USA kuishambulia Iran karibuni

Nakubaliana na wewe kwa 14%
 
Kutokana na ramani mlango bahari huo ni mali ya Iran na anao uwezo wa kuzuia meli yoyote isipite hapo lakini kibinadamu njia inayopitwa na watu wengi iko shambani kwako kuifunga si vizuri.Na kuhusu vikwazo Adui yako muombee njaa ili kumtia adabu lakini mjia hiyo ya vikwazo haiwezi kufaa kwa sababu anayewekewa vikwazo ana mafuta na wengi wanayahitaji ili kunusuru chumi zao sasa ni rahisi sana kusaliti juhudi za ADUI YAKO MUOMBEE NJAA.pia kuna watu wawili ambao njaa na shida zao za kutaka kuwa vinara wa dunia ndo wanampa kichwa huyu jamaa watu hao ni Mrusi na Mchina kwanza wao wanataka mafuta,Yaleyale ya syria kumpa back-up na ndiyo maana Assad yuko hadi leo.Vkwazo si rahisi kufanya kazi kwa mtu kama Iran
 
Kwa maoni yako mkuu... Unaona kama Iran ana anavuruga amani ya mashariki ya kati???

Unakubaliana na Trump kitu anachotaka kufanya kutaka kumdhibiti kwenye makombola???

Pia kwa maoni yako unazungumziaje uwezo wa kijeshi wa irani dhidi ya nchi wapinzani hapo mashariki ya kati.

Je nini sababu ya Iran kuwa proxy groups hapo mashariki ya kati.
 
Kwa maoni yangu ni kweli Iran inavuruga amani siyo mashariki ya kati tu bali hata huko Yemen na kwingine kwa kuwa sapoti Mjahidina wa maeneo hayo na kuweka kambi huko.Pia nakubaliana na Trump kuidhibiti Iran kutengeneza mfumo wa Makombola ya masafa marefu maana huo kwa Iran inataka uchokozi kwa nchi nyingine maana walishatangaza kuwa wanataka kuifuta Israel sasa nchi inayotaka kuifuta nchi nyingine ikianza kuchukua hatua hizo lazima wenye akili timamu wataanza kustuka kwa maana makombola hayo siyo ulinzi bali ni maangamizo kwa nchi zilizo mbali nawe.wasingekuwa wanatishia kufuta baadhi ya nchi basi nafikiri wangekuwa sawa tu tatizo lao ni hilo.Mwisho sababu ya kuwa na hawa proxy huko mashariki ya kati hasa hawa Hizbulah ni kupata influence katika eneo husika ili wao waweze kujipenyeza wazima wazima huko.Swali lako la tatu sijalielewa unaposema wapinzani wa Iran una maana gani maana Iran hapo mashariki ya kati hawampendi kabisa labda hao proxy wake tu
 

US-Iran: "The US has a weak hand... everyone know that it won't go to war"
 
Wapinzani wake hapo M.E ni pamoja na Israel,oman na Saudi Arabia..

Irani kwa maelezo yao tayari wana makombora ambayo yanafika M.E yote..

Sasa wana haja gan tena ya kumzuia kitu tayari anacho..

Unakuliana na mim kuwa urusi na China wanataka Marekan aingie vitani wamnyanyang'e u super power???

Kwa kutunguliwa drone yake je iyo Show of Force bado ina impact ..
 
