Urais ni taasisi, Magufuli anatapeliwa

Urais ni taasisi, Magufuli anatapeliwa

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,550
Hili jambo ni zito na linahitaji hekima sana kulijua, wengi wetu tumejikuta tunamchukia Sana Rais Magufuli kwa sababu ya mwenendo wa hali ya kisiasa na kiuchumi ndani ya taifa letu.

Nimekaa chini na kutafakari kwa kina sana baada ya kuwa nimemjadili kwa kina Rais Magufuli (mjadala wangu binafsi) na nikaibuka na jibu moja tu kwamba, Magufuli ana nia nzuri mno na Tanzania lakini watu waliomzunguka ni tatizo kubwa mno, (japokuwa na yeye ana matatizo yake binafsi).

Nimepata jibu hilo baada ya kuwa nimesoma kwa kina na kujua kazi za Urais na utendaji wake wote kwa ujumla.

Rais Magufuli amezungukwa na wachumia tumbo tupu, hawa kazi yao kubwa ni kumlaghai na kumtapeli Rais.

Kwa hiyo wanaichukulia tabia yake ya ukali kama point ya kutomshauri au kumweleza ukweli wa mambo ulivyo.

Fikiria Waziri mzima wa Fedha anapojigamba mbele ya media kuwa uchumi umekua, wakati mzunguko wa pesa mitaani umekata kabisa na pesa haina thamani hata kidogo.

Fikiria baraza la mawaziri kumwacha Rais asaini kufukuza kazi watu zaidi ya elfu kumi, bila ya waziri yoyote yule kumshauri Rais juu ya athari za kiuchumi na maisha ya familia zitakazo adhirika kwa wazazi kukosa ajira .

Fikiria baraza la mawaziri kumwacha Rais bila kumshauri azuie mikutano ya kisiasa na shughuli zote za kisiasa wakati katiba inaruhusu.

Kumwacha Rais bila kumshauri anunue ndege kwa pesa Cash wakati hata serikali ya Marekani yenyewe huwa inanunua silaha za kivita Kama ndege jeshi kutoka kampuni ya kimarekani ya "LOCKHEED MARTIN " kwa instalment, ije kuwa taifa maskini Kama letu?
Mambo ni mengi tu, kuyaeleza yote tutahitaji kitabu.

Mtu anapokuwa kiongozi mkuu wa nchi, kundi la watu waovu humzunguka ili kupata maslahi yao,wengine huwa ni under cover spies wa mataifa ya nje yenye chuki au kuhujumu taifa husika.

Kama kweli waliomzunguka Rais ni wazalendo wa kweli, wanaogopa nini kumshauri na kumwambia ukweli tu hata Kama atawafukuza kazi?

Kuogopa kufukuzwa kazi kwa maslahi ya taifa huo ni uchumia tumbo.

Mawaziri wote zaidi ya 50 kweli wangejitosa hata 15 tu na kumweleza ukweli Rais pengine hali ya kiuchumi isingekuwa ngumu hivi.

Kama hofu ni kwamba atawafukuza, unadhani atawafukuza wote, hata Kama ni wote, itafika wakati atakosa wa kufanya naye kazi na kujikuta anaanza kupokea ushauri.

Ndo maana nikasema Urais ni taasisi kwa maana ya kwamba ,Rais kuna sehemu nyingi tu anahitaji msaada wa mawazo kutoka kwa wenzake.

Nakumbuka ripot ya makinikia iliyokuwa ikirushwa live na TV, Rais aliwaomba Makamu wake na waziri mkuu aende nao pembeni wajadili jambo.

Humu JF kumejaa matapeli ya CCM kazi yao kubwa ni kumsifia Rais hata Kama kuna matatizo sehemu, hayo ndo matapeli kabisa, shida yao ni kupata shibe tu basi.

Bungeni ndo hovyo kabisa, kazi yao ni kupiga meza na kuunga mkono hoja, kwa hali hiyo Rais atawezaje ku Perform wakati kila jambo yeye anasifiwa tu,hata Kama ana hulka ya kupenda sifa, waliomzunguka wakionyesha kutokubaliana naye ni lazima atabadilika.

Rais kazungukwa na genge la matapeli.
 
