comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950

Ripoti ya mashirika ya kijasusi
ya Marekani ilisema kuwa Putin aliamrisha kufanyika kwa udukuzi,
Urusi inasema kuwa madai kuwa Urusi iliendesha kampeni ya udukuzi wa mitandao ili kushawishi uchaguzi wa urais nchini Marekani si kweli.
Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kuwa Urusi imechoshwa na madai hayo.
Alisema kuwa ripoti iliyotolewa na mashirika ya ujasusi nchini Marekani kuhudu madai hayo haina msingi wowote.
Hayo ndiyo matamshi ya kwanza kutoka Urusi tangu rais mteule Donald Trump akabidhiwe ripoti hiyo.
Trump amekuwa akipinga madai ya udukuzi wa Urusi tangu ashinde uchaguzi wa urais mwezi Novemba.