Urafiki wa Julius Nyerere na Zuberi Mtemvu

Urafiki wa Julius Nyerere na Zuberi Mtemvu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
URAFIKI WA JULIUS NYERERE NA ZUBERI MTEMVU

Kuna mambo mengi nimeyasikia udogoni kuhusu wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika ambayo kwa wakati ule sikujua kuwa ni mambo yatakayokuja kuwa muhimu na watu watapenda kuyafahamu kwa kina.

Katika video moja kuhusu nguvu ya TANU na jinsi chama kilivyokuwa kinashinda kila uchaguzi Mwalimu anaeleza uchaguzi wa Rais wa mwaka wa 1962 alioshindana na Zuberi Mtemvu wa Rais wa Congress.

Nyerere katika video hiyo anamwita Mtemvu "rafiki yake."
Kweli walikuwa marafiki.

Lakini kabla sijakwenda mbele ngoja niseme kitu.

Mimi nimezaliwa Mtaa wa Kipata na Zuberi Mtemvu akiishi Mtaa wa Somali (Sasa Mtaa wa Omari Londo).

Hii mitaa imekaribiana sana na wakazi wake wakifahamiana.

Mama yangu Bi. Mwanaidi bint Mohamed nimemsikia akisema kuwa siku zote alikuwa yeye akikutana na Mtemvu watazungumza Kiluguru.

Mama yangu akizungumza lugha zote mbili Kiluguru na Kizaramo na sababu ni kuwa baba yake Sheikh Mohamed Mvamila alikuwa Mzaramo na mama yake Bi. Mwatum bint Rajabu alikuwa Mluguru.

Turudi kwa Mtemvu.

Mtemvu alifahamiana na Nyerere wakati ule ule Nyerere alipojuana na Abdulwahid na Ally Sykes.

Nyumba ya baba yake Mtemvu, Mzee Mwinshehe Mmanga Mtemvu, Mtaa wa Somali haikuwa mbali na nyumba mbili za ukoo wa Sykes, nyumba ya Bi. Mluguru bint Mussa mama yao Abdul, Ally na Abbas Mtaa wa New Street (Sasa Lumumba Avenue) na nyumba ya Mzee Kleist ya Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Kleist Sykes).

Mwalimu alipotaka Zuberi Mtemvu aache kazi serikalini na kujiunga na TANU kama Secretary General ilibidi azungumza na baba yake Mtemvu, Mzee Mwinshehe kwanza kupata idhini yake.

Kuna mengi kati ya marafiki hawa wawili siwezi kueleza yote hapa kwa kuchelea kumchosha msomaji.

Nitalieleza hili moja.

Safari ya kwanza ya Nyerere ndani ya TANU alikwenda Morogoro akiongozana na Zuberi Mtemvu kuzungumza na wazee wa Morogoro.

Katika barua Mtemvu aliyomwandikia Ally Sykes anasema wazee wake hawakuwa tayari kuunga mkono TANU.

Nyerere na Mtemvu yaani President wa TANU na Secretary General walikuwa na kawaida ya kunywa chai pamoja asubuhi Cosy Cafe.

Yapo mengi sana.

Mzee Mtemvu siku za mwisho wa maisha yake alikuwa mzungumzaji wangu mkubwa na nilichota mengi kutoka kwake.

1754575114470.jpeg

1754575184188.jpeg

1754575246280.jpeg

1754575287230.jpeg


Picha:
1. Zuberi Mtemvu akiwa President wa Chama cha Congress (1958 - 1964).
2. Zuberi Mtemvu aliyeshika tama chini kulia ni Sheikh Suleiman Takadir kushoto ni John Rupia ambae kamziba Julius Nyerere tawi la TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni nyumbani kwa Ali Msham.
3. Gazeti la Mwafrika 11 Oktoba 1958 ukurasa wa mbele ukiwaonyesha waliofukuzwa TANU: Zuberi Mtemvu, Sheikh Suleiman Takadir, S. K. George na Patrick Kunambi.
4. Zuberi Mtemvu na Bibi Titi Mohamed siku Mtemvu aliporudi TANU pamoja na Said Chamwenyewe na wanachama wengine wa Congress.
 

Attachments

  • 1754575319720.jpeg
    1754575319720.jpeg
    305.8 KB · Views: 27
  • 1754575370797.jpeg
    1754575370797.jpeg
    305.8 KB · Views: 26
Kumbe Waislamu siasa za Dini hawajaanza leo.
 
Back
Top Bottom