Uraibu wa mamlaka si tatizo kwa viongozi tu bali hata kwa sisi wananchi

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
250
Nadhani Miongoni mwa matatizo ya makubwa yanayoikabili nchi kwa ni sasa URAIBU wa mamlaka na kupenda kufanya jambo moja kwa muda mrefu bila kuangalia matokeo ya jambo hilo kulingana na manufaa binafsi au wananchi kwa ujumla

Suala la Uraibu ni Pana sana kuanzia ngazi ya viongozi wa mtaa mpaka viongozi wa kitaifa viongozi wamekuwa wakitumia mamlaka vibaya kwa kupoka haki za wanyonge pia hutumia mamlaka ya Uongozi vibaya kwa kujinufaisha binafsi au kwa ajili wakubwa wao.

Uraibu pia hauishii kwenye Matumizi mabaya ya madaraka kwa Viongozi pia linaenda sambamba kwa wanachi pia wamekuwa na Uraibu kuamini kila jambo la maendeleo lazima lifanywe na Serikali bila wao kuchangia chochote.

Wananchi wamekuwa na URAIBU wa kutumia muda mwingi kujadili mambo ya CCM na CHADEMA au Diamond na Alikiba wakati kwa mujibu shirika la kazi Duniani Ukitumia zaidi ya lisaa limoja bila kufanya manake haujazalisha So nimegundua Tatizo la Uraibu limetufanya tuwe na idadi kubwa ya wananchi ambao hawazalishi katika Taifa.

Kimsingi kuna haja sasa ya sisi Wananchi kujitathimini wenyewe ni kiasi gani tutaitumikia nchi yetu. Pia kwa Viobgozi ipo haja ya kutumia Busara, katiba na sheria za nchi ili kuhakikisha tunaondokana na hili tatizo la Uraibu wa madaraka na kupelekea kufanya maamuzi ya haki.

[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#ilovetz[/HASHTAG] [HASHTAG]#maoniyangu[/HASHTAG] [HASHTAG]#Sangujoseph[/HASHTAG]
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,794
2,000
Mleta mada unaonekana umejaza manadharia kichwani. Hivi kazi ziko wapi ili tuzalishe? Mashambani umeona hali ya mvua? Kuna kiwanda kimekosa nguvu kazi? Au kwakuwa uko ofisini basi unajua kila mtu ana ajira kama ww?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom