Upotevu wa 2.4T: Wapinzani wajifunze kutengeneza uwongo ulio karibu na ukweli!

Kwani maelezo ya Asunga ndivyo majibu ya serikali yanavyotakiwa yatolewe kwa mujibu wa sheria? Yaani CAG anajibiwa kwa staili hii?
Uzuri Kamati ya PAC iko chini ya kambi ya upinzani.

Mwenyekiti wa Kamati alishatoa taarifa yao haya mengine ni yaleyale ninayoyasema kuwa wapinzani wanatakiwa watengeneze uwongo ulio karibu na ukweli.
 
Nianze kwa kumshukuru sana na kumpa pongezi nyingi MsemajiUkweli kwa bidii anayoionesha katika kutetea juhudi za awamu ya tano isiyokubali kukosolewa wala kupangiwa. Nina swali moja tu kwa MsemajiUkweli, hivi mpaka sasa tumetumia fedha kiasi gani katika manunuzi ya ndege! Nina hakika swali dogo kama hili halitakutatiza hata kidogo na kumbuka aulizaye ataka kujua.
 
Kwani kuna sehemu CAG kahoji 1.5T ktk ripoti yake?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
Kinachofurahisha ni kuwa aliyeanzisha hoja ya 1.5T kwa sasa ameishahamia kwenye hoja zingine wakati waliobaki na hoja hiyo ni wale kasuku wa kisiasa.

Ndio maana nikasema, wapinzani wajifunze kutengeneza uwongo ulio karibu na ukweli.
 
Huu wa sasa wa kuficha kila kitu ndo mbovu kuliko hata iliyopita. Mfumo wa kupaka rangi uchafu kama unavyojaribu kufanya wewe na wabunge wako ni hatari mno. Hata fedha za Tegeta Escrow mwanzoni mlijtahidi kuficha hivi hivi, usitudanganye kwamba ripoti ya Tegeta Escrow ilisomwa "from a white plate", ni uongo. Ilitoka kwa mbinde ingawaje angalau Kikwete alikuwa tayari hata kuvuliwa shati ili kifua kionekane. Lakini huyu kwa vile anataka watu waamini ni msafi kumbe kuna madudu kibao, hataki hata kuvuliwa koti. Ukweli uko wazi fedha zimepigwa. Na hili la kila sehemu nyeti kuwekwa "watoto wa Dada" matokeo yake mtayaona na kuyakiri ninyi wenyewe akishatoka madarakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri Kamati ya PAC iko chini ya kambi ya upinzani.

Mwenyekiti wa Kamati alishatoa taarifa yao haya mengine ni yaleyale ninayoyasema kuwa wapinzani wanatakiwa watengeneze uwongo ulio karibu na ukweli.
Kuibwa na kutokujulikana zimetumikaje ni vitu viwili tofauti lakini kimoja inawezekana kikawa chanzo cha kingine.

Inawezekana kuwa hazijulikani zimetumikaje, lakini mwisho wa siku uchunguzi ukifanyika itagundulika kwamba kulikuwa na wizi ama ufujaji wa fedha za Umma.
 

Kwahiyo uchumi wa gas ilikuwa ni kauli mbiu ya kampeni? Huna utetezi wa maana bali unalazimisha tu.
 
Nasema kila siku tz haina wapinzani ina wahuni flani,wajanja wajanja.
 
Huwa sihangaiki na maneno ambayo naona hayana Tija, watadanganywa hao , na ukiongelea tena udanganyifu wa kina Zitto unaendelea kuvuta attention ya watu kwa hilo,

Mi huwa ni vigumu kunilisha matango pori na niko hivo, wala sijawahi kufikiria kama Kuna upotevu wa 1.5 maana ni uongo mtupu
 
Mbona ripoti ya CAG hakuna sehemu iliyosema kuna wizi wa 1.5tr, na ripoti ya PAC pia imetoka na imefafanua hicho hicho, hakuna hata thumni iliyoibiwa ndio maana umemuona Zitto amefunga bakuli lake saivi.
Ni kweli report inaonyesha hakuna sehemu hela imeibiwa! Anachouliza CAG ni matumizi yake na siyo wizi! tofautisha vitu viwili
 
Weka fact hapa acha mbwembwe! Kwanza elimu yako kiasi gani labda tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…