Usafi wa sukari tunayoitumia

Usafi wa sukari tunayoitumia

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,244
Habari wakuu Imekuwa wikiendi tulivu na yenye rasharasha za hapa na pale za mvua
Twende Kwenye dhumuni la hii thread

Kwa muda sasa takribani miezi miwili nimekuwa nikifuatilia usafi wa sukari ninayoitumia hapa nyumbani
Nilijilidhisha na mazingira tunayohifadhia sukari kwa hapa nyumbani ila sijaridhishwa na jinsi sukari inavyohifadhiwa madukani,supermarket na hata Kwenye magodown huko viwandani kwa nionavyo Mimi usafi katika maeneo hayo tajwa hapo juu ni tatatizo na kupelekea Mimi mtumiaji wa mwisho kuwa na maswali mengi sana mpaka kufikia kujiuliza labda sukari tunayoinunua humu madukani kuwa imechakachuliwa,yenye ubora wa mwisho au labda ni makapi.

Haya yote yanakuja baada ya kugundua kuwa Mara nyingi ninapokoroga sukari Kwenye chai katika kikombe na kunywa Kuna vichembe chembe na takataka ambazo haziyayuki hata iweje labda Unaweza jiuliza kuwa ni kwa sababu ya majani ya ila sikweli maana Mimi huwa natumia tea bags na si rahisi kuweka chembe chembe za majani ya chai kutokana na uchunguzi nilioufanya.

Jambo hili linanipa ukakasi sana katika afya yanga au zetu Sisi walaji na watumiaji wa mwisho wa bidhaa hii

Sijajua watumiaji wengine humu JF kama mshakutana na kadhia hii.
0125201345.jpeg
0125201335.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu ipo sana tu,binafsi nimeshazoea kabisa hiyo hali ya uwepo wa takataka kwenye sukari hasa hizi tunazonunua madukani.Cha muhimu kumuomba Mungu atuepushe na maradhi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu sukari za packet.... Sukari za kupima dukani huwa nikinunua vinabaki viunga unga chini ambavyo navyo haviyeyuki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom