka abiria kulipa bei ya jioni kama waiitavyo...hii ni kero kubwa hasa kwa wale ambao bajeti zao ziko fixed na hawawezi kutoa zaidi. Solution ni kupata simu ya mbunge na kutaarifiwa juu ya tatizo hili. Asante kwa kuwakilisha wanakigamboni.
   
 8. MVAA GWANDA

  MVAA GWANDA Member

  #8
  Dec 10, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilio changu bado kipo pale pale wadau, sijapata suluhisho hadi leo! hivi wenye daladala zenu kwanini msilete huku mkapata hela zenu za maana kuliko hawa wapemba mdebwedo wanaturingia mbaya! yaani utadhani tunaomba msaada kumbe tunalipia nauli. Wanaume mnaojua kazi leteni magari huku, wenzenu wameshapata kiasi cha kutosha wanapaki magari saa kumi na mbili! aibu yao!
   
 9. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Hii mada tumewashawahi kuijadili humu na mbunge wa jimbo la kigamboni akiwemo humu lakini mpaka leo hatujamsikia akiongea lolote kuhusu swala hili. Kwa uzoefu wangu njia zote ambazo usafiri ni wa hiace (vipanya) huwa ni kero. Ufumbuzi wa kudumu ni kuondoa vipanya na kuweka mabasi makubwa kama coaster.
   
 10. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafakari Chukua Hatua! Ikibidi "Change inaanza na Wewe"
   
 11. Dr F. Ndugulile

  Dr F. Ndugulile MP Kigamboni

  #11
  Dec 31, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Niwie radhi, sikuona hii thread. Ila kwenye "The Kigamboni I want" tarehe 18.12.2012 nilisema hivi: "Sumatra kuanzisha ruti ya Kivukoni-Muhimbili. Ruti hii itapunguza kero iliyokuwa inawapata wakazi wa Kigamboni waendao Muhimbili. Bado nafuatilia kuanzisha ruti mpya ya Feri-Pemba Mnazi. Vile vile nimezifikisha SUMATRA kero mbali mbali za kukatisha ruti na upandishaji holela wa nauli".

  Natumai kuwa na mrejesho kwako ndani ya wiki hii.
   
 12. S

  Sangomwile JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,091
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa tunasubiri kwa hamu mrejesho.Mfano vipanya vyote vinavyoenda Tungi-Mbalamaziwa,ni kipanya kimoja tu chenye sifa ya kubeba abiria,vingine vyote ni chuma chakavu.
   
Loading...