Uraia wawatesa Watanzania ughaibuni

Uraia wawatesa Watanzania ughaibuni

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Posts
480
Reaction score
644
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Watanzania wengi walio ughaibuni wanaathirika sana na suala la uraia wa nchi mbili. Membe alitoa kauli hiyo mjini hapa jana wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014, ambapo alibainisha kutokuwepo kwa sheria inayoruhusu uraia wa nchi mbili kunawafanya wakose ajira za kueleweka, huduma za afya, elimu na mikopo. Membe alisema kuwa wizara hiyo katika maoni yake kwa Tume ya Katiba ililipa suala la uraia pacha kipaumbele kwa kuwa wanaamini kwamba kufanya hivyo kutawawezesha Watanzania walioko nje kuchangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya nchi.

Kuhusu ziara za viongozi wakuu wa kimataifa kuitembelea Tanzania, Membe alisema kuwa zimefungua milango mipya ya mashirikiano kati yake na mataifa pamoja na kuchochea na kukuza biashara. Mbali na Rais wa Marekani ambaye anatarajiwa kuitembelea Tanzania hivi karibuni, Membe alisema kuwa vilevile kati ya Juni na Julai mwaka huu, Rais wa Sri-Lanka, Mahinda Rajapaksa, na Waziri Mkuu wa Thailand, Yungluck Shinawatra, watafanya ziara rasmi hapa nchni. Nayo Kamati ya Mambo ya Nje katika maoni yake, ilisema kuwa licha ya wizara kukubali manufaa ya kutekeleza ushauri uliotolewa bungeni mwaka jana, mambo mengi hayakufanyiwa kazi kabisa.

“Kwa mfano, kamati ilishauri kuhusu kufanyika kwa mikutano ya mabalozi ili kufanya tathmini na kuboresha masuala mbalimbali ya utekelezaji balozini. “Taarifa za wizara zilionyesha kuwa kwa mara ya mwisho mkutano wa mabalozi Tanzania ulifanyika Zanzibar mwaka 2008. Ni takriban miaka mitano sasa mikutano hiyo haijafanyika, jambo ambalo si jema,” alisema Juma Nkamia kwa niaba ya kamati. Aliongeza kuwa kutokana na maelezo hayo ya matumizi kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ni dhahiri kuwa hali ya majengo ya balozi zetu nyingi inaachwa kuendelea kuwa mbaya na mengine kiasi cha kutisha. “Kwa mfano, jengo la ofisi ya ubalozi wetu huko Brussels Ubelgiji lililonunuliwa mwaka 2004 kwa gharama ya euro milioni 1.5, limechakaa na kuvuja kiasi cha kusababisha baadhi ya kuta kutoa harufu mbaya na kuiaibisha nchini yetu,” alisema.

Source: CHADEMA DIASPORA : Uraia wawatesa Watanzania ughaibuni
 
Wapitishe tuu uraia wa nchi mbili wanaogopa nini?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkafie mbele mamluki nyinyi! Hatutaki mambo yenu ya Kiliberal huku TZ, Huku ni mwendo wa ku conserve na Ujamaa.
 
Mkafie mbele mamluki nyinyi! Hatutaki mambo yenu ya Kiliberal huku TZ, Huku ni mwendo wa ku conserve na Ujamaa.

Watanzania tuko nyuma mno katika mambo mengi, tuko radhi kuwakaribisha wageni wanaobeba rasilimalizetu badala ya wazawa wenye uchungu wa kuwekeza walivyovichuma huko kwao. Hata biashara zitashamiri vizuri kwa vile hao wanapenya kote kote bila usumbufu kuliko gharama za sasa.

Wakiruhusu hilo mimi naenda kuchukua urai kwa wale jamaa nipate uraia pacha, chezea nini,
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Membe peleka muswada wa kuruhusu uraia wa nchi mbili bungeni sasa kama unataka ku-'make headway'..
 
Ili iwe rahisi mafisadi mkiiba unachomoa passport yako ya switzerland uyooo unasepa nadhani viongozi wote na familia zao watachukua dual citizenship,au basi mtu akiwa na dual uraia asiruhusiwe kuserve jeshini,usalama wa taifa,serikalini na kwenye nafasi za siasa imagine kua na rais ambaye pia ni raia wa china!!
 
Hili la uraia wa nchi mbili binafsi huwa nina wasiwasi nalo sana, bado sijajua kwa nini ni baadhi tu ya wanasiasa ndio wanalishupalia...sasa sijajua ni kwamba kuna jambo lapigiwa upatu kwa mgongo wa dual citizenship au kuna mengineyo ambayo hayajawekwa bayana bado?
 
Watanzania tuko nyuma mno katika mambo mengi, tuko radhi kuwakaribisha wageni wanaobeba rasilimalizetu badala ya wazawa wenye uchungu wa kuwekeza walivyovichuma huko kwao. Hata biashara zitashamiri vizuri kwa vile hao wanapenya kote kote bila usumbufu kuliko gharama za sasa.

