Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,427
SERIKALI ya hapa imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa enzi ya vita baridi kufutia uamuzi uliochukuliwa na Marekani.
Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kusitisha rasmi wajibu wake mwishoni mwa wiki.
Akizungumza juzi mjini hapa, kiongozi wa nchi hii, Rais Vladimir Putin alisema taifa hili litaanza kuunda makombora mapya na akaonya endapo Marekani itatengeneza makombora na wao watafanya hivyo.
Mkataba huo uliofikiwa kati ya Marekani na muungano wa Jamhuri ya Kisovieti na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri.
“Washirika wetu wa Marekani wametangaza kusitisha wajibu wao katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,”alisema Rais Putin.
Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa mataifa ya Magharibi Nato, Jens Stoltenberg alisema kwamba washirika wote Ulaya yanaunga mkono hatua ya Marekani kwa sababu Urusi imekiuka mkataba huo kwa miaka kadhaa.
Alisema matakwa ya miezi sita iliyotolewa na Marekani kwa Urusi kufuata kutekeleza kikamilifu yanafaa kuzingatiwa.