Urusi: Marekani Imetangaza Vita Vya Kibiashara

Kamanda wa Kweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2014
Posts
1,448
Reaction score
846
Waziri mkuu Wa Urusi amesema vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Urusi ni sawa na kitangaza vita vya kibiashara.Amesema kuwa mikakati iliotiwa saini na rais Trump, insonyesha udhaifu Wa rais huyo Wa Marekani ambaye alisema ameaibishwa na bunge la Congress.
Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi Wa 2016, ns vitendo vyake dhidi ya Ukraine.

Bwana Trump alilishutumu bunge la congress kwa sheria hiyo.

Katika kutia saini makubaliano hayo, dhidi ya adui Wa marekani Siku ya jumatano, Trump alisema mkajati huo sio sawa.

Sheria hiyo pia inaiwekea vikwazo Iran na Korea ya Kaskazini.

Bwana Medvedev alionya kuwa, hatua mpya zinazolenga kumuondoaTrump madarakani zitachukuliwa kwa kuwa siyo MTU aliye na utaratibu.

Urusi tayari ilishalipiza kizqzi wiki iliyopita kwa kuwatimua wanadiplomasua 755 waliokuwa wanatanya kazi katika ubalozi Wa Marekani.
Iran kwa upande wake imesema vikwazo hivyo vinakiuka makubaliano ya nuclear na jwamba itachukua hatua zilizo sahihi na sawa ili kulipiza kisasi.

Korea ya Kaskazini kwa upande wake bado haijatoa taarifa yo yote.

Mataifa kadhaa ya ulaya ikiwemo Ujerumani yanahofia vikwazo hivyo vipya vinaweza kuathiri kawi hiyo ya Ulaya.

Source: BBC Swahili.
 
Huyu Medvedev na Putin washaigeuza Russia kama mali yao. Huwa wanabadilisha urais na uwaziri mkuu; term ya huyu ikiisha kikatiba wanabadilisha hizo nafasi; term ikiisha tena wanabadilishana tena; hivyo hivyo nadhani hadi watakapokufa.
 
"Hatua mpya zinazolenga kumuondoa Trump madarakani zitachukuliwa, kwa kuwa ni MTU asiye na utaratibu" hii kauli inamaanisha nini ??? Wajuzi Wa maswala ya kimataifa nifahamisheni Tafadhali.
 
Hivi vikwazo ukifatilia kwa jicho la tatu vinalenga kukuza biashara ya gas ya Marekani pale Europe. Maana Russia anauza 38% ya gas yake Ulaya huku Marekani ni 2% tu. Maana wanajua wakishaharibu biashara ya gas ya Russia kwa Ulaya bhas washammaliza Urusi maana uchumi wake utakua taabani. Ukitaka kujua zaidi jaribu pia kufatilia hotuba ya Trump alipokua Poland aliyoyasema kuhusiana na biashara ya Nishati.
 
Huyu Medvedev na Putin washaigeuza Russia kama mali yao. Huwa wanabadilisha urais na uwaziri mkuu; term ya huyu ikiisha kikatiba wanabadilisha hizo nafasi; term ikiisha tena wanabadilishana tena; hivyo hivyo nadhani hadi watakapokufa.
Huo ndio ujuha kabisa. Ww inakuhusu nn?
Wananchi wao ndio wamewaweka madarakan halafu ww kutoka manyara inakuuma. Mtume basi baba yako akagombee
 
Mkuu kwema? kama urusi imeweza kuingilia uchaguzi wa Marekani kumsaidia Trump basi ni lazima tuelewe kuwa warusi si watu wa mchezo mchezo!! ndio sababu Marekani inawawekea vikwazo. Kuhusu gesi ni ngumu sana kwa Marekani kuuza gesi yake Ulaya, kivipi? ataisafirisha kwa meli? angalia geografia kati ya Marekani na Ulaya. Mrusi anasafirisha gesi yake kwa njia ya Bomba ambayo kimsingi inapunguza gharama. Hivyo vikwazo vipya vitaiumiza sana ulaya kuliko Urusi, nafikiri umesoma alichosema rais wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker!!
 
Hao watu wawili ndio wamerudisha hadhi ya urusi...kutoka kuishi kwenye magoti hadi kusimama na miguu yote miwili.
Russia ilikua crippled Putin na Medvedev wameiponya na wanaendelea kuangalia isiumie tena.
Huyu Medvedev na Putin washaigeuza Russia kama mali yao. Huwa wanabadilisha urais na uwaziri mkuu; term ya huyu ikiisha kikatiba wanabadilisha hizo nafasi; term ikiisha tena wanabadilishana tena; hivyo hivyo nadhani hadi watakapokufa.
 
Hivi vikwazo ukifatilia kwa jicho la tatu vinalenga kukuza biashara ya gas ya Marekani pale Europe. Maana Russia anauza 38% ya gas yake Ulaya huku Marekani ni 2% tu. Maana wanajua wakishaharibu biashara ya gas ya Russia kwa Ulaya bhas washammaliza Urusi maana uchumi wake utakua taabani. Ukitaka kujua zaidi jaribu pia kufatilia hotuba ya Trump alipokua Poland aliyoyasema kuhusiana na biashara ya Nishati.
Sasa ndugu yangu hebu tupe ELIMU kidogo hapo uliposema MAREKANI (US)
inalenga kufanya BIASHARA ya gas EUROPE kwa style ipi ....sasa hivi US ni wachimbaji wakubwa wa Gas Duniani?

Zimwi likujualo......
 
Umoja wa ulaya bado hawajakubaliana na hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo Russia kuziumiza pia nchi za Ulaya
 
Hao watu wawili ndio wamerudisha hadhi ya urusi...kutoka kuishi kwenye magoti hadi kusimama na miguu yote miwili.
Russia ilikua crippled Putin na Medvedev wameiponya na wanaendelea kuangalia isiumie tena.
russia bado ni crippled tu. wangekua wamesimama na miguu yote miwili na wao wangeiwekea marekani vikwazo badala ya kulialia tu. unafkiri marekani anauwezo wa kuiwekea china au nchi za ulaya vikwazo? hivi vikwazo ni kwaajili ya nchi ndogo ndogo. iran, venezuela, cuba, russia, korea kaskazini. kama hiyo ndio hadhi ya russia sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, kwa akili kama hizi ccm itaendelea kutawala milele.
 
russia bado ni crippled tu. wangekua wamesimama na miguu yote miwili na wao wangeiwekea marekani vikwazo badala ya kulialia tu. unafkiri marekani anauwezo wa kuiwekea china au nchi za ulaya vikwazo? hivi vikwazo ni kwaajili ya nchi ndogo ndogo. iran, venezuela, cuba, russia, korea kaskazini. kama hiyo ndio hadhi ya russia sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Pambana na Hali yako,hayo uliyo yaandika sio bure
 
Back
Top Bottom