kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,129
- 24,429
Russia kujenga mji mwezini ifikapo 2040
Russia imetangaza kuwa imenuia kujenga mji mwezini ifikapo mwaka 2040, katika mradi ambao utafanyika kwa awamu tatu.
Kwa mujibu wa televisheni ya al Alam, ratiba ya huko nyuma ya Shirika la Anga za Juu la Russia iliyotangazwa mwaka 2014 ilisema kuwa, shirika hilo lina mpango wa kutuma mwanadamu mwezini ili kuandaa mazingira ya kuwekwa jiwe la msingi la kujenga mji katika usawa wa mwezi.
Mamia ya wataalamu wa anga za juu wa Russia wamewasilisha maombi yao ya kutaka kuteuliwa kuwa watu wa kwanza kwenda kufanikiza kazi hiyo.
Hata hivyo na baada ya kuitisha kikao maalumu, shirika hilo la anga za juu la Russia limetangaza kuwa, kazi ya kujenga mji huo wa kwanza mwezini itafanyika kwa awamu tatu na kukamilika mwaka 2040.
Katika awamu ya kwanza itatumwa 'module' maalumu kuzunguka mwezi. Awamu ya pili itakuwa ni ya operesheni maalumu ya kupeleka watu mwezini na pia kujenga kituo cha kudumu juu ya mwezi baina ya mwaka 2025 hadi 2040.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, awamu ya tatu ya ujenzi wa mji huo itamalizika mwaka 2040. Kwa mujibu wa Shirika la Anga za Juu la Russia, hati za mwisho za operesheni hiyo ya mwezini zitakamilika mwishoni mwa mwezi Februari 2019.

unaona mbele sana aisee, yani siku ikisikika vita ya dunia wenzetu tayari wamesha andaa mji wao mpya,Kazi kwetu kwa sisi Waafrika, Mwenyez Mungu atatulinda tu 