Wakiruhusu hilo mimi naenda kuchukua urai kwa wale jamaa nipate uraia pacha, chezea nini,

Acha kudanganya na kupotosha watu, hakuna kitu chochote kinachowazuia Watz waishio nje ya TZ wasiwekeze TZ kwa sasa, hilo swala la Uraia wa pacha hata likiruhusiwa hakutakuwa na tofauti yoyote ile, mbona Wageni kibao wamewekeza TZ na wanatoa ajira kwa Watz na hawana Uraia wa Tanzania?

Kama wewe unauwezo wa kuwekeza TZ ni vipi kuwa au kutokuwa na Uraia wa TZ kukuzuie? Nyie semeni Uraia wa Nchi mbili utawasaidieni ninyi na Familia zenu labda kwa kuwa mtaweza kuishi huku na kule, lkn kusema kwamba kutokuwapa Uraia wa nchi mbili nchi haitanufaika ni UONGO na hiyo sababu haijitoshelezi!

 
Membe alitoa kauli hiyo mjini hapa jana wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014, ambapo alibainisha kutokuwepo kwa sheria inayoruhusu uraia wa nchi mbili kunawafanya wakose ajira za kueleweka, huduma za afya, elimu na mikopo. Membe alisema kuwa wizara hiyo katika maoni yake kwa Tume ya Katiba ililipa suala la uraia pacha kipaumbele kwa kuwa wanaamini kwamba kufanya hivyo kutawawezesha Watanzania walioko nje kuchangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya nchi.
Kwani hapa kuna uongo wowote? Pale Denmark nani mwenye haki zaidi ya ajira,elimu,huduma za afya n.k, Mtanzania au Mdenmark? Hii itapunguza wimbi la Watanzania 'kujilipua' wakijiita Warundi, Wanyarwanda,Wakongo au Wasomali.. Pia tusisahau 'Diaspora remittances' ni muhimu kwa maendeleo ya nchi nyingi za Kiafrika..Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia $401 Bilioni zilienda kwenye nchi zinazoendelea mwaka 2012.
 
Acha kudanganya na kupotosha watu, hakuna kitu chochote kinachowazuia Watz waishio nje ya TZ wasiwekeze TZ kwa sasa, hilo swala la Uraia wa pacha hata likiruhusiwa hakutakuwa na tofauti yoyote ile, mbona Wageni kibao wamewekeza TZ na wanatoa ajira kwa Watz na hawana Uraia wa Tanzania?

Kama wewe unauwezo wa kuwekeza TZ ni vipi kuwa au kutokuwa na Uraia wa TZ kukuzuie? Nyie semeni Uraia wa Nchi mbili utawasaidieni ninyi na Familia zenu labda kwa kuwa mtaweza kuishi huku na kule, lkn kusema kwamba kutokuwapa Uraia wa nchi mbili nchi haitanufaika ni UONGO na hiyo sababu haijitoshelezi!


Si kitu cha ajabu kupata maoni tofauti kama ya kwako. Kwa wenye uelewa wa Diaspora wanajua nini maana ya dual Citizenship wakati mtazamo wa wengi kama mimi nisiye na upeo ni kuona kama kuwanufaisha hao badala ya kuangalia namufaa ya kiuchumi kitaifa.

Watanzania walio na uraia wa nchi nyingine hawana uhuru wa kuingia nchini mwao Tanzania kwa uhuru kama wazawa ila kwa visa, na wengi nimewasikia wakilalamika kila watakachokusudia kufanya hufikia kunyanyaswa napengine hata kunyimwa kwa sababu tu wamechukua uraia wa nchi nyingine tofauti na wageni wa kuja wanavyotetemekewa. Hiyo ndiyo hali halisi.

Watanzania katika ulimwengu huu wa kutumia matunda ya wenzetu wenye nafasi ya kuingia huku na kule kwa manufaa ya nchi tuko nyuma sana na pengine hali ya wivu ndiyo inayoturudisha nyuma na kuona wageni wa kuja ndio wakuenziwa kuliko wazawa wa nchi hii.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu huu uDC hauna maslahi kwa Mafisadi ndani ya Serikali na CCM hivyo hauna kiupambele chochote. Watakwambia hawa wamekosa uzalendo hivyo kuikimbia nchi wakiruhusiwa wataongeza ujambazi nchini. Wakati nchi za majirani zetu kama Kenya, Uganda, Rwanda, South Africa n.k. ambako kote uDC unaruhusiwa ujambazi haujaongezeka kutokana na kuruhusu uDC. Ukichukua uraia wa nchi za nje unaonekana si mzalendo wakati wale wanaoficha $5.9 Billion kule Uswiss ndio wanaonekana Wazalendo wa kutupwa!!!!

Si kitu cha ajabu kupata maoni tofauti kama ya kwako. Kwa wenye uelewa wa Diaspora wanajua nini maana ya dual Citizenship wakati mtazamo wa wengi kama mimi nisiye na upeo ni kuona kama kuwanufaisha hao badala ya kuangalia namufaa ya kiuchumi kitaifa.

