Vyoo vya feri (kivukoni) navyo ni vichafu sana halafu viko finyu sana, marumaru zimebadilika rangi zimekuwa nyeusi. Ukiingia vyoo mbalimbali vya kulipia Dar hautakuta mabomba yanayotoa maji. Maji umewekewa kwenye ndoo, kuna uhakika gani na usalama wa hayo maji?
Hebu tutoke nje ya Dar vilevile. Serikali ilipiga marufuku wasafiri wa mabasi kuchimba dawa porini na ikajenga vyoo baadhi ya maeneo hususan palipo na mizani, vyoo hivyo ni vichafu sana. Nakumbuka safari moja nikielekea Mbeya tulifika sehemu, kabla ya Kitonga, kuna choo cha serikali, abiria ilibidi kweda nyuma ya choo (porini) maana choo hakifai.