Urusi na China zaanza mazoezi ya pamoja

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
China na Russia zaanza mazoezi yao ya pamoja ya kijeshi katika eneo la Ningxia



Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB limeripoti kutoka mji mkuu wa China, Beijing kuwa manuva hayo yanaendelea hivi sasa katika eneo hilo linalojiendeshea mambo yake lililoko kaskazini mwa katikati ya China yakishirikisha askari zaidi ya elfu kumi wa nchi hizo mbili pamoja na aina mbalimbali za ndege za kivita, mizinga, vifaru na magari ya deraya.

Kwa mujibu wa makamanda wa kijeshi wa China na Russia, mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi yanaakisi upeo mpya na wa juu kabisa wa stratejia jumuishi ya nchi hizo mbili.


Rais Vladimir Putin wa Russia (kulia) na Rais Xi Jinping wa China
Luteka hiyo inafanyika sambamba na maadhimisho ya mwaka wa 20 tangu uliposainiwa mkataba wa ushirikiano wa kirafiki na ujirani mwema kati ya China na Russia.

Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema, manuva hayo ya pamoja yanayoshirikisha majeshi ya China na Russia yanaweza kutafisiriwa pia kuwa ni ujumbe wa kutoa onyo na indhari kwa uingiliaji wa Marekani katika eneo hilo.../
 
Umoja was China na Russia unaitwaje?
Kichwa umepewa kitumie kufikiria na sio kufugia nywele.
Wewe ni MPUMBAVU.
Na sijui Dunia imepatwa na nini tu.. Kadili maalifa yanavyoongezeka na wapumbavu ndivyo wanazidi kuongezeka.

Kwa hiyo hayo mazoezi ya pamoja kwako yanakupa picha gani?

Kwako umoja ni Jina, sio MATENDO?.
 
wa kupuliza na mbalaka,........acheni hay0 mambo wakuu!! Mbona mnataka kuiharibu siku njema kabisa hii ya ibada? Tutofautiane kistaha tu
Hako kabinti kanajifanya kana uchungu Sana na US kanakuja na lugha za hovyo hovyo jamvini.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom