Urasimi utaisha lini nchi hii?

Urasimi utaisha lini nchi hii?

bob kalo

Member
Joined
Jul 30, 2009
Posts
7
Reaction score
0
Mimi ni mwajiriwa katika ofisi moja hapa jijini dar, juzi ijumaa tarehe 4 Jan 2013. Mimi na wenzangu tulienda ofisi za NIDA kwa ajili kupiga picha za kuweka kwenye vitambulisho vya uraia.

Hamuwezi kuamini ndg wanajf yaani zoezi la kupiga picha tu lilichukua zaidi ya saa tatu. Cha kushangaza wafanyakazi wengi ni vijana, nilifikiri kwa kuwa ni vijana basi watakuwa shapu kumbe hakuna lolote sana sana ni mbwembwe eti anaetakiwa kukupiga picha anakuambia ana pass word hawezi kuingia kwenye system oh mara system iko down.

Kasheshe nyingine nilikumbana nayo TRA- Samora branch siku ya alhamis tarehe 3 Jan 2013. Nilienda kukata road licence ya gari yangu. kawaida nilienda na road licence iliyoisha wakaniambie nirudi nilite pia kadi ya gari nikafanya hivyo.Wakaniandikia nikaenda nikalipa benki, sasa shughuli ikaja niliporudi Tra kuchukua raod licence nikaambiwa road licence hawatoi mpaka baada ya siku moja kwa maana nirudi kesho,. Nikaaenda kesho yake saa nne asubuhi wakadai bado hawajaprint hizo road licence wakasema nirudi mchane saa nane, nikarudi hiyo saa nane niliikaa mpaka saa kumi. Sikupata kitu zaidi ya kuambiwa nirudi jumatatu. Hivi kweli kwenye karne yenye teknolojia za kila aina bado mamba ya urasimu yanaendelea kwa kama ni hivi watanzania maendeleo yatakuwa ni ndoto kwetu.
 
Pole sana mkuu, hii ndiyo TANZANIA tusioijuwa, ina mambo mengi sana ya ajabu ajabu!
 
Back
Top Bottom