Upofu wa ukawa hili group la wezi lowasa hajalikana popote

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
SIKU Edward Lowassa alipotangaza rasmi
kugombea urais wa Tanzania nilibahatika
kumsikiliza na nilishuhudia umati mkubwa
wa watu waliofurika kumsikiliza. Ni kweli
yalikuwa ni mafuriko ya watu. Sijui kama
walikwenda kwa hiari yao au walilipwa ili
waende kwenye mkutano huo.
Hilo sijui wala si ajenda yangu kwenye
makala hii. Jambo ambalo ninataka
wasomaji wa makala hii walizingatie ni
aina ya watu waliokuwepo kwenye mafuriko hayo,
kwani ndege wenye manyoa yanayofanana ndiyo
wanaoruka pamoja.
Tumeona utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Rais
aliyeingia kwa hamasa kubwa akibeba matumaini
na matamanio ya mamilioni ya Watanzania .
Utawala wa Kikwete ulikuja na kila ahadi za
kurudisha utukufu wa Taifa. Lakini Kikwete
atakapoondoka mwezi wa kumi mwaka huu, Je
atakuwa amefanikiwa kurudisha heshima ya taifa
letu?
Na wakati wa mchakato wa kugombea urais,
Watanzania wengi walimuunga mkono Kikwete
hadi baadhi ya viongozi wa dini walifikia kusema
alikuwa chaguo la Mungu. Walisema sauti ya
wengi ni sauti ya Mungu! Leo ukisema kwamba
Kikwete alikuwa chaguo la Mungu, sijui kama
Watanzania wengi watakubaliana na wewe. Sijui.
Rais Kikwete alitengeneza mtandao uliomsaidia
kuingia Ikulu. Lowassa ametengeneza mtandao
unaomsaidia aingie Ikulu. Isipokuwa katika
maelezo yake Lowassa, amejitahidi kujitofautisha
na Kikwete na hasa aliposema suala la urafiki
wao lisihusishwe katika azma yake ya kuomba
nafasi ya kuwa rais.
Anawataka Watanzania wampime kama yeye
binafsi na wasilihusishe suala la urafiki wao. Sijui
kwa nini kwa sasa Lowassa anajitenga na
Kikwete. Lakini Watanzania wanakumbuka
Lowassa aliwahi kusema urafiki wao si wa
kukutana barabarani.
Kwa kuwa Lowassa anaomba nafasi ya nyeti ya
urais ni muhimu Watanzania wajiridhishe bila
shaka yoyote Lowassa ni nani. Na je anaweza
kukabiliana na changamoto zinazolikabili Taifa
letu hasa ufisadi, rushwa na kuporomoka kwa
maadili.
Mwalimu Nyerere katika kitabu chake, Nyufa, cha
mwaka 1995, alisema: “Sasa Tanzania inanuka
rushwa… tunataka kiongozi anayejua hivyo,
ambaye atasema rushwa kwangu mwiko,
mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa
na… watoa rushwa watamjua hivyo. Lakini
hatutaki aishie hapo tu, maana haitoshi wewe
mwenyewe uwe mwaminifu… Unaweza ukawa
wewe mwaminifu kabisa kabisa, lakini una
shinikizo la ndugu zako, jamaa zako na marafiki
zako.
“Kwa hiyo si inatosha wewe kuwa mwaminifu tu,
lakini uwe na uwezo wa kuwaambia jamaa zako
kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia
tena. Unawaambia jamaa na rafiki zako kwa
dhati kabisa… Ikulu ni mahali patakatifu, mimi
sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja
kupageuza pango la walanguzi na hakuna serikali
yoyote duniani inayoongozwa bila miiko”.
Zipo taarifa zinazoeleza kwamba fedha nyingi
zimetumika katika kufanya maandalizi ya
mkutano wa Arusha uliosababisha mafuriko ya
watu. Aidha, ndugu Lowassa mara kadhaa
amekiri kwamba marafiki zake ndio
wanaomchangia kufanikisha safari yake ya
matumaini.
Hivyo fedha nyingi anazochangia kwenye
harambee kwenye misikiti na makanisani nyingine
anatoa yeye na nyingine anachangiwa na hawa
marafiki zake ambao wengi wao ni wafanya
biashara matajiri na wengi wao ni wale
waliotajwa kwenye kashfa za ufisadi na tuhuma
mbalimbali.
Hawa marafiki zake Lowassa wamesaidia sana
kumjua Lowassa ni nani, kwani wahenga
walisema, “Nionyeshe marafiki zako na mimi
nitakuambia wewe ni nani au wewe una tabia
gani”.
Hawa marafiki zake na Lowassa wanaweza
kuwasababisha Watanzania wamtilie shaka
Lowassa kama anaweza kuwa safi na kustahili
kupewa dhamana ya kuongoza nchi. Naomba
niwakumbushe kauli ya Mwalimu Nyerere kuhusu
mmoja wa wagombea urais kwenye NEC Dodoma
mwaka 1995, “Hapa hatuchagui mtu maarufu,
tunachagua mtu safi na huyu si safi”.
“Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe
nae chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu.
Hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini
mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa
ugoni, Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike”.
“Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba si
kweli. Lakini Kaisari bado akamwacha, akasema
mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na
sisi hapa mgombea wetu hapaswi hata
kutuhumiwa wakati wapo wengine wasafi ambao
hawana tuhuma.
“Kama mtamteua huyu mimi sitapiga kampeni.
Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu
nimwombee kura. Hapana kabisa . Huyu najua si
msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa
mgombea wetu”.
Aidha, mtakumbuka pia kuwa mwaka 1995, kundi
la Vijana lilimtaka Lowassa ateuliwe kugombea
urais wa Tanzania. Hata hivyo, ilitolewa kauli
kuwa Lowassa alikuwa na tuhuma za rushwa,
kujilimbikizia mali na kupungukiwa na maadili,
kinyume na katiba ya CCM na kanuni za chama
hicho.
Kamati Kuu ilipopeleka mapendekezo ya
kutompendekeza kugombea urais, Lowassa
alitetewa kwa makelele, kihuni, bila kufuata
taratibu za kikao cha NEC Dodoma. Kundi moja
lilikuwa limejiandaa kumpitisha kwa hoja ya
nguvu na si kwa nguvu ya hoja.
Waliyatetea maelezo ya Kamati Kuu, lakini
waliyakataa yale ya nyongeza aliyoyatoa
Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi (Rais wa wakati
huo) ambaye alielezea tuhuma hizo zilizokuwa
zinamkabili Lowassa. Hivyo, naomba kusisitiza
kwamba Lowassa hakuwa chaguo la CCM katika
uchaguzi wa mwaka 1995.
Katika kikao hicho cha Kamati Kuu, Mwalimu
Nyerere aliamua kusaidia kikao kwa kutoa
maelezo ya nyongeza. Aliwauliza wajumbe wa
NEC maswali, kwamba wao ni wahuni au ni
viongozi wa CCM? Ikiwa wao ni viongozi wa
CCM, je, hivyo ndivyo wanavyopaswa kumtafuta
mgombea wa urais, kwa makelele?
Kama Watanzania wangewaona walivyokuwa
wanafanya katika kikao hicho, je, wangeamini
kuwa wao ni viongozi kweli? (Wajumbe walibaki
kimya). Kisha Mwalimu aliendelea kusisitiza
maelezo aliyoyatoa Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi
akisema: “Mwinyi amemstahi sana Lowassa”.
Hakuwaambia wajumbe wa NEC baadhi ya
tuhuma mbaya kabisa kuhusu Lowassa.
Ikiwa NEC inachoombwa ni kuchagua kati ya
wenye tuhuma za rushwa kuchaguliwa kwa nafasi
ya urais, na wale wasioitaka, basi huu ni wakati
muafaka kwao kuipeleka hoja hiyo mbele ya
Watanzania waiamue kwa kuwa ndani ya NEC
hakuna mwenye uwezo wa kumfukuza mwenzie,
wote ni wajumbe sawa kwa mujibu wa katiba ya
CCM”.
Hatimaye kikao cha NEC kiliondoa jina la
Lowassa, kikawateua Benjamin William Mkapa,
Cleopa David Msuya na Jakaya Mrisho Kikwete
kuwa wagombea. Majina yao yaliwasilishwa
kwenye Mkutano Mkuu ambao ndio uliopaswa
kumchagua miongoni mwao kuwa mgombea urais
wa CCM.
Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM, wagombea hao
watatu walijinadi kwa wajumbe. Kikwete
alipokuwa akijinadi aliwaeleza wajumbe kwamba
endapo wangempitisha kugombea na akashinda,
angemteua Lowassa kuwa Waziri Mkuu wake.
