Mimi nilihapa kutofanya tena urafiki na mademu wa kibongo zaidi ya kupeana gegedo tu. Kuna kipindi nilikutana na mwanamke mmoja tulikuwa tunasoma University siku za nyuma. Tulifurahi kukutana tena, tukaanza urafiki wa kishikaji huku tukikumbushana ya chuoni na baadhi ya vituko vya chuo na marafiki zetu. Yakawa mazoea ya ukweli kama kaka na dada hivi. Bahati mbaya ikaja, kila huyu dada nikimualika mtoko LAZIMA atakuj na marafiki zake, au anaweza kunipigia simu ananiambia wikiendi anakuja, kumbe anakuja hajajiandaa (kama kuleta msosi wa mchango), utashitukia huyo kaja na timu nzima na kuuliza tunapika nini hao wenzangu wanakunywa Konyagi au Heineken. Nilikuwa naumia sana moyoni ila nilikuwa sina ubavu wa kumfukuza, mwanamme ilibidi nijikaze tu na kuingia hasara ya kufariji wageni nisiowajuwa na wasio na faida kwangu. Siku nikapanga mpango na demu wa pale mtaani kusingizia kuwa yeye ni demu wangu...nilimsimulia huyu demu kila kitu kuhusu huyu rafiki wa chuo jinsi anavyonitumia, akakubali kumkomesha kiaina. Siku aliyokuja yule rafiki wa chuo acha apandishiwe na kukunjwa kuwa anamuiba mchumba mtarajiwa, aisee nilifurahi kishenzi na kuacha yule demu anakunjwa maana nilijifanya sina nguvu ya kuingilia. Baada ya majirani kuingilia ndipo akaachwa yule demu na kuondoka hapo hapo. Usiku ananipigia simu na kunigombeza kwanini sikumuhusisha kuchagua mke mzuri eti nikiendelea na yule angenitia hasara siku za mbeleni. Nikamjibu tu yeye ni chaguo la moyo wangu na ndio ukawa mwisho wa urafiki wetu. Kwa sasa nina watoto wawili na demu aliyenifundisha maujanja ya kufukuza demu hasara.