Urais 2015: Lowassa alijimaliza mwenyewe

Elineema J Mosi

JF-Expert Member
May 17, 2013
808
148
WIKI iliyopita, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006), Absalom Kibanda, aliandika yafuatayo kuhusu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa: " Sina shaka hata kidogo kwamba, watu wanaoijua vyema historia ya siasa katika nchi hii, watakubaliana nami kuwa jina la Edward Lowassa limekuwa ni miongoni mwa majina makubwa kwenye siasa za kitaifa, hususan zile zinazogusa nafasi ya urais kwa kipindi cha miaka 20 na ushee sasa.

Katika kipindi chote hicho, ukubwa wa jina la Lowassa umepita katika hatua mbalimbali za kuvuma, kusakamwa, kutengwa, kujizatiti, kuibuka upya, kujiimarisha na mara kadhaa kujipambanua katika sura na tafsiri ambazo zimekuwa zikiacha maswali na kuibua hoja nyingi tofauti.

Awali kabisa, niseme kwamba kipindi cha miaka 20 si kipindi kifupi kwa mwanasiasa yeyote bora kuweza kufika kwenye nafasi ya juu kabisa ya utumishi wa taifa, hasa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa na wenye utulivu.

Binafsi naona kama kuna hitilafu za msingi kuhusiana na jina la Lowassa kwenye medani ya siasa. Utadhania ya kwamba kwa kipindi hicho chote cha miaka 20 pengine amekuwa akipambana na kiongozi dikteta kiasi cha kufungwa gerezani ama alikuwa uhamishoni.

Katika kumchambua Lowassa, ni vyema nirejee mahojiano ya kina aliyofanya na gazeti la RAI, mwaka 1995, katikati ya kinyan'ganyiro. Ni muhimu kusema kwamba kwa upande fulani, Lowassa alistahili pongezi kwa kukubali kuhojiwa kutokana na taarifa za uhakika nilizozipata kuwa Rais Kikwete alikwepa kabisa. Vilevile hata Rais wa zamani, Benjamin Mkapa, alikwepa mahojiano hadi baada ya kupitishwa na chama chake.

Jambo moja ambalo ni dhahiri katika mahojiano ya Lowassa ni kutokutetereka kwake kwenye masuala mawili ya ajira na elimu. Nikinukuu: "Kwa mfano, eneo moja la haraka kabisa la kushugulikiwa ni ajira. Ajira mijini ni tatizo na tusipoliangalia sasa ni bomu.

Tumekalia bomu na wakati wowote linaweza kulipuka. Wamachinga hawa tumeshindwa kushughulika nao vizuri, na hata wanapokuja mjini hatujajibu mahitaji yao kikamilifu, kwa hiyo eneo moja la ajira kwangu mimi ni muhimu.

Lakini pili ningependa kutizama suala la elimu, elimu ni agenda moja ya haraka haraka sana. Na tukiendelea kuipuuza tunajiangamiza sisi wenyewe."
Anaendelea pia kuzungumzia uzoefu aliopata wa kushughulika na masuala ya rushwa ndani ya Wizara ya Ardhi. Anasema:

"Nilivyoshugulikia mimi nadhani naweza kutoa uzoefu huo nikaupeleka mahali pengine nchini. Lakini jambo kubwa ni nini, siyo ya mtu mmoja, yuko anayetoa na anayepokea, wote wanafanya rushwa.

Mambo ya watu yakiendeshwa kwa misingi bayana, kwa namna ambayo wote wanaona, hakuna vifichovificho, na wakaelezwa utaratibu ni huu, ukawekwa kwa msingi kwamba anastahili kama anavyostahili. Juma anastahili kama Edward anavyostahili, nadhani mambo ya rushwa yatapungua sana nchi hii.

Lakini lazima vilevile kutazama kipato cha wafanyakazi ndani ya serikali. Unawapa uwezo wa kusimamia mamilioni ya fedha wakati unawalipa kipato ambacho hakifanani na kazi wanayoifanya."

Maeneo mengine aliyogusia ni jinsi atakavyosaidia tabaka la wakulima na wafanyakazi livuke, kulitazama upya sera ya ubinafsishaji na kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Niongeze pia tofauti na wanasiasa wengi wa CCM wanaoimba kila uchao wimbo wa amani na utulivu, yeye alitamka kwamba "haitoshi kuendelea kusema tuna umoja, amani na utulivu, ndiyo hii ni hali, tunaitumiaje hali hii kumnufaisha vizuri zaidi Mtanzania."

