Urais: Anne Makinda anafaa

Urais: Anne Makinda anafaa

Mzito Kabwela

Platinum Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,904
Reaction score
7,746
1. Hana Kashfa, sio za kujilimbikizia Mali wala kashfa zingine za Maadili. Anajiheshimu
2. Yuko thabiti. Hayumbishwi, anasimamia anachoamini. Mfano mzuri ni jinsi anavyoliongoza Bunge
3. Ni mzoefu na mweledi wa mambo ya kiserikali, amekuwa Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa siku nyingi, ameongoza kamati mbalimbali za Bunge na sasa ni Spika
4. Ni mjuzi (mweledi)wa maswala ya uchumi wa ndani na wa kimataifa(uchumi wa dunia)
5. Msomi mzuri tu na mcha Mungu
6. Kiungo kizuri cha watanzania wa dini rangi na itikadi zote

Nawasilisha
 
Jaribu kumchagua uone moto wake, wengine wako kwenye majuto sasa hivi ya uchaguzo waliofanya 2010
 
Kuna member amewahi kusema kuwa JK amefanya kila mtu yeyote aonekane anaweza urais. Na Makinda naye ni Mtu yeyote so she fits.
 
1. Hana Kashfa, sio za kujilimbikizia Mali wala kashfa zingine za Maadili. Anajiheshimu
2. Yuko thabiti. Hayumbishwi, anasimamia anachoamini. Mfano mzuri ni jinsi anavyoliongoza Bunge
3. Ni mzoefu na mweledi wa mambo ya kiserikali, amekuwa Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa siku nyingi, ameongoza kamati mbalimbali za Bunge na sasa ni Spika
4. Ni mjuzi (mweledi)wa maswala ya uchumi wa ndani na wa kimataifa(uchumi wa dunia)
5. Msomi mzuri tu na mcha Mungu
6. Kiungo kizuri cha watanzania wa dini rangi na itikadi zote

Nawasilisha
haa haa haa... umeamua kumkejeli sio?
 
Nadhani ni kweli ana msimamo na atahakikisha wabunge wanalipwa posho mpya pamoja na Rais kutoipitisha!
 
anafaa sana kama tunataka Tanzania iendelee kuwa dimbwi la mafisadi, mfumuko wa bei uzidi kupaa, kushuka kwa thamani ya shilingi< na ukosefu wa maadili kwa viongozi na kuyaendeleza aliyoyaanzisha Baba Riz
 
Muulizeni Ridhwan akapige chabo kwa babake jina la Rais ajae ili tusipoteze muda
 
1. Hana Kashfa, sio za kujilimbikizia Mali wala kashfa zingine za Maadili. Anajiheshimu
2. Yuko thabiti. Hayumbishwi, anasimamia anachoamini. Mfano mzuri ni jinsi anavyoliongoza Bunge
3. Ni mzoefu na mweledi wa mambo ya kiserikali, amekuwa Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa siku nyingi, ameongoza kamati mbalimbali za Bunge na sasa ni Spika
4. Ni mjuzi (mweledi)wa maswala ya uchumi wa ndani na wa kimataifa(uchumi wa dunia)
5. Msomi mzuri tu na mcha Mungu
6. Kiungo kizuri cha watanzania wa dini rangi na itikadi zote

Nawasilisha

Hivi mkuu uko Siriaz au una joke..hana uwezo wowote, ni mwepesi mno hebu cheki anavyopwaya bungeni..anafaa kuwa afisa kilimo na ufugaji, angemudu vizuri
 
Anafaa sana kuwa raisi wa waimba taarabu mana ana exprienc ya mipacho.
 
Punguza kashfa mkuu huyu mama amekamata nafisi muhimu sana za uongozi nchini na hajawahi kutetereka
 
Hafai yule,kwanza sio mkweli,alituambia kwamba rais amebariki posho kwa wabunge wakati sio kweli,pili hajaolewa,tatu ametumika sana hivyo akili imeshachoka,maana yupo bungeni kwa zaidi ya miaka 36,.hana jipya..tunataka chama kipya,sera mpya,mikakati na utendaji mpya,,
 
Back
Top Bottom