Upotoshaji juu ya uwekezaji wa DP World unalengo la kuwahadaa wananchi kutokufanya maandalizi ya kuzichangamkia fursa zinazokuja katika Bandari zetu

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Maandalizi ndio msingi wa kila jambo,huwezi kufaulu usaili vema bila kufanya maandalizi,huwezi kufundisha vema kama ni mwalimu bila kufanya maandalizi,huwezi kugombea nafasi ya kisiasa,huwezi kusafri,kucheza mpira au kufanya jambo lolote bila kufanya maandalizi.Kadiri maandalizi yanavyofanyika mapema ndivyo unapokua katika nafasi nzuri ya kupata mafanikio.

Hakuna shaka kuwa kila nchi inatengeneza mazingira mazuri ili kuvutia wawekezaji kuwekeza kwenye nchi zao kutokana na manufaa makubwa yanayopatikana kwenye uwekezaji.Nchi makini zinaweka mazingira mazuri kuvutia wawekezaji wakubwa kama Dp World ambao wamewekeza kwenye bandari kubwa katika nchi nyingi za Ulaya,Asia na baadhi ya nchi za Afrika.Uwekezaji wa DP World katika nchi hizi unaongeza ajira,unaongeza ufanisi kwenye bandari,na kuleta pato la uhakika kwa serikali.

Bandari ya Tanzania kwa miaka mingi imekua haitoi tija ambayo inapaswa kutoa na kuleta maendeleo kwa wananchi. Jitihada nyingi zimefanyika kuifanya bandri iweze kuwanufaisha Watanzania wengi,uwekezaji wa TICTS ni mfano mmoja wapo nah atua za mara kwa mara za pangua pangua ya uongozi wa bandari na malalamiko mengi ya utendaji.

Ni vema wanchi wakaelewa kuwa,propaganda zinazoendelea sasa hivi juu ya uwekezaji katika bandari yetu ndizo zilizofanyika kwenye uwekezaji wa bwawa la Nyerere,ndizo zilizofanyika kwenye ujenzi wa SGR na miradi mingine mingi ya kimkakati. Upotoshaji unaweza kutoka kwa wananchi wasioelewa ukweli na wale wachache wenye maslahi yao binafsi na yale ya nchi zao wanayopata kutokana na ufanisi duni wa bandari yetu.Hakuna bandari shindani inayoweza kufurahia hatua kubwa ya kiuchumi ambayo bandari za Tanzania zinaenda kuingia na kampuni kubwa na mahiri duniani. Vile vile sio rahisi kwa wale wachache waliokua wakihujumu bandari yetu kufurahia juu ya mabadiliko yanayoenda kutokea.

Kubwa ninalotaka kueleza hapa ni kuwa wananchi sasa hivi wanapaswa kujiandaa namna ya kuzichukua fursa mbalimbali ambazo kwa miaka zaidi ya 30 fursa hizi zimekua zikiwafaidisha watu wachache na bandari za nchi Jirani.

Maandalizi ya kupokea ajira nyingi kwa pamoja.
Miaka mingi iliyopita ajira katika bandari zetu zilikua chache na za watu kufahamiana,serikali kwa muda mrefu sasa haija ajiri wafanyakazi wengi katika bandari.DP world itafungua ajira kwa Watanzania ambao wana vigezo ili kutoa huduma mbalimbali bandarini.Kampuni mbalimbali zinazotoa huduma bandarini zitafungua ajira nyingi ili kuendana na kasi,na ukubwa wa kazi za utoaji mizigo bandarini.Ni muda wa wananchi kuandaa wasifu na kufahamu ni ujuzi gani unahitajika wapi ili kuweza kuchukua fursa hizi.

Fedha kuingia kwenye miradi ya maendeleo

Wananchi wategemee kuona fedha zinazokusanywa kama mapato ya bandari haziishii mifukoni mwa wafanyakazi wasiozidi 400 wa bandari peke yao kutokana na ufanisi duni, bali fedha hizi pia zitafikia watanzania wapatao milioni 60 kupitia miradi ya maendeleo ambayo serikali itatekeleza.Miradi hii itakua na manufaa ziada ya kiuchumi (multiplier effect) kwa kila mwananchi.Miradi ya maendeleo itaajiri,itatoa huduma na kuongeza mzunguko wa uchumi kwa wananchi wote ambao wanajishughulisha.

Idadi kubwa ya wafanyakazi watakaoajiriwa katika badari zetu itahitaji huduma za chakula,usafri na huduma zingine ambazo wananchi wanaweza kufaidika nazo.Ni muda wa kuandaa kampuni au kutafuta mitaji ya kutoa huduma hizi katika bandari zetu na sio kusubiri hizi fursa kuchukuliwa na watu wengine.

Wananchi wanaokaa karibu na bandari

Wananchi wenye maeneo yao nje ya wanaweza kuyakodisha kwa wawekezaji wanaoanzisha bandari kavu,watoa huduma mbalimbali.

Watoa huduma za bandari
Kampuni nyingi za wakala wa forodha ambazo zilikua zimekufa sasa hivi ndio wakati wa kuzifufua ili kuweza kuchukua fursa ya kuondosha mizigo bandarini.Ongezeko la 70% ya shehena kutoka 18 milioni mpaka kufikia 58milioni ni ongezeko kubwa sana la shehena ya mzigo ambao utahitaji ongezeko kubwa la watoa huduma ndani ya bandari zetu

Nitaendelea kuandika hapa kadiri nitakapopata muda
 
Back
Top Bottom