Upweke Dawa Yake nini?

Kaka mambo yote haya ndio kaomba kwenye content ya thread yake🥺😂😂😂. Sijamalizia kuisoma.
 
Kuna mambo mawili ambayo yanakosekana kwenye mahusiano mengi ya Bongo. 1. Urafiki: kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na mpenzi na kuwa na mpenzi +rafiki! Wengi mahusiano yao ni ya ''wapenzi'' tena waliotamaniana (ngono), na siyo wapenzi wanaopendana na kuwa marafiki. Wewe unatakiwa upate mpenzi+rafiki na siyo mpenzi. Mpenzi rafiki ni yule mnayeaminiana na kupeana siri za ndani. Jambo jingine linalokosekana kwa wapenzi wngi wa kibongo empathy. Empathy ni ile hali ya mtu kujali mwingine kiasi ambacho akipatwa na tatizo, mwenzake anahisi ni kama yeye ndiye kapatwa. Kwa Bongo, ni changamoto sana kupata wapenzi au wenzi wenye sifa zote mbili na ndilo tatizo linalokukabili. Bado mambo yangu hayajakaa vzr, ningekutafuta kwa sababu nina hizo sifa!
 
Mmmmh wanaume Nyie Nyie

Mtu akifunguka si mnamlabel “malaya”?
Tatizo la Bongo mwanamke akifunguka wanaume wengi hutumia huo mwanya kutimiza malengo yao ambayo mengi yanakuwa na tamaa ya ngono. Mtu wa kufunguka inabidi umsome kwa muda sana.
 
Wewe inabidi ukutane na Mimi nisiyekuwa na mambo mengi.Make mi napenda sana peace na sehemu tulivu sana ndo maana sikauki Slip way nicheki Bahari tu ila nadhani tungekutana ingekuwa faida.
 
Tatizo la Bongo mwanamke akifunguka wanaume wengi hutumia huo mwanya kutimiza malengo yao ambayo mengi yanakuwa na tamaa ya ngono. Mtu wa kufunguka inabidi umsome kwa muda sana.
Wanawake wanafunguka vizuri tu watu wapo wametulia ...Tatizo ni kwamba wanawake hawana moyo wa kukubali rejection kama wanaume.

Visa atakavyomfanyia mwanaume kama atamkataa ni hatari zaid na pia mtamchukia milele.

Kuna huu ukweli mwanamke binafsi akikupenda na kashindwa kukuambia ikipita kipind kirefu na wewe hauna time naye ni mawili atakupakazia au kukuchukia ili mradi tu.!!
 

Umemaliza kila kitu. Sasa tunatokaje hapo na jamii hii tuliyomo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…