A
Anonymous
Guest
Waziri wa Ardhi nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Napende kukutumia ujumbe wa utapeli au uporaji wa ardhi kwa wananchi wa Mbopo wilaya ya kinondoni na watu wanaojiita DDC (Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam). wanavizia wananchi wakiwa hawapo then wanakwenda kupima maeneo yao. Ila pia kuna maswali fikirishi ya kisheria ambayo wananchi wakijaribu kuhoji hawapati majibu sana sana ni vitisho. Hili jambo ni mwendelezo wa chuki kwa serikali kutoka kwa wananchi

- Wananchi wanataka kujua uhalali wa hati ya umiliki wa ardhi ya DDC kwenye eneo la Mbopo, Mabwepande. Je, hati yao ipo kihalali, na lini hiyo hati ilitolewa na imekuwaje kumekuwa tena na hati juu ya hati maana kuna wananchi walinunua maeneo eneo hilo alafu wakaweza kutengeneza hati
- Pia kama serikali inalitaka hilo eneo kwanini hakuna utaratibu mzuri wa kuwaelesha, kuwapa taarifa na kuelewana namna ya kufanya compansation maana wananchi wako eneo hilo kwa muda mrefu sasa na sheria nadhani inaelekeza kuwa kama mtu yupo eneo fulani zaidi ya miaka 12 basi kuna namna za kufuata
- kiujumla wananchi wanaona serikali imeamua kupora ardhi yao