Mimi naomba mnisaidie. Uponyaji wa Mungu unaambatana na kuamini injili ya kristo, au kila kitu kinajitegemea? Tiba ya babu unaambatana na kuhubiri neno? Au mtu akinywa dawa anaruhusiwa kuendelea na maovu yake yaleyale? Naomba msaada wenu. Stevemike.
ushauri wa kwanza mada hii ungeiweka kwenye jukwaa la dini, maana imekaa kidinidini hivi, ungewapata wakina Maxshimba wakuelezee vizuri zaidi,
So far kama ulivyosikia na ilivyo ni kuwa babu anakupa dawa unywe, kwa imani yake na sala zake anaamini utapona, na wewe mnywaji imani yako ndiyo itakayokuponya,,, na wengi walioamini wamepona...........
Inaelekea wewe ni wale wanaojiita wa-kristo,lakini neno la Mungu hamlijui wala Roho Mtakatifu hamnae.Katika hali hiyo ni rahisi sana kutekwa na udanganyifu kama huu wa mchungaji wa Loliomdo.Nakushauri umuombe Mungu akujaze Roho Mtakatifu,halafu neno la Mungu lijae kwa wingi ndani yako.Hutayumbishwa kamwe na shetani.
Ukiwa na Imaani KIasi cha chembe ya haradani, waweza kuhamisha milima na kuitupa baharini, Ukitaka kufahamu kitu mwombe roho wa BWANA, na sio kujazwa na roho mtakatifu (mtakafujo). Mtatizamo wa mtu (MTU) binafsi pamoja nauwezo wake wakuelewa mambo, usilazimishe kuwa ndio msimamo wa jambo liwalo lote. Kwa imani tunapona, ninakiri kupona maradhi kwa imani.Mchungaji anataja MUNGU, YESU, ambayo huyo shetani akisikia hudondoka kipi ni bora jamani? kuponya au kuangamiza! Busara itawale...Inaelekea wewe ni wale wanaojiita wa-kristo,lakini neno la Mungu hamlijui wala Roho Mtakatifu hamnae.Katika hali hiyo ni rahisi sana kutekwa na udanganyifu kama huu wa mchungaji wa Loliomdo.Nakushauri umuombe Mungu akujaze Roho Mtakatifu,halafu neno la Mungu lijae kwa wingi ndani yako.Hutayumbishwa kamwe na shetani.