Urasimu DES out

Urasimu DES out

HADOHADO

Member
Joined
May 18, 2012
Posts
31
Reaction score
0
Nimehitimu chuo kikuu huria mwaka jana, Vyeti vimetoka mwaka huu mwezi wa tano.

Tatizo lipo kwenye utaratibu wa kuchukua vyeti hivyo. Chuo kimetoa masharti magumu , kati ya masharti ni kujaza fomu maalumu na kwenda kuapa mahakamani au kwa wakili ili kugongewa mhuri.

Kama mnavyojua mahakama zetu na mawakili mhuri bila pesa haiwezekani, hapo wanafunzi inatutoka si chini ya Tsh10,000, lakini pia ukifika kwa watumishi wanaotoa vyeti utakutana mapozi kibao.

Na kilichonikera mimi ni kuambiwa eti baadhi ya vyeti havijatoka vipo nje ya nchi kwa ajili ya kusainiwa! Na Kitu ambacho mimi nakiona ni urasimu mtupu! Mara naambiwa vilipotea wakati wanahamisha ofisi!

Inakera na inaleta usumbufu sana hasa kwa wahitimu kutoka Mikoani.

Naomba wahusika waiangalie vizuri ofisi hiyo ya Director of Exammination Syndicate,DES.
 
wapumbavu sana hao wahudumu wa ofisi au wanataka uwape rushwa? Ipo kwenye vyuo vingi hyo tabia, ila wote wenye tabia za namna hyo ***** ZAO...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom