Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,336
- 10,896
Habari wakuu!!
Nikiwa kama kijana mwenye fikra tata ambazo baadhi huweza kuzipokea vibaya kulingana na mfumo waliolelewa. Sitaogopa kusema ukweli bila kujali unamgusa nani. Wapo wengine wanadhani kumheshimu mzazi ni kubariki makosa ya wazazi wao. Mtoto mwenye akili hujifunza mambo mazuri kwa wazazi wake lakini mwana mpumbavu huiga na kujivunia uovu wa wazazi wake. Inashangaza kuona mtu akiona fahari kusema " Kwetu sisi tunapenda kutembea na wanawake" Wengine husema " kwetu sisi ni walevi" mara sisi ni wakatili. Huu ni upuuzi na ujinga. Mtu mwenye hekima hujivunia mambo mema.
Moja ya haki kubwa ya mtoto ni kupata urithi wa mali. Ikiwa umemrithisisha lugha, vyakula, miiko, mavazi, dini na mengineyo. Kwa nini utoe udhuru kwenye ishu ya kumrithisha mtoto Mali ambayo ni haki yake ya msingi.
Urithi hutegemea jamii husika na wakati husika. Kipindi cha zamani wazazi waliwarithisha watoto wao Mashamba na mifugo kutokana na kuwa maeneo hayo ndio yalikuwa chanzo kikuu cha mapato. Ndio maana jamii, na mataifa yalipigana kupanua maeneo ya ardhi.
Zama zimebadilika. Siku hizi kuna nyenzo nyingi za kupata kipato. Wengi husingizia kuwa tunawarithisha watoto wetu elimu. Ni sawa. Hata zamani watu walirithishwa Elimu ambayo haikuwa ya darasani lakini pia walirithishwa na mali na miradi ya kuzalisha.
Nikiwa kama kijana ninao wajibu wakujiandaa kwaajili ya watoto wangu. Tunaowajibu wa kuwaandalia watoto wetu urithi. Na si kuandaa visingizio. Visingizio havitakusaidia kitu zaidi ya kuthibitisha haukuwa Baba bora.
Usishangae mtoto wako akikudai urithi wake. Mpe na si kulalamika. Mara sijui nilikusomesha, sijui nini. Elimu ni haki ya mtoto na urithi pia ni haki ya mtoto. Ukiwa mzazi unayewaza kuwa watoto wangu watarithi nini mbali na elimu huwezi kuchezea pesa kijinga jinga. huwezi honga wanawake kama kichaa. Huwezi poteza muda hata kidogo. Wazungu hili wanalijua. Pamoja na kuwa wanawapa watoto wao elimu lakini wanawaandalia na mali nyingine haswa haswa ardhi. Ndio Maana wanahangaika kuitawala dunia na kuteka nchi za kiafrika ili wapate ardhi.
Wahindi licha ya kuwapeleka watoto shule lakini watoto wao huwarithisha miradi mbalimbali. Katika hili sidhani kuna ubishi.
Ni wajibu wetu vijana wa sasa tupige kazi. Tufikiri kuhusu watoto wetu watarithi nini. Hili tunapaswa kulifikiri hata kabla hatujaoa. Hii itasaidia kizazi kijacho kupiga hatua na si kuitegemea serikali kwa kila kitu.
Mwisho: Soma andiko hilo hapo uniambie nikisemacho hapo juu ni kweli au si kweli.
Luka 15
11 Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili;
12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake.
13 Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.
14 Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.
15 Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.
17 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;
19 sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
20 Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.
21 Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena.
22 Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
23 mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi;
24 kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.
26 Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?
27 Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima.
28 Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
29 Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
Nawasilisha!