Kumfananisha Marehemu na dhahabu iliyopandwa? Sipati maana? navyojua mimi dhahabu hununuliwa, hutumika kwa urembo, thamani yake hushuka na kupanda! sasa kama Dr Gama alikuwa dhahabu ni kumshushia heshima! Binafsi nathani alikuwa mtu safi na mchapa kazi! Hivi huyu Makamba ana wasaidizi? Huwa anaandika speeches au huwa ana-flow tu? Maana tunajionea mengi kila siku na yanakuja mengineyo!
20th December 09
JK kuhudhuria mazishi ya Gama
Gideon Mwakanosya
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili mjini hapa leo mchana kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Dk. Lawrence Gama.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Christine Ishengoma, alisema jana kuwa Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili leo saa 6:00 mchana ambapo ataelekea katika kijiji cha Amani Makolo atakakozikwa marehemu Gama.
Hata hivyo, jana mamia ya wananchi walijitokeza kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Gama mara baada ya mwili wake kuwasili mjini hapa. Mwili wa Gama ulipelekwa katika makumbusho ya mashujaa wa vita vya Majimaji na kuagwa kwa heshima zote za kimila.
Baadaye mwili huo ulipelekwa katika uwanja wa Majimaji ambapo viongozi mbalimbali wa chama na Serikali waliweza kutoa heshima zao.
Akizungumzia utendaji wa Dk. Gama, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alisema marehemu alikuwa dhahabu iliyopandwa katika maeneo mbalimbali Tanzania na kwamba mchango wake hautasahaulika.
Mwili wa marehemu Gama ulisindikizwa na Makamba ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emanuel Nchimbi.
Marehemu Gama anatarajiwa kuzikwa leo mchana.
NIPASHE JUMAPILI
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=11479