Gomez Luna
Senior Member
- Mar 13, 2017
- 187
- 205
Jeshi la anga la Marekani limefanyia majaribio bomu lake jipya la nyuklia B61-12.
Jaribio hilo lililofanyika March 14 kwenye jangwa la Nevada limewekwa wazi Leo kwamba lilikua la mafanikio makubwa.
Bomu hilo lilibebwa na ndege vita aina ya F16 katika jaribio hilo. Lengo la jaribio hilo lilikua ni kujua uwezo wa ndege vita hiyo F16 katika ubebaji na urushaji wa bomu hilo pia kujua uwezo wa bomu hilo ukiacha ule wa nyuklia.
Bomu hili ni jipya kabisa kabisa katika hifadhi ya silaha za jeshi la Marekani likiwa pia na uwezo wa kupeleka nyuklia mpaka kwenye ngome za adui zilizopo chini ya ardhi.
Inaarifiwa kwamba majaribio haya ni moja ya uendelezwaji wa sera ya Rais mpya wa Marekani Donald Trump kuboresha mifumo ya nyuklia ya jeshi la Marekani kama alivyoahidi wakati wa kampeni.
Updates:
Idadi ya wapiganaji waliokufa imefikia 94,maafisa wa Afghan wamesema.
Source:Abcnews