Sasa katika kujibu swali kuhusu utajiri wake, anasema yafuatayo: "Kuna utamaduni...tumekwisha jenga utamaduni wa kushukiana na tumejenga utamaduni vilevile wa wale viongozi walio na chochote wanaficha. Utaona anaandika jina la ndugu yake au jina ambalo halipo na kujifanya ni maskini kana kwamba kuwa fukura ndiyo kigezo cha uongozi.

Ufukura siyo kigezo cha uongozi wala utajiri sana siyo kigezo cha uongozi pia... Lakini napenda kuhakikisha kwamba mimi sikuficha, hicho nilichonacho ndicho nilichonacho, wala sikionei haya kwa sababu sikukipata kwa njia yoyote ambayo ni ya hilahila hivi au ni ya wizi."

Bila kutaka kuzungumzia utamaduni anaodai wa kushukiana na kuficha mali, kuna tatizo la msingi ambalo lilisababisha kilichokuja kutokea ndani ya CCM muda mfupi baada ya mahojiano hayo.

Sina budi kwanza kurejea maneno ya hivi karibuni ya Lord David Triesman, Waziri wa zamani wa Michezo nchini Uingereza, ambaye aliwashukia vikali viongozi wa Shirika la Kandanda Duniani (FIFA), akisema: "Watu wenye uhitilafu mkubwa ( deeply flawed) wanaiendesha FIFA na watu hao wasingedumu kama kwa mfano, wangekuwa wanaendesha kampuni binafsi au shirika."

Maneno hayo kwangu yanauzito wa kipekee kabisa. Kabla ya kuzungumzia viongozi na uendeshaji wa kampuni binafsi au shirika, kwanza kabisa nasema Lowassa alidhihirisha uhitilafu wake wa kwanza hapo hapo kwenye maelezo kuhusu utajiri wake.

Hivi kama ambavyo tumeaminishwa kwamba Hayati Mwalimu Nyerere alihoji sana mali yake kiasi cha kusababisha aenguliwe, mwanasiasa yeyote makini lazima angemjia juu Mwalimu kwa kuamini maneno ya kuzushi. Lakini yeye hakufanya hivyo kabisa na badala yake wafuasi wake sasa wanajidai leo hii kwamba Mwalimu hakuwahi kutamka hadharani maneno kama hayo. Hili si jambo dogo kabisa.

Tukirudi kwenye viongozi wa kuendesha kampuni binafsi au shirika, ni mwanahabari mkongwe, Jenerali Ulimwengu, aliyetamka kwamba wanaojiita viongozi, wengi wao hata kuendesha kiosk hawajawahi lakini wanakimbilia madaraka makubwa ya nchi.

Nikimtazama Lowassa, ni dhahiri kuwa ni mtu tajiri muda mrefu kwa vigezo vya Tanzania, isipokuwa napata taabu kidogo kama nimwite mfanyabiashara kama ambavyo nilivyozoea kuwatambua wafanyabiashara ulimwenguni. Sijui hata biashara moja kubwa anayoifanya. Vilevile anawaajiri watu wangapi na rekodi yake kwenye kodi nk. Hii ni hitilafu ya pili.

Jambo la tatu lililodhihirisha hitilafu za msingi ni kuhusiana na aina ya usafari wa ndege alioutumia mwaka 1995 kwenda kuchukua fomu za Urais akiwa na Kikwete. Licha ya maneno yaliyotolewa na timu yao ya kampeni pamoja na wenye ndege vilevile ya jinsi walivyokodisha ndege, utumiaji wa ndege kwa kipindi hicho hakika lilikuwa na walakini.

Na hali hiyo ilimpelekea Dk. Rugatiri Mekacha wa Chuo Kikuu cha DSM kuandika kwenye gazeti la RAI maneno mazito kwamba: "Mimi binafsi kwa kweli nimestushwa sana na habari kuwa mtu anayetaka kuwa Rais wa nchi yenye umaskini uliokithiri kama hii anaweza kutumia shilingi millioni mbili kwenda Dodoma na kurudi.

Au ndiyo mbwembwe za kirais? Kama ni hivyo basi Mungu aibariki Tanzania na watu wake maskini.

