ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Marekani imedondosha bomu kubwa la kabisa kuliko yote(non-nuclear) dhidi ya Islamic state nchini Afghanistan.
Msemaji wa jeshi la Marekani anasema bomu hilo limedondoshwa mashariki mwa Afghanistan kwenye mapango makubwa ambapo iliarifiwa kuna wapiganaji wa Islamic state.
Hii ni Mara ya kwanza kabisa kwa bomu hili kutumika tangu kutengenezwa kwake.Liliangushwa na ndege aina ya MC-130 kwenye eneo la Nangarhar karibu na mpaka wa Pakistan.
Mpaka sasa haijajulikana ni kiasi gani cha madhara kimesababishwa na bomu hili kubwa kabisa lenye uwezo wa kuchimba hadi futi 200 chini ya ardhi.
Je, nini kitafuata toka kwa Trump baada ya hili?!