Urusi katika Kutimiza Malengo na Ushindi wanavyopata

Pearce

JF-Expert Member
Dec 15, 2018
577
1,381
Kwa wasomaji wa historia wanawezea kufahamu hili

Urusi katika Vita ya Dunia walivyoingia 1941 baada ya Germany kukiuka mkataba na Soviet walioingia kwa Siri kugawana ulaya Mashariki. Ambapo Russia alianza kwa kuivamia Finland 1939 Hadi 1940 akiwa na lengo aichukue nchi yote lakini aliishia Chukua kilomita 35,000 tu

Huku akipoteza askari taklibani laki 160 na majeruhi zaidi ya laki 210, Finland akipoteza askari 25k na majeruhi elfu 60

Ambapo Stalin akifurushwa kutoka katika League of Nation, Russia kwao ikawa ushindi ingawa malengo hayakutimia waliweza Chukua sehemu ya Finland na ambayo wameikalia mpaka leo

Wakiwa Bado wanampango wa kujitanua .Wakati Germany kaivamia Poland nao Russia wakaingia mashariki ya Poland baada ya kuwahadaa Wapoland kuwa wanaisaidia dhidi ya uvamizi wa Germany hivyo wakafanikiwa kuwahadaa maofisa wa jeshi na Serikali

wakawasafirisha kwa nyakati tofauti tofauti na kuenda waua takribani watu 22,000 katika msitu ulioitwa KATYN (Poland bado Ina kisasi kwa Urusi mpaka leo) hapo kwa hadaa malengo yao yalifanikiwa pasipo madhara upande wao

Ndio ilipofika Mwaka 1941 Hitler akageuka makubaliano akaanzisha operation Barbarossa kwenda Ulaya Mashariki.

Pasipo msaada wa Marekani kwenda Soviet kuanzia intelejensia Hadi vifaa hasa viwanda vya mwanzo vya magari ya Vita na vifaru vya Soviet Soviet alikuwa kashindwa awali au maafa yangekua makubwa zaidi kwake.

pamoja na hali ya hewa ya Baridi Kali, Urusi alikuwa kashashindwa Vita awamu ya kwanza, sababu nchi za mashariki hapo awali ziliwakaribisha wapiganaji wa Germany kama wakombozi mfano Ukraine ikiwa mojawapo (Hii ilimpa kisasi Stalin kwa Ukraine baadae)

Lakini kilichofuata Soviet Russia ilipata ushindi kwa gharama ya watu milioni 27 huku alieshindwa Germany akipoteza askari Milioni 5.5 zaidi ya asilimia za vifo zikitokea Mashariki ya Ulaya

Kwa idadi hiyo utafahamu Urusi inapotaka malengo yake yatimie hawatishiwi na watu wao kufa, Urusi huanza Mali au vitu kabla ya watu.

Ndio maana unaona kwa Pride tu ya kusherekea siku ya ushindi wa vita ya 2 ya Dunia kuunganisha sherehe inoge hapo May 9 vita Bado inaendelea na ingawa kapoteza watu wengi sana,

Licha ya Putin kushindwa Malengo amegeukia mashambulizi mashariki ambapo ni rahisi zaidi kuunganisha mashambulizi mpakani mwa Nyumbani ili kufika siku hiyo atangaze kaikomboa Donbass na Luhasky na Malengo yametimia awamu ya kwanza

Pia Urusi ni taifa ambalo huwa wanakisasi sana tayari vipindi vya luninga wachambuzi wao na Viongozi wameanza hamasisha kulipiza kisasi kwa upotevu mkubwa na hasara walioipata kwenye vita hiyo dhidi ya Ukraine (sababu walifikiri watapokewa vizuri katika uvamizi wao).

Linapokuja suala la Kisasi utaona baada ya Malengo kuchukua Kiev Kushindikana wakaanza kuua raia wa Ukraine ndio yakafahamika Bucha Massacre

Pia wamewahi kufanya hivyo Chechnya dhidi ya Raia baada ya vita ya kwanza ya Chechnya kushindwa vibaya na kwa aibu

Ukirudi katika Historia Stalin kashawahi kuua wa Ukraine zaidi ya Milioni 3.9 kwa njaa kama njia ya kujilipizia kisasi sababu walitaka kuwa taifa huru Nationalism, sawa na Putin anachofanya leo.
 
Nimekuelewa vizuri....
Sababu mimi ni big fan wa Discovery channel (History).....
Hawa wasiokuelewa, vyanzo vyao vya habari ni vijiwe vya kahawa....
 
Nimekuelewa vizuri....
Sababu mimi ni big fan wa Discovery channel (History).....
Hawa wasiokuelewa, vyanzo vyao vya habari ni vijiwe vya kahawa....
Ni ukweli ambao wengi hawawezi amini sababu hawaingii ndani zaidi Kujifunza historia ukiachana na historia ya darasani
 
Back
Top Bottom