Jambo la nne lililodhihirisha hitilafu nyingine ya msingi ni kwenye ndoa ya kisiasa na Kikwete. Katika ufuatiliaji wote wa siasa duniani, sijapata kuona uhusiano kama huu wa Lowassa na Kikwete. Nikimnukuu Lowassa: "Tunasindikizana. Tuko pamoja.

Sisi ni vijana, ni wadogo, tunafikiri ni vizuri sisi wawili tushirikiane, two in one, tushikamane tu na baadaye tutakavyoona mbele atakayefanikiwa amefanikiwa mwenzake atamsaidia, atakayekuwa ameshinda na mwenzake ataendelea kuangalia."

Kwenye siasa hakuna kitu kama kusindikizana, pengine kwenye vyuo vikuu. Ikibidi wote wanagombea kwa nguvu zao zote na katika hatua za mwisho basi wanaweza kukubaliana kuhusu nafasi za uongozi. Vilevile hata kama ni muungano wa vyama au serikali ya mseto, ni lazima kuwa na kiongozi. Sasa taarifa zinaonyesha kwamba Lowassa alikuwa juu kabisa ya Kikwete kiasi cha jina lake kuwa miongoni mwa majina manne yaliopendekezwa na UVCCM kugombea Urais. Sasa tena alijushusha kwa mtu ambaye siku nyingi sana anasifa ya kutoaminika sawasawa. Ni kama alivuna alichopanda kwa kuingia kwenye ndoa isiyotakatifu.

Jambo la tano lililodhihirisha hitilafu ya msingi ni yeye Lowassa mwaka 1995 kugombea Urais na Ubunge kwa pamoja. Huu ni ugonjwa wa viongozi wengi sana kwa kweli. Hizi ngazi ni tofauti kabisa kiasi cha mimi kudiriki kusema karibu watu wote kama si wote wanaogombea vyeo hivi vyote viwili wana matatizo makubwa. Ilibidi alenge ama kwenye Urais au Uwaziri Mkuu.

Jambo la sita linalodhihirisha hitilafu ya msingi ni maneno ya mwandishi Johnson Mbwambo wa gazeti la Raia Mwema. Mbwambo aliandika yafuatayo:

"Ni kweli tuna matatizo mengi - kuanzia ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni, ukosefu wa maji safi na salama kwa watu wetu, demokrasia changa, utawala dhaifu nk, lakini, kwa mtazamo wangu, bado tatizo kuu linabiki kuwa ni ufisadi - kuporomoka kwa maadili...

"Na ndiyo maana, binafsi, nampima Lowassa kwa kigezo hicho, na sio wingi wa shule za sekondari za kata ambazo alisimamia kujengwa wakati akiwa Waziri Mkuu!"

Ni jambo la kusikitisha kwamba ukiondoa maneno yake ya hapo juu kuhusiana na rushwa kwenye Wizara ya Ardhi, sina kumbukumbu tena ya yeye kuonyesha kujali tatizo hili sugu. Hii ni kero namba moja kwa nchi nyingi za Afrika na ndiyo maana Mwalimu alihangaika kwenye uchaguzi mkuu wa 1995 kiasi cha kumbatiza Mkapa jina la 'Mr Clean'. Hakumnadi kwamba anafaa kusimamia uchumi wa nchi nk.

Jambo la saba linalodhihirisha hitilafu ya msingi ni kwenye suala la ajira. Pamoja na Lowassa kuzungumzia tatizo hilo tangu miaka 20 iliyopita, cha ajabu ni kwamba alipojibiwa na Waziri wa Kazi kwamba ajira si bomu linalosubiri kulipuka, alijitokeza na kusema hataki kuendelea kulizungumzia kutokana na kueleweka tofauti. Hapo nashangaa sana. Siasa haitaki watu 'wanaoufyata' wakibanwa kidogo tu! Haiwezekani kuwaridhisha watu wote katika mchakato wa kutafuta kura.

Mwalimu Nyerere alisema katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, kwamba "hatuwezi kuachia utamaduni wa woga ukawa ni mbinu au sifa mpya ya uongozi. Na sasa lazima tukiri kwamba utamaduni huu wa woga unaanza kuwa ni sehemu ya tatizo letu la kitaifa.

