Urgent!...ushauri unahitajika kuninusuru

calm down......

fanya uchunguzi kimya kimya... saa nyingine si kila unaloambiwa / unalosikia ni la kweli au likutie presha...

mfano ukifunga chuo unaweza kwenda kufanya uchunguzi, na angalia mwendo wa mwenzio, amebadilika nk


 
Ivi we ulitaka ule peke yako? Acha ubinafsi waache na wenzio wajipigie, we unadhani utampatia wapi wakumiliki peke yako! Tambua kabisa hyo mwenzio anamoyo wa nyama ivo usishangae akamtamani mwingine akamegwa.ivo ushauri wangu kaka maliza kwanza mishe zako siku ukitulia na kazi yako ndo usake mke, acha kukurupuka!
 
calm down......

fanya uchunguzi kimya kimya... saa nyingine si kila unaloambiwa / unalosikia ni la kweli au likutie presha...

mfano ukifunga chuo unaweza kwenda kufanya uchunguzi, na angalia mwendo wa mwenzio, amebadilika nk



Naunga mkono, aendelee na uchunguzi. Mapenzi ni kama kikohozi, huwa hayafichi ipo siku atagundua!
 
Kijana wangu Mapenzi ya mbali ni shida mno, trust me. Ukiona dalili za namna hio jaribu kuwa calm kupita kiasi halafu chunguza kimya kimya sana bila kushirikisha mtu mwingine moja kwa moja (yaani usimwambie mtu kuwa hebu nipatie taarifa za fulani) wewe ndenda mdogo mdogo kabisa na kama una mazoea ya kucheki simu yake mkiwa wote, pia acha kabisa, hata ikiita usipokee muite apokee mwenyewe.

Endelea kumpenda na muaminishe kuwa unampenda na hakuna chochote kibaya unachokiwaza juu yake, unajua kitakachotokea?? Kama ni kweli ni mwizi, utamakamata tu maana hivi vitu kuna kujisahau, kwa njia hii utapata ushahidi original na sio ule wa kuambiwa na watu.

hata hivyo, ikishindikana, mshukuru kwa muda mzuri mliowahi kuwa nao, then angalia mbele,ni rahisi kwa vijana wa kiume kupata mchumba anaemataka yeye lakini ni HATARI sana kwa binti kumpata mchumba nowadays. Labda wale wa ku-hit and run.
 

Dah!!! Dunia sasa inaelekea mwishoni.
Umri uliokuwa nao, na matatizo ya kamapenzi yatakusababishia future yako kuwa mbaya, epuka kuwa katika mahusiano yenye committment kubwa namna hiyo.
Achana nae huyo mdada.
 
Calm down focus on your studies, usichukilie kwa wakati huu hayo unayopitia kwa uzito mkubwa sana. Ndiyo ni mapenzi yanaumiza lakini piga moyo konde na uache kumfuatilia sana. Na kadri utakvyomfuatilia tena hasa kw kupitia watu wengine ndivyo utakavyopata habari mbaya lakini zisizo na ushahidi moja kwa moja na utazidi kuumia.

Mwisho siku nyingine kama unapata habari kama hizo usimuulizeulize wewe tulia.
 
kawaida sana, mwalimu anawaza apate mtoto na kuenjoy, sasa kama kakutana na mwalimu mwenzake ahaaaa..bhaaaaaaas, huna chako kijana, mapenzi is like novel ukisoma unampa na mwingine.
 
Siku hizi umekua?
Unakula mchicha??

 
Soma shule ukifunga chuo utamchunguza vizuri mwenyewe, alafu jiepushe kuwashirikisha watu jambo ambalo hata wewe huna uhakika utaishia kuachana tu na mwenzio, ukiwa likizo chunguza mwenyewe tabia zake na utaamua kutokana na wewe mwenyewe unavyo ona moyo wako unataka, kumbuka masuala ya mapenzi ni personal sana huwezi kuamua jambo kutokana na watu wanavyoona wao, kwa mfano mimi kuna mwaka nilisafiri mwaka mmoja na nusu kwenda masomoni nikawa mbali na mpenzi wangu kwa kipindi hicho hicho, niliambiwa mengi sana na watu kuhusu huyu mwanamke lakini kwasababu nilikuwa ninampenda sana na sikuwahi kuthibitisha maneno niliyokuwa naambiwa na watu ikiwemo ndugu zangu, mimi niliamua kuendelea naye na nikamuoa kwasasa ndoa yetu ina zaidi ya miaka kumi na tuna watoto wawili hatukwaruzani sana japo migogoro midogomidogo ya kindoa ipo katika ndoa karibu zote, japokuwa inawezekana kabisa mambo niliyoambiwa yalikuwa ya kweli kwamba alikuwa anacheat lakini sikuweza kufanya maamuzi bila uthibitisho, ningekuwa nimeudhulumu sana moyo wangu kwa kuamua Jambo kisa tu John na Ally wao wanaona mpenzi wangu hafai
 

Siyo ushauri mzuri,afadhali ungepita kimya!
 
Piga buku kijana achana na mapenzi utayakuta tu, ukiendekeza wataku-discontinue hapo utatia akili sasa.....!!:whistle:
 
Kijana mapenzi na shule vimekatazwa....msikilize mbarak mwinshehe (RIP)
 
nakubaliana na wadau " usiulizie sana kwa watu" wengi hawapendi uhusiano wenu. kama unataka ukweli mshirikishe Mungu kwa maombi. pia unaweza kwenda msalimia bila kumtaarifu lazima utagundua tu kitu. Pio wakikupa taarifa zake waambia unahitaji ushahiidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