Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,347
- 26,153
Kugombea,hata bila Kamusi kutumika,ni kupambania au kupigania kwa nia ya kupata kitu au nafasi fulani. Sharti kuu la kugombea ni kuwepo kwa upinzani. Lazima watu,wanaogombea wawe kuanzia wawili na kuendelea. Wagombea huitajika hasa kwenye nafasi za kuchaguliwa.
Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini-TFF unatarajiwa kufanyika hivi karibuni. Nafasi mbalimbali zinawaniwa/zinagombewa. Lakini,nafasi ya juu kabisa ya Rais wa TFF imekosa Wagombea. Jina la mtu mmoja,ambaye kimantiki si mgombea,limeachwa kwenye nafasi hiyo. Ni la Athumani Nyamlani.
Athumani Nyamlani hawezi kamwe kuitwa mgombea. Ni kwakuwa yu pekee. Mambo ya kura za 'ndio' au 'hapana' yamepitwa na wakati. Nafasi ya Urais wa TFF ilihitaji wagombea.Imekosa. Inatabiriwa kuwa Athumani Nyamlani atateuliwa na Kamati ya Uchaguzi kuwa Rais wa TFF.
Uteuzi wake utakaofanywa siku ya uchaguzi ni batili. Katiba ya TFF yataka Rais wake achaguliwe. Kama kitu kiko kimoja,nani ataweza kuchagua? Kama Nyamlani amebaki pekee,hakuna ndani ya TFF atakayeweza kumchagua zaidi ya kumteua. Baada ya uvunjaji huo wa Katiba ya TFF, soka ya Bongo haitatawalika....natabiri tu.
Kwanini nafasi nyeti kama hii ya Urais wa TFF imekosa wagombea?