Watanzania walio na uraia wa nchi nyingine hawana uhuru wa kuingia nchini mwao Tanzania kwa uhuru kama wazawa ila kwa visa, na wengi nimewasikia wakilalamika kila watakachokusudia kufanya hufikia kunyanyaswa napengine hata kunyimwa kwa sababu tu wamechukua uraia wa nchi nyingine tofauti na wageni wa kuja wanavyotetemekewa. Hiyo ndiyo hali halisi.

Watanzania katika ulimwengu huu wa kutumia matunda ya wenzetu wenye nafasi ya kuingia huku na kule kwa manufaa ya nchi tuko nyuma sana na pengine hali ya wivu ndiyo inayoturudisha nyuma na kuona wageni wa kuja ndio wakuenziwa kuliko wazawa wa nchi hii.
 
Si kitu cha ajabu kupata maoni tofauti kama ya kwako. Kwa wenye uelewa wa Diaspora wanajua nini maana ya dual Citizenship wakati mtazamo wa wengi kama mimi nisiye na upeo ni kuona kama kuwanufaisha hao badala ya kuangalia namufaa ya kiuchumi kitaifa.

Watanzania walio na uraia wa nchi nyingine hawana uhuru wa kuingia nchini mwao Tanzania kwa uhuru kama wazawa ila kwa visa, na wengi nimewasikia wakilalamika kila watakachokusudia kufanya hufikia kunyanyaswa napengine hata kunyimwa kwa sababu tu wamechukua uraia wa nchi nyingine tofauti na wageni wa kuja wanavyotetemekewa. Hiyo ndiyo hali halisi.

Watanzania katika ulimwengu huu wa kutumia matunda ya wenzetu wenye nafasi ya kuingia huku na kule kwa manufaa ya nchi tuko nyuma sana na pengine hali ya wivu ndiyo inayoturudisha nyuma na kuona wageni wa kuja ndio wakuenziwa kuliko wazawa wa nchi hii.

Katika Nchi zote zilizoenedelea na zinazoendelea sasa kwa kasi, sijawahi kusikia mahali wamesema kwamba kukua kwa Uchumi wao kumechangiwa na Raia wao kuwa na Uraia 2, ila zinatajwa sababu nyingine kabisa, ambazo ndio sisi tunapaswa tuziangalie na sio kupoteza muda kujadili na kujaribu kubadili mfumo wetu ili kuwafurahisha watu ambao wameondoka nchini kwa utashi wao wenyewe!

Kama TZ ingekuwa na vita kama Rwanda au Somalia ningeelewa kwa kuwa watu walikuwa hawana jinsi bali kuondoka kuokoa Maisha yao na mali zao, lkn hawa wameondoka wenyewe sasa kwa nini sisi tupoteze muda na Fedha zetu za kodi kujaribu kuwafikiria?

Kama wanataka kuwekeza watawekeza tu bila ya kuwa na Uraia 2, Wazungu, Waarabu, Wahindi, Wasomali ndio wawekezaji wakubwa TZ na hawana Uraia 2, hivyo hoja yao haina mshiko!

Tuwekeze nguvu zetu kwenye kusaidia kuwainua Watz wanaoishi TZ hao wa nje hawatuhusu na ndio maana kuna Ubalozi huko wa kuwashughulikia, tusije kuwa kama Wakenya wanamlilia Obama wakati yeye hata time nao hana!

KIPAUMBELE KWA WATZ WAISHIO TANZANIA KWANZA!
​

 
Mbona hili tatizo limeshamalizwa kimya kimya?

Unachukua uraia wa kwenye maboksi na kwa vile wao wanatambua uraia pacha basi wewe unakuwa huna haja ya kuukana uraia wako wa kibongo.

Unautumia Uraia wako wa kwenye maboksi kwenye kazi zinazohitaji uraia, kusafiri nchi bila ya viza nchi nyingi duniani na wakati ukija Tanzainia unachomoa pasi yako ya kibongo ili kukwepa gharama za viza na inakusaidia kukaa zaidi ya miezi mitatu.

Vinginevyo uraia wa kigeni pekee unakuwa ni gharama kubwa sana kwa mtu mwenye familia, tuseme mtu mwenye mke na watoto wawili zitawatoka $200 kwa ajili ya viza za kuingilia na ikitokea kuwa ni mtu anayetoka sehemu za mipakani mwa Tanzania na ana ndugu upande wa pili basi zitamtoka $ 200 yeye na familia yake kwenda mfano Kenya! siku wakirudi TZ zitawatoka tena $200 nyingine kama hawajachukua double visa mara ya kwanza walipoingia! tunazungumzia $ 600 kwa ajili ya viza tu!

Ubaya mwingine ni kuwa una miezi mtatu tu ikiisha inabidi u-renew! ...muhimu ni kuchukua uraia wa kwenye maboksi halafu usiukane Utanzania ambao utakuja kukusaidia wakati wa kuingia nchini.
ni hay tu.
 
Back
Top Bottom