Lakini hapa pia tujiulize, pamoja na maelezo ya
Mwalimu Nyerere na Kamati Kuu kuondoa jina la
Lowassa kwa nini bado Kikwete alidiriki kumtaka
Lowassa awe Waziri wake Mkuu?
Hapa kwa akili za kawaida inaonekana dhahiri
kuwa Kikwete na Lowassa ni marafiki wakubwa.
Lowassa Alisha sema urafiki wao si wa kukutana
barabarani. Nionyeshe rafiki yako na mimi
nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani au
nitakuambia tabia yako.
Hata hivyo Kikwete hakuchaguliwa kuwa
mgombea urais. Historia hii inatoa mfano hai wa
jinsi matatizo yanayolikumba taifa letu
yalivyoanza.
Ni dhahiri kabisa kuwa watu walewale,
wakiongozwa na tamaa zilezile za kuwa matajiri
na kutaka urais kwa gharama yoyote hata
kuhonga au kutumia fedha, ndio wanaolisumbua
taifa letu mpaka sasa.
Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba, wale
wanaoomba nafasi ya urais hawapaswi
kutuhumiwa kwa jambo lolote. Hawapaswi
kutiliwa mashaka kuhusu uadilifu wao.
Wanapaswa kuaminiwa kuhusu dhamira yao ya
kupiga vita ufisadi na rushwa.
Na wagombea hawa tunaweza kuwajua kutokana
na hulka au tabia za marafiki zao. Katika
mafuriko ya Arusha, baadhi ya walioshiriki
mkutano huo walitajwa. Hawa walitajwa kuwa ni
marafiki wa Lowassa. Wengine walikuwa
wamevaa nguo zilizoandikwa “Marafiki wa
Lowassa”.
Baadhi ya marafiki wa Lowassa ni pamoja na
Rostam Aziz, Andrew Chenge, Anna Tibaijuka,
Cyril Chami, Ezekiel Mayige, David Matayo, Nazir
Karamagi na kadhalika.
Baadhi ya marafiki hawa wa Lowassa wengi wao
ni wale ambao ama walijiuzuru kwa kupatikana
na tuhuma za ufisadi, au wengi wao
waliondolewa kwenye nyadhifa zao kwa kashfa za
kutokuwa waadilifu.
Na wengi wao ni wafanyabiashara na matajiri.
Tunapoliangalia kundi la watu wanaomuunga
mkono Lowassa, tunaweza kujua Lowassa ni
nani. Tukiliangalia kundi linalomuunga mkono
Lowasssa tunaweza kujua kama Lowassa akiingia
Ikulu atapambana na rushwa na ufisadi au
ataenda kufanya biashara.
Je, marafiki wa Lowassa anaowataja na
walioonekana kwenye mafuriko ya Arusha
wanakerwa na rushwa na ufisadi kwa dhati?.
Ndege wenye manyoya yanayofanana ndio
wanaoruka pamoja.
Watanzania tukumbuke kwamba utumishi wa
umma ni dhamana na fursa adhimu kwa ajili ya
kulinda na kutetea maslahi ya wananchi wote.
Haya ni maneno aliyoyasema Rais Barack Obama
baada ya kula kiapo cha kuongoza Marekani.
Inawapasa wale wanaopata nafasi za
kuchaguliwa wafahamu kwamba wamepewa
dhamana ya kuwatumikia wananchi na si nafasi
ya kujitajirisha au kumnufaisha ndugu au
marafiki. Kutokana na kumomonyoka kwa maadili
na moyo wa uzalendo nchini, uongozi umegeuzwa
kuwa nafasi ya kujitajirisha. Urais, uimekuwa
fursa ya uwekezaji, na wala si fursa ya
kuwatumikia wananchi.
Ukweli kwamba kuna matajiri au watu
wanaotumia pesa kumiliki siasa na uongozi katika
nchi yetu, ni jambo lililo wazi. Zipo taarifa
kwamba baadhi ya watu wanaokwenda kwenye
mikutano ya watia nia ya urais mfano waliofurika
Arusha walinunuliwa waende kwenye mkutano,
walilipwa wapige kelele “Rais, Rais”.
Matumizi makubwa ya fedha yalionekana katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Baada ya
kutangazwa mshindi wa kiti cha urais katika
uchaguzi huo, Kikwete, alizindua Bunge Desemba
30, 2005 alidhibitisha hili alisema: “Yameanza
mawazo kuwa uongozi unaweza kununuliwa kwa
fedha.