Utamshauri vipi mtu asiyeshaurika, utamshauri vipi mtu anayejidai anajua kila kitu, utamshauri vipi mtu mwenye kiburi na majivuno, utamshauri vipi mtu aliyelewa madaraka, utamshauri vipi mtu anayependa kusifiwa muda wote, utamshauri vipi mtu anayejiona ana sifa za kuwa mshauri wa wanafunzi, wafanyabiashara, wawekezaji, wakulima, wafanyakazi, polisi, wanajeshi na hata machinga, utamshauri vipi mtu jiwe, mtukufu wa kiwango cha malaika Gabriel? Tulimpenda wenyewe, chaguo letu milele tuendelee tu kuisoma namba
 
wiseboy
kiongozi wako hashauriki huo ndio ukweli wenyewe kwa sbb kama watu wanamshauri vibaya ingebidi awatimue kwani nchi sasa uchumi unakwenda chini
 
Utamshauri vipi mtu asiyeshaurika, utamshauri vipi mtu anayejidai anajua kila kitu, utamshauri vipi mtu mwenye kiburi na majivuno, utamshauri vipi mtu aliyelewa madaraka, utamshauri vipi mtu anayependa kusifiwa muda wote, utamshauri vipi mtu anayejiona ana sifa za kuwa mshauri wa wanafunzi, wafanyabiashara, wawekezaji, wakulima, wafanyakazi, polisi, wanajeshi na hata machinga, utamshauri vipi mtu jiwe, mtukufu wa kiwango cha malaika Gabriel? Tulimpenda wenyewe, chaguo letu milele tuendelee tu kuisoma namba
Tukumbuke ya Hitler na Idd Amin. Historia itatuhukumu.
 
Endeleeni kujitapeli mkitarajia Tanzania itarejea kwenye ule upuuzi wa miaka kadhaa nyuma.
This is business unusual
 
Noted, Hata mbwa anathamini mabaki ya vyakula toka kwa Boss wake, Unaweza bomoa ukuta kumbe unabomoa nyumba yako mwenyewe

Jifunze maji yamebomoa ukuta au wigo wa nwendokasi stand jangwani, walichovuna wanajua wamiliki? Business as usual itabaki as usual tena itakufa zaidi bora ingebaki as usual
 
Itasimama tu tawala uja Na upita,
Mungu mwenyewe alipenda utawala huu uje ili tukae sawa sawa tusonge mbele ...ni utawala utakaokumbukwa...ni utawala unaoacha alama.
 
Endeleeni kujitapeli mkitarajia Tanzania itarejea kwenye ule upuuzi wa miaka kadhaa nyuma.
This is business unusual
If he is a serious man na kweli ana uchungu na hii Nchi kwanini HAMTUMBUI Mkandarasi ambae ni rafiki yake mkubwa ambae ndie anajenga Chato Airport wakati hana credibility ya kazi hiyo??

Mkandarasi huyohuyo ameshalipwa Tshs.14Bil mwaka wa 3 sasa kujenga barabara moja kwa kiwango cua lami iliyopo/inayopita Wilaya ya Serengeti lakini mpaka sasa hajajenga hata Mita 1 lakini ni yeye ndie ANAMLINDA..?? WHY??

Eti ana uchungu na rasilimali za Tanzania..!!

Huyu ni Mwizi kama wezi wengine tu waliopita.
 
Mungu mwenyewe alipenda utawala huu uje ili tukae sawa sawa tusonge mbele ...ni utawala utakaokumbukwa...ni utawala unaoacha alama.
Kuna tawala nyingine Mungu huruhusu ili iwe adhabu kwa wanadamu. Mkipata tawala za namna hiyo inawahitaji mtubu, mmgeukia Mungu, na sala zenu zikishapokelewa, Mungu mwenyewe huzipeperusha tawala hizo dhalimu.
 
Utamshauri vipi mtu asiyeshaurika, utamshauri vipi mtu anayejidai anajua kila kitu, utamshauri vipi mtu mwenye kiburi na majivuno, utamshauri vipi mtu aliyelewa madaraka, utamshauri vipi mtu anayependa kusifiwa muda wote, utamshauri vipi mtu anayejiona ana sifa za kuwa mshauri wa wanafunzi, wafanyabiashara, wawekezaji, wakulima, wafanyakazi, polisi, wanajeshi na hata machinga, utamshauri vipi mtu jiwe, mtukufu wa kiwango cha malaika Gabriel? Tulimpenda wenyewe, chaguo letu milele tuendelee tu kuisoma namba
Nikichukua fomu/Urais watalimia meno.
Ninanyoosha nchi kwanza, mimi huyu unishauri kitu, ww nani?
-Mimi ni Rais ninayejiamini, mimi ni jiwe, jiwe kweli.
 
