Uraia wa nchi mbili ni muhimu kwa maslahi mapana ya taifa

masterzero

Member
Feb 11, 2015
36
37
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana na Mungu tuna fursa nyingi za kazi na malengo mapana ambayo yanahitaji mabilioni ya dola kutekelezeka haraka kwa kuwa issue ya viwanda imepewa kipaumbele sana itakuwa ni vyema kuangalia nchi zenye viwanda zilifanikiwa vipi/kufikia malengo yao.

Marekani nchi zote za barani Ulaya, South Africa, South Korea uae(Dubai)zote zinaruhusu uraia wa nchi mbili kwa kuwa unavutia sana wawekezaji watakao kuja kuishi Tanzania huku wakiwa ni watanzania menye haki kama mtanzania yeyote wanakuwa huru kukopa mabenki ya Tanzania na kukopa benki walizotoka.

Watanzania waliokuwa na uraia wa nchi yeyote ya nje watapata fursa ya dhahabu ya kuwa raia tena wa Tanzania huku wakibakiwa na uraia wao wa nje itakuwa ni motisha kwao kile wanachochuma kule ulaya marekani Arabuni kukirudisha Tanzania na kukiwekeza hivyo kusaidia mzunguko wa pesa kuwa wa kasi zaidi

UKIZINGATIA MASHARTI YA MUWEKEZAJI NI MAGUMU NAYANAHITAJI MTAJI MNENE NA WENGI HUWA MATAPELI WASIOKUWA NA NIA NJEMA NA TAIFA LETU

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Magufuli
IKIWEZEKANA ATAWALE HATA MIAKA SITINI NA TANO!
HAPA KAZI TU BABA
 
Back
Top Bottom