Urasimu katika upatikanaji wa kipimo cha MRI Muhimbili

Kitukuu

Member
Oct 18, 2008
34
19
Ndugu wana JF, wasalaam!

Kwanza nianze kwa kutoa pongezi kwa raisi JPM kwa kuwezesha mashine mbalimbali, ikiwamo MRI na CT scan, za kupima afya zetu kuwapo pale hospitali ya Taifa Muhimbili ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikifanyiwa mizengwe ili mradi tu huduma isipatikane hospitalini pale na badala yake huduma hiyo ipatikane katika hospitali binafsi ambazo wamiliki wake ni waajiriwa wa hospitali ya Taifa.

Pamoja na kuwapo kwa mashine hizo hospitalini, bado kuna kasoro nyingi. Nikitolea mfano wa mashine ya MRI, kuna urasimu mkubwa katika kupatiwa huduma ya kipimo cha MRI licha ya kuwa daktari kashamwandikia mgonjwa kupima na istoshe tayari malipo ya kupatiwa huduma yenyewe mgonjwa kashafanya. Lakini pia, endapo mgonjwa atabahatika kufanyiwa kipimo hicho bado upatikanaji wa majibu ya kipimo una urasimu pia.

Nayaeleza haya kwa sababu nimeyaona mwenyewe na yamenikuta mimi mwenyewe. Nina mgonjwa wangu ana tatizo la kupalalaizi upande mmoja wa mwili wake. Katika kutafuta chanzo cha tatizo hilo, daktari alimwandikia mgonjwa kupima MRI na CT scan. Ilikuwa Jumatatu ya wiki hii mgonjwa wangu alipoandikiwa kufanya vipimo hivyo. CT scan alipimwa siku hiyo ya Jumatatu na majibu yake yalipatikana kesho yake, yaani Jumanne. Taitizo ni MRI. Siku hiyo ya Jumatatu nilimpeleka mgonjwa mahali huduma ya MRI inafanyika. Nikaonana na mhudumu wa pale, nikampatia documents zote, ikiwa ni pamoja na risiti ya malipo ya kipimo chenyewe. Baada ya kuziangalia zile documents mhudumu alisema nije kesho yake, tena bila hata kutoa maelezo ya kwanini nije kesho. Na mimi bila kusita nilikubali maelekezo yake na kesho yake mimi na mgonjwa tukarudi tena. Kama kawaida nikaingia sehemu husika na mhudumu kumwambia shinda yangu. Kwa mara nyingine tena nikaambiwa nirudi kesho. Nikamwuliza kwanini? Hakuwa na jibu lenye maana zaidi ya kunipatia kisogo tu. Basi nilivotoka nje nikaongea na wagonjwa wengine ambao walikuwa nje wakisubiri kuingia kuulizia huduma hiyo hiyo. Wengi wao waliniambia kuwa wanakaribia wiki moja bila kupatiwa huduma hiyo na kila wakija wanaambiwa waje kesho. Mwingine aliniambia kuwa yeye alishapata kipimo hicho lakini baada ya kumshika mkono mmoja wa watoa huduma hiyo, ila bado anahangaishwa kupata majibu ya kipimo. Kupata majibu pia inahitajika kumshika mkono mtoa huduma.

MY TAKE! Hivi raisi Magufuli analijua hili? Nadhani hili ni JIPU lingine la kutumbua. Tafadhali raisi hili nalo linahitaji kutazamwa, waziri husika hebu fuatilia hili, wagonjwa wanaumia kwa kukosa huduma ili hali mashine ni nzima.

Naomba kuwasilisha.
 
Nashauri tu, kama kipimo unakihitaji kwa haraka na mfukoni uko vizuri nenda BESTA ipo maeneo ya Kinondoni hakuna longolongo huko. Hata NHIF pia ukipata kibali wanapima.
 
Dah!pole sana kiongozi!unajua serikali bado haijawa sirias na suala la kutokomeza rushwa ambayo inasababisha wanyonge kupata huduma!hivi ile staili ya kuwakamata wala rushwa kwa kuwawekea pesa za moto ilifia wapi?!kiongozi MRI Muhimbili sh. Ngapi?
 
Back
Top Bottom