Upungufu mabasi ya mwendokasi, mengi mabovu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
da4e36161484d5e6b7e2632b7db47c51

Dar es Salaam. Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), imesema kuna uhaba wa mabasi yanayotoa huduma na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa usafiri huo.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano Aprili 10, 2019 kwa vyombo vya habari na Meneja Uhusiano wa Umma wa Dart, William Gatambi imesema uhaba huo unatokana na mabasi hayo kupata hitilafu mbalimbali.

“Idadi ya mabasi yanayotoa huduma leo katika mfumo wa Dart ni 85, huku 58 yakifanyiwa matengenezo makubwa na madogo.

“Tunawaomba wateja wetu kuwa na subira wakati mabasi hayo yakifanyiwa matengenezo. Tunawaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza,”amesema Gatambi.

Aprili 5, mwaka huu mtendaji mkuu wa Dart, Ronaldo Lwakatare alisema kipindi cha mpito cha uendeshaji wa mradi huo kimewapa funzo kubwa kutokana na changamoto zilizojitokeza.

Alisema katika kipindi hicho wamekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uchache wa mabasi tofauti na matarajio hali inayosababisha abiria wanaotumia mradi huo kupata adha ya usafiri huku baadhi yao wakilazimika kutumia muda mrefu kukaa vituoni kuyasubiria mabasi hayo.

Lwakatare alisema kwa sasa mradi huo una mabasi 140 yanayotoa huduma badala ya 300, lakini bado wanakumbana na changamoto kwa robo ya mabasi yaliyokuwapo kuwa mabovu hata hivyo wanashirikiana na mtoa huduma hiyo kampuni ya Udart.

“Mabasi mengi ni mabovu na yanapita katika kipindi kigumu. Lakini Dart inashirikiana na Udart kuhakikisha yanatengenezwa ili kurejea barabarani na hatimaye huduma iwe ya kawaida,” alisema Lwakatare.
 
Jf sio ya kuchezea aisee..Tumelijadili hili suala kwa wiki sasa na salamu zimewafikia wahusika.
Msimamo wetu wana JF ni kwamba ile ahadi ya Waziri Jafffo ya kupatikana kwa muendeshaji mwenza wa mradi wa mabasi imefikia wapi maana alikaririwa akisema kwenye mwezi Machi 2019 angeanza kazi hadi leo kimya na wala Serikali haijasema chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni kushinikiza kuachiwa kwa mabasi kule bandarini bila kulipiwa kodi, hilo haliwezekani! Kama mtoa huduma kashindwa kazi atafutwe mwingine.
 
Zikitunzwa nankufanyiwa service stahiki hazina breakdown za kijinga kama basi za mchina,nishawahi panda Higer ya mkoani ilikatika gear shift stick tumetoka iringa kuja dar. Sijawahi ona breakdown ya aina toka nizaliwe.
Ununue Benzi halafu yaje yakae juu ya mawe kwa ughali wa spea? Injector pump ya engine utaambiwa milioni 30 au 40, si uchizi huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
58 out of 140 ni mbovu na viongozi bado wako ofisini. What a shame.
Kwanini uongozi usijiuzulu watu wenye akili waendeshe huo mradi?
 
Mpaka yanafikia 58 mabovu walikuwa wapi kuyatengeneza siku zote,au yaliharibika yote kwa siku moja?huu ni uzembe...
 
1067846

Ongeza na hili.Njoo kwenye sifa zetu sasa za kiuendeshaji hasa ngozi nyeusi.Roho mbaya...chuki...uchawi na kutokuwa na mipangalio na mahitaji na vipao mbele.Ndio kunapelekea huo mradi kufa taratibu.Kuna watu tayari wametajirika kwa Nauli za hayo mabasi wakisahau matengenezo na Ununuaji wa magari hayo.Hapo kuna fitna pia zisizo na msingi.
Huo mradi hakika ungekaa watu makini kiakili wangepiga pesa mingi mno mpaka waseme baasi.Hakuna raia ambaye asingeaacha kupanda kwa sababu ungekuwa bora kukicha.Lakini wapi..Hapo ndio utaamini jinsi tulivyo na mapungufu mengi kiuendeshaji watanzania waliopewa dhamana hiyo hawatoshi kutimiza.Wanachosubiri ni kusikia watu wanafia kwenye hayo magari ndio waamke walikolala waje waseme ni mipango ya Mungu.Kama wameshindwa wafunge tu hizo dude zao watu warudie ustaarabu wao wa mwanzo.
Waongeze mabasi waache uhuni uhuni,wajirekebishe kwa kutuwekea pia madereva wenye weledi maana kuna wengine ni kama popobawa.Waache uzembe uzembe usio na maana.Hakuna visingizio hapo mradi huo unalipa..wakishindwa wawatafute watu wenye machungu na pesa wawekwe hapo wapewa uhuru waone kitachotokea.
 
View attachment 1067846

Pamoja na hayo, lakini kuna kitu kingine haiwezekani kabisa, magari yapo yamepaki kituoni lakini wanasubiri watu wajazane ili gari lijaze kupita kiasi, kuna namna fulani hapa aidha kubania mafuta.
Ukweli kama kweli TB inaambukizwa kwa njia ya hewa, sina uhakika kama sisi watu wa Kimara na Mbezi tutapona..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sisi tunaotumia usafiri huu sasa siyo issue tena kuikuta moja wapo wa hizi bus zao imezima katikati ya vile vichochoro vyao maana moja likizima likaziba barabara yake hakuna atakaepita labda mpae.
 
da4e36161484d5e6b7e2632b7db47c51

Dar es Salaam. Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), imesema kuna uhaba wa mabasi yanayotoa huduma na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa usafiri huo.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano Aprili 10, 2019 kwa vyombo vya habari na Meneja Uhusiano wa Umma wa Dart, William Gatambi imesema uhaba huo unatokana na mabasi hayo kupata hitilafu mbalimbali.
“Idadi ya mabasi yanayotoa huduma leo katika mfumo wa Dart ni 85, huku 58 yakifanyiwa matengenezo makubwa na madogo.
“Tunawaomba wateja wetu kuwa na subira wakati mabasi hayo yakifanyiwa matengenezo. Tunawaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza,”amesema Gatambi.
Aprili 5, mwaka huu mtendaji mkuu wa Dart, Ronaldo Lwakatare alisema kipindi cha mpito cha uendeshaji wa mradi huo kimewapa funzo kubwa kutokana na changamoto zilizojitokeza.
Alisema katika kipindi hicho wamekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uchache wa mabasi tofauti na matarajio hali inayosababisha abiria wanaotumia mradi huo kupata adha ya usafiri huku baadhi yao wakilazimika kutumia muda mrefu kukaa vituoni kuyasubiria mabasi hayo.
Lwakatare alisema kwa sasa mradi huo una mabasi 140 yanayotoa huduma badala ya 300, lakini bado wanakumbana na changamoto kwa robo ya mabasi yaliyokuwapo kuwa mabovu hata hivyo wanashirikiana na mtoa huduma hiyo kampuni ya Udart.
“Mabasi mengi ni mabovu na yanapita katika kipindi kigumu. Lakini Dart inashirikiana na Udart kuhakikisha yanatengenezwa ili kurejea barabarani na hatimaye huduma iwe ya kawaida,” alisema Lwakatare.
Huu ni upumbavu na dharau kubwa kwa wananchi tunaotumia usafiri huu. Kwani matengenezo ya magari ya mradi huu ni dharura.? Iko siku wananchi watachoshwa na uzembe huu..
 
Back
Top Bottom