Hili jambo ni zito na linahitaji hekima sana kulijua, wengi wetu tumejikuta tunamchukia Sana Rais Magufuli kwa sababu ya mwenendo wa hali ya kisiasa na kiuchumi ndani ya taifa letu.
Nimekaa chini na kutafakari kwa kina sana baada ya kuwa nimemjadili kwa kina Rais Magufuli (mjadala wangu binafsi) na nikaibuka na jibu moja tu kwamba, Magufuli ana nia nzuri mno na Tanzania lakini watu waliomzunguka ni tatizo kubwa mno, (japokuwa na yeye ana matatizo yake binafsi).
Nimepata jibu hilo baada ya kuwa nimesoma kwa kina na kujua kazi za Urais na utendaji wake wote kwa ujumla.
Rais Magufuli amezungukwa na wachumia tumbo tupu, hawa kazi yao kubwa ni kumlaghai na kumtapeli Rais.
Kwa hiyo wanaichukulia tabia yake ya ukali kama point ya kutomshauri au kumweleza ukweli wa mambo ulivyo.
Fikiria Waziri mzima wa Fedha anapojigamba mbele ya media kuwa uchumi umekua, wakati mzunguko wa pesa mitaani umekata kabisa na pesa haina thamani hata kidogo.
Fikiria baraza la mawaziri kumwacha Rais asaini kufukuza kazi watu zaidi ya elfu kumi, bila ya waziri yoyote yule kumshauri Rais juu ya athari za kiuchumi na maisha ya familia zitakazo adhirika kwa wazazi kukosa ajira .
Fikiria baraza la mawaziri kumwacha Rais bila kumshauri azuie mikutano ya kisiasa na shughuli zote za kisiasa wakati katiba inaruhusu.
Kumwacha Rais bila kumshauri anunue ndege kwa pesa Cash wakati hata serikali ya Marekani yenyewe huwa inanunua silaha za kivita Kama ndege jeshi kutoka kampuni ya kimarekani ya "LOCKHEED MARTIN " kwa instalment, ije kuwa taifa maskini Kama letu?
Mambo ni mengi tu, kuyaeleza yote tutahitaji kitabu.
Mtu anapokuwa kiongozi mkuu wa nchi, kundi la watu waovu humzunguka ili kupata maslahi yao,wengine huwa ni under cover spies wa mataifa ya nje yenye chuki au kuhujumu taifa husika.
Kama kweli waliomzunguka Rais ni wazalendo wa kweli, wanaogopa nini kumshauri na kumwambia ukweli tu hata Kama atawafukuza kazi?
Kuogopa kufukuzwa kazi kwa maslahi ya taifa huo ni uchumia tumbo.
Mawaziri wote zaidi ya 50 kweli wangejitosa hata 15 tu na kumweleza ukweli Rais pengine hali ya kiuchumi isingekuwa ngumu hivi.
Kama hofu ni kwamba atawafukuza, unadhani atawafukuza wote, hata Kama ni wote, itafika wakati atakosa wa kufanya naye kazi na kujikuta anaanza kupokea ushauri.
Ndo maana nikasema Urais ni taasisi kwa maana ya kwamba ,Rais kuna sehemu nyingi tu anahitaji msaada wa mawazo kutoka kwa wenzake.
Nakumbuka ripot ya makinikia iliyokuwa ikirushwa live na TV, Rais aliwaomba Makamu wake na waziri mkuu aende nao pembeni wajadili jambo.
Humu JF kumejaa matapeli ya CCM kazi yao kubwa ni kumsifia Rais hata Kama kuna matatizo sehemu, hayo ndo matapeli kabisa, shida yao ni kupata shibe tu basi.
Bungeni ndo hovyo kabisa, kazi yao ni kupiga meza na kuunga mkono hoja, kwa hali hiyo Rais atawezaje ku Perform wakati kila jambo yeye anasifiwa tu,hata Kama ana hulka ya kupenda sifa, waliomzunguka wakionyesha kutokubaliana naye ni lazima atabadilika.
Rais kazungukwa na genge la matapeli.
Ina maana wakati anasema yeye hapangiwi hukumsikia?

Na alimwambia mzee Makamba ushauri wako baki nao hukumsikia?

Wewe ni alama ya wanafiki, msitafute mchawi shida ipo Chato.
 
Back
Top Bottom