Otorong'ong'o
JF-Expert Member
- Aug 17, 2011
- 37,526
- 25,734
Wana Bodi,
Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza kwa dhati kabisa Halamashauri ya Jiji la Arusha kwa kuuboresha mji huu...
WACHUUZI NA WAMACHINGA
Hakika kwa mtu yeyote mgeni akifika leo Arusha atastaajabu kwa usafi wa Jiji hili la Kimataifa na kitalii Barani Afrika..
Sikuwahi kuamini kwamba ipo siku wale wafanya biashara wadowadogo sana sana kina mama waliokuwa wanapanga bidhaa zao chini mf. nyanya, parachichi, ndizi mbivu kuku wabichi n.k, kwamba kuna siku watakuja kutoka katikati ya Jiji.
Ila kwasasa hakuna hata mchuuzi mmoja unaweza ukamuona katikati ya mji....Hapa naomba kutoa pongezi za dhati kabisa.
Maduka ya bishara nayo yanaudhabidhaa zao ndani ya duka bila kutoa baadhi ya bidhaa zao nje ya maduka...
PARKING
Kwasasa bara bara za arusha zina pitika kwa raha mustarehe kabisa. Magari yamepaki kwa utaratibu maalu(I love this)....Kuna space ya kutosha, bara bara unaiona mwanzo mpaka mwisho kabisa....nazo boda boda zinapaki kwa ustaarabu wa ajabu kabisa....Pia napenda kutoa pongezi zangu za dhati katika hili...
USAFI WA BARABARA
Hakika bara za jiji la Arusha hususani maeneo ya katikati ya mji ni safi mno....isipokuwa maeneo machache ambayo yanauchafu, mchanga na tope lilikwama pembezoni mwa bara bara.....Natoa pongezi pia katika hili..
OMBI KWA MANISPAA
Naomba usafi huu uendelee hivi hivi isije ikawa ni nguvu ya soda.....Pia naomba Manispaa iwe makini sana maana nimeshaanza kuona baadhi ya kina mama na wamachinga wanarejeakatikati ya mji hasa wakati wa jioni kuanzia saa 4.00pm..(Saa kumi jioni)....Hasa maeneo ya France corner na kilombero...Naomba Manispaa ifuatilie swala hili...
Yote kwa yote mji wa Arusha kwa sasa ni msafi....Hakika kwa staili hii tunaweza ipiku Manispaa ya Moshi kwa usafi;
Karibu Arusha, Karibu mji wa kitalii, karibu Geneva of Afrika.