Iran si ya kubeza kijeshi hata hivyo hana ubavu wa kuwashinda maadui zake kwa pamoja,Kwa maelezo yao tayari wanayo makombora ya kufikia nchi zote za Mashariki ya kati ni uongo,Maana Mara nyingi sana wanajeshi wa Iran wanauwawa na ndege za kivita za Israel katika kambi zao zilizoko Syria na Lebanon na kama ninavyoijua Iran wangekuwa wamevurumisha makombora hayo nchini Israel kulipiza kisasa lakini mpaka Leo vituo vya Iran huko Syria na Lebanon vinapata mkong"oto kila uchao toka Israel. Huu in mchezo aliokuwa anaucheza Saddam Hussein mbele ya majeshi ya ushirika kwa kudai anazo silaha za maangamizi kumbe hana chochote na Iran naye anaimba wimbo huo huo wa aliyekuwa jirani yake Saddam Hussein.Urusi na China hawawezi kumnyang"anya Marekani u-superpower simply tu ameingia vitani na Iran Superpower hauji hivihivi tu Bali in kuwa na nguvu za kiuchumi na nguvu za Kijeshi kitu ambacho si rahisi kwa Urusi na China kuupata kwa sababu ya Marekani kuingia vitani.Mwisho kabisa baada ya kuanguswa hiyo Drone Marekani ilitangaza kuishambulia Iran kitu ambacho si kawaida na baadaye ilitangaza tens kusitisha shambulio hill Kijeshi kitu kama hicho hakipo huwezi to a taarifa kwa adui Bali hushambuliwa kwa kustukiza Ndiyo maana Mimi hiyo niliita ni SHOW OF FORCE tu.
 
Unaamin hawana wakati mwaka huu walipiga makombora toka kwao Iran mpk Syria kwenye kambi ya ISI karibu na kambi ya marekan..

Me naamin huwez shambulia toka irani kwenda Israel sababu hapo inakuwa vita moja kwa moja na ndo maana Israel pia hawez shambulia direct toka Israel to Iran

Unazungumziaje pia swala la Irani kupandisha uchakataji wa uranium to weapon grade kuanzia tarehe 27June..

Kuna wachambuzi wa siasa za mashariki ya kati wanasema mpango wa Trump kuhusu irani umeanza ku backfire.. We unazungumziaje hilo???
 
Iran na Syria wanapakana hivyo uwezo huo anao lakini wa kufika Israel hana kinyume chake Israel wanao uweza wa kushambulia Iran bila shida yoyote,Sijapata kitu kinachonidhibitishia kuwa Iran ana uwezo wa kufika Tel Aviv pamoja na kwamba ana hamu sana lakini uwezo sasa unamkosa siku akifanikiwa basi anaweza kutekeleza azima yake hapo sasa ndipo Israel nayo inaweza kutumia silaha yake ya turufu.
 
Ingependeza sana kama ungekuwa unakuja na swali moja hapo ningekuwa na uwanja mpana kuelezea zaidi kwa nin iwe hivyo, sababu gani na kadhalika!!.
 
nasikia USA kazuia kabisa mafuta yao kuuzwa popote pale, mwaka 2017 ilikuwa ivyo ivyo na kupelekea mauzo kushuka kutoka barrels 8 million per day hadi 1 million per day. Sasa saiv wamezuia kabisa wairan watakula jeuri yao.
 
nasikia USA kazuia kabisa mafuta yao kuuzwa popote pale, mwaka 2017 ilikuwa ivyo ivyo na kupelekea mauzo kushuka kutoka barrels 8 million per day hadi 1 million per day. Sasa saiv wamezuia kabisa wairan watakula jeuri yao.
Kwani USA anatoa riziki au Allah?

Mungu anasema binadamu wangejua navyo gawa riziki wasinge tapa tapa, wangetulia kwa amani na ninge wapa riziki zao kama ndege, Mungu anauliza nani anaye mlisha samaki kwenye bahari kama si Mungu.

Yani kusema wa Iran watakula jeuri yao, hawawezi kula jeuri yao, mpaa Mungu atake.

USA c mgawa riziki anaye gawa riziki ni Mungu, yani lazima ujuwe kuwa super power ni Mungu tu c USA.

Iran watashinda c kwa sababu ni wana power kuliko USA, ni kwa sababu wanamini Kwenye haki hata ichukue mda gani haki inapatikana tu.

Mungu anasema hakuna Jeuri hamuangamiz,i kumbuka hapo jeuri ni USA anatoka wapi mpaa wapi kumfata Iran.
 
Ujinga kama huu hata kwa Saddam Hussein walikuwa wanasema haya haya mwishowe akapata kichapo cha mbwa koko,Kwenye mambo ya vita hayo mambo weka pembeni jipange pambana usitegemee Imani akusaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…