Uraia pacha umezibeba team nyingi AFCOM

Uraia pacha umezibeba team nyingi AFCOM

one by one

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
5,835
Reaction score
9,330
Nimejaribu kuangali team nyingi nazoweza kusema zinaonesha mafanikio kila miaka ni zile zinazoruhusu raia pacha. Ukiangalia kama jana team ya Algeria karibia wote wamezaliwa France na baadae wakaamua kuchezea team zao za asili kuna mwingine tena sio hata muislamu sababu ya mama yake kaamua kucheza Algeria na anapewa nafasi na wanaonesha ubora na kuitangaza nchi. na team kama Mali, Tunisia, Ivory coast, Morocco, Senegal, Nigeria, Ghana na wengine hawa super power wa mpira wa Africa wanaruhusu raia pacha. team nyingi ambazo hazina uraia pacha zimepata tabu japo inaweza kuwa sio wote. nchi kama Kenya ndio wameanza uraia pacha naamini kama labda ingekuwa wameanza mapema labda Origi angeamua kuchezea Kenya. sasa kwa trend hii ukweli hatuwezi kuja kuwafikia hawa sababu kuna kizazi kingine huko wanaanza kuwa wachezaji siku wakiona chance yao ya kufanikiwa kucheza team ya taifa huko wana switch team ya asili kama yule kijana jana aliyetupiga goal 2 yuko Napoli, alichezea France under 20 baadae akaamua kuchezea Algeria. Mimi kwa style hii nadhani tusahau kushindana na hizi team na siku tukiweza itakuwa jambo la mara moja tu wao watabaki kuwa juu. sisemi turuhusu uraia pacha haya ni mambo ya siasa lakini kwa kuangalia wale wachezaji itakuwa shida sisi kuwafikia maana huko wanakotoka wanakuwa katika mazingira mazuri ya kimpira na wanapata nafasi kucheza vilabu vya huko kirahisi baadae wanakuja kusaidia team ya taifa zao. sisi tuombe wengi watoke kama kina Mbwana na kupata nafasi mitihani kweli kwa hiyo tukubali matokeo tu tutegemee kupata wacheza sijui Lipuli, Mbao na wengine wenzetu wanawatoa ready huko katika league za nje. Haya ni maoni yangu baada ya kuwasoma wengi ya hawa wachezaji wametokea wapi?
 
Uraia pacha una faida sana lakini ubinafsi wa viongoziwetu unatufanya taifa kuchelewa kupiga hatua katika mambo mengi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom