Urejeshaji wa mikopo heslb

Urejeshaji wa mikopo heslb

GreatMkubwa

Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
99
Reaction score
57
Habari wanajamvi?
Mimi ni mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu.
Nafanya kazi sekta binafsi, mara kadhaa wamekuja watu wakidai wanatoka bodi ya mikopo kwa ajili ya kutambua na kukusanya mikopo ya wadaiwa.
wanasema wao ni mawakala wa bodi ya mikopo. Ila tuliwabana kwa maswali wakashindwa kabisa kutoa evidence ya uhalali wao kufanya wanachotaka kufanya.
Wapo wafanyakazi wawili wanakatwa pesa zao na hawapewi risiti. Walidai risiti ila jamaa wakasema wanatoa risiti moja tuu kwa taasisi na sio individuals!

Swali:
Je ni halali kukusanya hizi pesa kwa staili hii ya mawakala?
Je ni sawa kulipa bila risiti na eti risiti ipewe taasisi ambayo kimsingi haijakopa HESLB?

Naomba mwenye kujua au kama mhusika wa bodi yumo humu anisaidie tafadhali
 
Piga kura kwa lowassa alisema atafuta huu ujinga.


swissme
 
HESLB nimewatumia email ya malalamiko hawajanijibu kitu hii ni wiki ya tatu!!
Nilipiga namba yao ya mezani haikuita!! Napata dial tone kama ya namba bize!!
Nipo Arusha
 
Yani na hili pia unakuja kuuliza huku??? Ah! Bado tunasafari ndefu mbele yetu.
Hiyo pesa hukupewa msaada ulikopeshwa na unapolipa unahaki zote za msingi za kufahamu taratibu zote za malipo kutoka kwa anayekudai, una haki ya kujua deni lako lililosalia ni kiasi gani, na utalipa kwa muda gani hadi kuisha. Yote haya na mengine mengi ni haki yako ya msingi kuyafahamu na hakuna mwingine anayeweza kukupa taarifa sahihi na rasmi zaidi ya yule anayekudai
 
Habari wanajamvi?
Mimi ni mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu.
Nafanya kazi sekta binafsi, mara kadhaa wamekuja watu wakidai wanatoka bodi ya mikopo kwa ajili ya kutambua na kukusanya mikopo ya wadaiwa.
wanasema wao ni mawakala wa bodi ya mikopo. Ila tuliwabana kwa maswali wakashindwa kabisa kutoa evidence ya uhalali wao kufanya wanachotaka kufanya.
Wapo wafanyakazi wawili wanakatwa pesa zao na hawapewi risiti. Walidai risiti ila jamaa wakasema wanatoa risiti moja tuu kwa taasisi na sio individuals!

Swali:
Je ni halali kukusanya hizi pesa kwa staili hii ya mawakala?
Je ni sawa kulipa bila risiti na eti risiti ipewe taasisi ambayo kimsingi haijakopa HESLB?

Naomba mwenye kujua au kama mhusika wa bodi yumo humu anisaidie tafadhali

Rudisha hela hizo ulizokopeshwa wadogo zako wasome.Mpaka umefuatwa,wewe ni mdaiwa sugu.
 
Back
Top Bottom