Urais miaka saba

Kwa nini maika saba? Mhura mmoja ni miaka mitano! Kama tunakuubaliana rais wa Tanzania akae madarkani mhura 1 basi na iwe miaka 5!
 
Hahahahah nacheka na kuwaza watumishi,wameambiwa wasubiri hadi mwaka wake wa mwisho,sasa ingekuwa miaka saba sijui ingekuaje
 
hatutaki miungu watu ikulu, kwasasa inaweza kuonekana ukomo wa 5 yrs hauna ulazima kwakua chaguzi zetu sio huru wala za haki, suluhisho ni kuwa na chaguzi huru na za haki
 
Kwa wengine wajao poa, lakini kwa aliepo madarakani akiondoka hata leo vigeregere mitaani vitatawala,kwa watumishi wa umma ndio usiseme kabisa watasherehekea kwa muda wa miaka 5 sawa na umri wa kipindi kimoja cha uchaguzi cha hivi sasa.
 
CCM itoke kwanza ndipo tutapata fursa ya kuitafakari nchi yetu hii. Kama haitoki tuingie msituni tuitoe kwa mtutu.
 
Kumbe tume ya katiba imerudi tena kukusanya maoni?
 
Miaka 4 yenyewe imekuwa mzigo mzito zaidi ya gunia la misumari ikiwa zaidi ya hapo tutashuhudia makaburi mengi sana Tanzania plus na makaburi yasiyojulikana.
 

Hoja hii ina mashiko lakini isianzie kipindi hiki cha Rais Maghufuli. Utaratibu huu uanzie Uchaguzi Mkuu wa 2025 tutakapoingia kutafuta Rais wa Awamu ya 6.
 
Muda sio issue. Hivi tatizo kubwa tulilonalo ni muda wa urais au ni uzalendo wa rais tunayekuwa naye. Hivi nchi zinazotawaliwa na wafalme huwa zinaendeleaje. nadhan hata anayepambana na mda wa kuongoza anasumbuliwa na tamaa na uchu wa nafas kama hizo ili naye afanye yale yale na kunufaika kama yule. Iwe kiuchumi au kijamii. Ukipatikana mfumo wa kujenga uzalendo kwa wananchi hata rais atakuwa mzalendo. Maana atakuwa ni zao la jamii ya kizalendo. Niulize tu hivi mfumo wetu wa leo una mwanya gani tukimpata rais mzalendo na mleta maendeleo ili aendelee kuwepo?(maana kitamu hakiishi utamu). Kama tatzo letu ni sura mpya ..basi sawa!
"Democracy is the worst form of government, except for all the others" by Churchill (1947)
 
Mawazo yako mazuri lakini hii mitano ya kwanza inawafanya wapige kazi ili tuwachague tena mitano ujayo.
 
Mi nadhani waliokuwa wametangulia walifikiria mbali sana mpaka wakaweka ukomo wa rais kwa muhula mmoja ni miaka 5, ni kwa sababu ndani ya miaka mitano kama rais atakuwa tofauti na matarajio yetu basi tutaweza kumvumilia na awamu ya pili tunamtosa. Sasa ndani ya hiyo miaka saba unayopendekeza tukipata rais asie na utu, kichwa cha mwendawazimu itakuaje??!! Hauoni watanzania tutateseka sana???
Tena mi naona hata 5 ni mingi inabidi iwe hata minne maana suala la uongozi ni la kupokezana ndio maana tuna uchaguzi ulio huru. Kutakuwa na haja gani uongoze miaka 10+ kama hata maendeleo unayojivunia hayana msaada kwa mtu mmoja mmoja!!
 
Tatizo sio kukaa miaka mingapi. Ukweli ni kuwa nafasi ya ukuu wa nchi haipaswi kukaliwa kipindi kirefu.

Tatizo tunakosa vipau mbele vya kitaifa kama Nchi kwa kuongozwa na vipau mbele vya raisi aliyeko madarakani.
Dhana ya Raisi ni taasisi haipo kabisa katika hizi Nchi zetu
 
When you are bias you always find data to backup your biasness.
 

Mtizamo wako utaheshimiwa ila sidhani kama kwa Tanzania ya sasa iliyo na Vyama vya Siasa vibovu vibovu, vigeugeu na havina Umoja pamoja na kile Tawala ambacho hakipendi mabadiliko ya Kidemokrasia ulichokishauri kitawezekana.
 
Du wengine tumeshamshtakia mwenyezi Mungu afanye kileatakachoona kinafaa Hali zetu ni ngumu Kila leo.

Na maafa haya ya alaiki manake hana ridhaa Tena na walioshika hatamu ni wao kujipima na kujichukulia hatua tu.
 
Kuna spa escrow nk atulie tuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…