"Pamoja na mimi kuamini kabisa kuwa Mwalimu alichangia pia katika hilo lakini wanasiasa wetu nao wanachangia sehemu yao pasipo sababu nzuri. Mfano mwingine tu ni adhabu ya kufungiwa kwa wagombea Urais na kamati ya maadili ya CCM. Nilitarajia Lowassa angesimama kidete na kukataa katakata kudhalilishwa na watu wengine waliokuwa wadogo sana kwake akiwa

Waziri Mkuu. Aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, alijaribu kidogo lakini aliishia njiani.

Jambo la nane linalodhihirisha hitilafu ya msingi ni suala nyeti la kutunikiwa nishani. Tumeona kwamba ni yeye Lowassa na Malecela tu miongoni mwa Mawaziri Wakuu wastaafu ambao hawakutunukiwa nishani katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Licha ya ukweli kwamba kuna maswali mengi kuhusu nishani za Tanzania, kukosa kwake ni doa kubwa. Ina maana akiingia jumba kubwa la Ikulu ataanza kwa kujitunuku kwanza? Kuna hatari kubwa ya kutaka kulipa kisasi kwa mtangulizi wake.

Mwisho kabisa, niseme kwamba kipaumbele namba moja tunavyoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu kwa tathmini yangu ni kama ambavyo Balozi mstaafu, Juma Mwapachu, alivyoandika kwenye jarida la CHANGE, Vol.4. la mwaka 1996. Balozi aliandika:

"Haipingiki kwamba Tanzania kwa sasa iko katika hali mbaya kiuchumi na kaulimbiu inayopaswa kutumika ni uokozi wa kiuchumi. Isipokuwa bila kuwa na mfumo wa kikatiba na kisheria ambao si tu unaokubalika kwa mapana bali pia unaoweka mwelekeo wa wazi wa taifa - kijamii, kisiasa na kiuchumi - Tanzania inaweza isitatue na kukabili kwa mafanikio ya kuridhisha maadui wakubwa wa maendeleo, ambao ni umaskini, ujinga na maradhi." (Tafsiri ni yangu).

Adui mwingine mkubwa kwa sasa ni rushwa.
Kuhusiana na mfumo wa kikatiba na kisheria unaokubalika kwa masilahi ya nchi, sikumbuki Lowassa akisisitiza maridhiano ya kitaifa!.

Chanzo:Raia Mwema
 
Mbona urais tunauchukua bila kupingwa,ninachowaambia leo na haya maneno mnanikumbusha baada ya uchaguzi
ccm hana namna nyingine yeyote ile ya kushinda urais bila kumsimamisha lowasa,wakicheka tu ukawa wanachukua dola
 
Mbona urais tunauchukua bila kupingwa,ninachowaambia leo na haya maneno mnanikumbusha baada ya uchaguzi
ccm hana namna nyingine yeyote ile ya kushinda urais bila kumsimamisha lowasa,wakicheka tu ukawa wanachukua dola

nnawashauri nyie wamasai na lowassa anzisheni Chama chenu lakini siyo ccm.
 
nnawashauri nyie wamasai na lowassa anzisheni chama chenu lakini siyo ccm.

chama atakachombea lowasa ni ccm,ukitaka kuamini maneno yangu subiri mwezi wa tano,tumebakiza siku chache tu,kikubwa ni kuomba uzima
 
Ni mawazo yako ila ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa LOWASA ndiye anayetajwa na watu wengi, najua moyo utakuuma ila ndiyo ukweli
 
chama atakachombea lowasa ni ccm,ukitaka kuamini maneno yangu subiri mwezi wa tano,tumebakiza siku chache tu,kikubwa ni kuomba uzima
kwa sababu wanaccm wana price tag mgongoni inawezekana , lakini UKAWA itamtandika vibaya sana mitaani , mkithubutu kutuwekea huyu mmekwisha tena round ya kwanza tu !
 
Hatajwi na watu wengi Anold sema anajitaja kwa Watu Wengi Sana...ila kibaya anajitaja kwa kutumia hela nyingi mnoo..sijui itakuwaje kuppta Rais anayetumia gharama kubwa na marafiki zake katika kuusaka uongozi.!! According to Mwl. Nyerere RIP mtu wa aina hii ni wa kumuogopa kama UKOMA..anyway ngoja tuone na mwisho utakuwaje
 
Nchi haiwez ongozwa na fisadi, kama tuliwachagua katika marais walopita basi tulikuwa wazembe wa kufikiri sasa hivi ni wajanja, twaweza pata Rais Malaya, Rais mpenda kujirusha lakin fisadi hapana,
 
Back
Top Bottom