Upunguzaji wa ghrama za kulisha kuku kipindi hiki kigumu

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,872
9,261
UPUNGUZAJI WA GHARAMA ZA KULISHA KUKU KIPINDI HIKI KIGUMU KABISA.
15965960_1367718033272371_5506445511535010650_n.jpg

Ni ukweli kwamba gharama za vyakula vya kuku viko juu sana na gharama hizi huchukua asilimia 80 ya gharama zote za matunzo ya kuku.

Yaani unapo kokotoa gharama za matunzo ya kuku basi chakula huchukua asilimia 80 ya gharama zote.

Na hii imekuwa inaumiza sana wafugaji wa kuku kiasi kwamba wamekuwa wakijikuta wanatumia gharama kubwa sana na faida inakuwa kidogo sana.

Kipindi tulichopo kwa sasa ni kipindi kigumu sana tena mno, kaisi kwamba wengine wetu either tutaacha kufuga kwa sababu ya gharama kubwa hasa kwenye chakuka.

Hiki ni kipindi ambacho bei hasa ya mahindi iko juu sana na kumbuka kwamba mahindi ndo malighafi namba moja kwa kutengeneza chakula cha kuku,

Kuku hawajui cha kiangazi, wala masika wao wanapiga tu msosi kwenda mbele.

NINI CHA KUFANYA?
1. Hakikisha upotevu haupo kabisa, kama ni vijana wa kazi wasimamie kuhakikisha hakuna hata punje moja inadondoka chini.

Hapa hakikisha pia vyombo vyako havimwagi chakula hovyo, na chakula kisijazwe hadi juu, make kinapotea kingi sana kwa staili hiyo.

2. Wapatie kuku maji kwa wingi sana yenye vitamini ili saa zingine maji yakafidie chakula wanacho kula. maji ni muhimu sana kwe kuku, na anaweza kaa hata siku 3 bila chakula lakini si maji.

3. Chakula mbadala
Huu ni wakati hasa wa kudili na chakula mbadala, kama kuku wako sio wengi sana basi walishe cgakula asubuhi na mchana wapatie majani pekee, watafutie mboga za majani au mabaki ya matunda kama tikitiki maji na pia maboga, Kuku wanaweza ishi kwa mtindo huu kwamba watakula asubuhi na mchana watakula majani kwa wingi, hapo utakuwa umeokoa kiasi cha chakula.

4. Ondoa kuku wote un productive
Chambua kuku ambao hawana uzalishaji na waondoe faster bandani, kagua na pima kujua ni kuku wapi wana taga na wapi hawatagi,
Unaweza ukawa na Layers 400 kumba kati ya hao wanao taga ni 320 pekee na wengine wanakutia hasara kwa kula bure, sasa ni wakati wa kuwoandoa,

Usiendelee kulisha kuku wa mayai wasio taga, labda tu wanao karibia kutaga lakini kama ni tasa au walisha choka kutaga basi usiendelee kuwapiga misosi ilihari utagaji wao usha fika mwisho.

5. Wapige pasi ndefu kwa wiki mara mbili au 3.
Hii inaruhusiwa kitalamu, siku zingine unaweza walisha asubuhi pekee na mchana wakapiga dash. hii inaweza fanywa kwa wiki mara 3 kulingana na kuku.

6. KUKU WA NYAMA
Hakikisha una mteja pembeni kipindi hiki, ili basi wakifikia bei ya soko ni kuwatoa faster na usiendelee kuwalisha itakuwa ni hasara kubwa sana.

7. Mahindi si yamepanda Bei?

Why Mayai, kuku bei ibakie kama mwanzo? ni wakti sasa wakupandisha bei ili basi ufudie gharama za chakula, haitakuwa na tija kuendelea kuwalisha kuku kwa gharama kubwa na kisha kuwauza kwa bei ya chini sana.

8. Loweka chakula cha kuku
Hii ni aplcable kwa kuku wa mayai na hawa chotara, chakula chao kinaweza lowekwa na ukifanya hivyo kuku hupunguza kiwango cha ulaji, kama walikuwa wanakula Gram 140 kwa kuku mmoja basi kuku anaweza kula gram 100, hii ni kwa sababu kuna virutubisho huongezeka, ila inahitaji elimu kufanya hivyo.

Yangu ni hayo tu Wadau

Chasha Farming- 0767-69-10-71
 
Asante sana mkuu, hili ni somo Mujarabu kabisa, hasa kwa kipindi hiki. Leo asubuhi nimeumia sana kuona kijana amemwaga chakula cha kuku hovyo. Hajui majira tuliyomo. Asante sana.
 
mkuu, ungefafanua vizuri juu ya kuloweka chakula cha kuku maana hata mimi nafuga ndugu.

Kuku wanakula kupindukia mkuu, ukicheza wanakuangusha chini.

Alafu ukienda mtaani wateja wanakudengulia mayai.

Yaani unaweza kumnasa mtu makofi, maana hajui dhahama inayotupata kuwalisha mpaka watage mayai.

Watanzania tubadilike tuache mashauzi kwenye Biashara za watu.
 
ki ukweli hali kwa sasa ni mbaya hata kuku aliekua anataka kuatamia mayai amehairisha zoezi ilo. nachoshukuru kuku wangu wanapenda majani kushinda pumba za mahindi, nawapa chenga za dagaa ,wanakula kidogo na kukimbilia sehemu majani ya mbigiri yameota nasikitika kwani yanaisha sasa.
 
8. Loweka chakula cha kuku
Hii ni aplcable kwa kuku wa mayai na hawa chotara, chakula chao kinaweza lowekwa na ukifanya hivyo kuku hupunguza kiwango cha ulaji, kama walikuwa wanakula Gram 140 kwa kuku mmoja basi kuku anaweza kula gram 100, hii ni kwa sababu kuna virutubisho huongezeka, ila inahitaji elimu kufanya hivyo
Hii njia inafanya kazi kwa kuku wa nyama, hebu fafanua kiasi tafadhali
 
Nashukuru sana Mkuu, kwa kunifungua Macho na Masikio..nilikuwa najiuliza siku zote, ni mimi ama wife, aliye/anae shindwa kutimiza wajibu wake...!!

Kuku wanamaliza chakula, zaidi ya kutaga Mayai, kufidia gharama za malezi na matunzo...!!

Nimefikia hatua nikajiuliza, nani ni Mfalme kati yangu na mifugo (kuku) ninao wamiliki..!!

Nahangaika na Chakula pamoja na kuwatengea Maji safi ya kunywa...!

Mwisho wa yote , nikitazama Mayai na watoto walio Anguliwa (tagwa/kuzaliwa) najikuta sioni faida ninayo pata..!!

Wafugaji NGULI wanasema, faida ya UFUGAJI ilikuwa zamani..
 
Back
Top Bottom