Kuhusu namna ya kuwa na furaha, nakumbuka mwanandishi mmoja wa Kiyahudi (jina nimesahau), alisema "Kitu pekee cha kukufanya uwe na furaha ni kazi na marafiki". Hakutaja wapenzi wala familia. Nadhani kwa sababu wapenzi na familia mara nyengine wanaweza kutusaliti, watoto na wapenzi wanaweza kukutoka, ama kwa sababu wana maisha yao, wanaweza kuwa mbali nasi na si kila kitu tunapaswa kuwaeleza wao; Mungu anaweza kuwahitaji au wakaamua kutuwacha. Wanaokuwepo karibu yako siku zote ni rafiki zako na kazi au amali yako.
Ushauri wangu kwa hivyo ni kuwa kukimbilia kwa rafiki mkweli na mwaminifu wa kuongea naye, angalau kwa kutoa dukuduku lako. Huyu atakushauri na kukupa moyo. Si pombe, wala ngono kama walivyoshauri wengi.