“Tusipokuwa waangalifu, nchi yetu inaweza
kuwekwa rehani kwa watu wenye fedha za
kununua uongozi au wanaoweza kupata fedha za
kufanya hivyo, maana unaweza kufadhiliwa na
mtu ili ununue uongozi, ni vema sasa
tulishughulikie suala hili”.
Kuna mawazo kwamba sasa Tanzania inahitaji
Rais tajiri. Ninapenda niwakumbushe wosia
alilowahi kuutoa Mwalim Nyerere wakati wa uhai
wake juu ya hatari ya watu wachache wenye pesa
kujaribu kutafuta uongozi kwa manufaa yao.
Alisema: “Tanzania halijawa taifa imara sana na
adilifu kiasi cha kuruhusu matajiri kuingia kwenye
uongozi wa nchi kama ilivyo Marekani na Ulaya.
Wakati huo bado uko mbali sana na tukitaka
kuuvuta kwa kamba huko ndiko kuliingiza taifa
letu changa kwenye kiwango cha ufisadi”.
Mgombea mmoja wa urais amesema bado
anasaka utajiri na anaomba aende Ikulu. Je Ikulu
kuna biashara gani itakayompatia utajiri? Na wale
wanaomuunga mkono atawalipaje akienda Ikulu?
Nchi kuwekwa rehani kwa matajiri ni jambo la
hatari sana, kwa maana serikali itaongozwa na
matajiri na haitawajibika kwa wananchi. Hili
limeanza kujitokeza. Demokrasia itakoma na
udikteta utatawala.
Jambo linalojitokeza hapa na ambalo ni matokeo
ya matumizi makubwa ya fedha na rushwa
kwenye chaguzi, ni kupatikana kwa viongozi
ambao hawakuchaguliwa na wananchi bali
walinunua uongozi au waliotoa rushwa
kushawishi wapiga kura wawape uongozi.
Serikali inayopatikana kwa rushwa haiwajibiki
kwa wananchi. Hutumikishwa na matajiri
walionunua uongozi na waliotoa rushwa. Serikali
hiyo huwaabudu matajiri walioiweka madarakani,
haiwezi kufanya maamuzi yenye maslahi kwa
wananchi.
Serikali hiyo hulinda maslahi ya watu wachache,
haiwezi kuchukua hatua dhidi ya ufisadi. Baadhi
ya maamuzi ambayo yamekuwa yakitolewa na
utawala wa awamu ya nne, ripoti ya hivi karibuni
ya Ikulu ya TOKOMEZA na ESCROW ni ushahidi
wa ninachokieleza.
Tuwe makini na wagombea wanaotumia fedha
nyingi na wanaopewa fedha nyingi na marafiki
zao katika mchakato wa kutafuta nafasi za
kuchaguliwa urais, ubunge na udiwani.
Tumejifunza katika utawala wa awamu ya nne.
Tusirudie makosa.
Ningependa kusisitiza, Watanzania tunatakiwa
tuichukie rushwa ya aina yoyote. Rushwa ni
dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti.
Rushwa hupofusha macho na moyo. Taifa
linaoendekeza rushwa ni taifa ambalo watu wake
ni sawa na vipofu na wafu.
Vipofu ambao hawaoni madhara ya rushwa na
mioyo yao imekufa. Rushwa inapotolewa na
kupokelewa kwa shangwe makanisani na
misikitini na wagombea wa vyama vya siasa ni
ushahidi wa jambo hili.
Tanzania ina nafasi ya kuwa Taifa
linaloheshimika kama tutaichukia rushwa na
kukataa kuipokea au kuitoa. Mfalme Suileman
aliwahi kusema; “haki huinua taifa bali dhambi na
uovu ni aibu ya watu wote”. Rushwa ni dhambi
na ni aibu kwa watanzania wote.
Tanzania imepoteza heshima kwa sababu ya
rushwa. Pia napenda kusisistiza, Kwenye nchi
ambapo rushwa imetawala sauti ya wengi si sauti
ya Mungu. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu
kwenye nchi ambapo haki, usawa na upendo
vinatamalaki.
Mafuriko ya watu kule Arusha kama walilipwa ili
waende kwenye mkutano sauti yao si sauti ya
Mungu. Na, Je Lowassa ana dhamira ya kweli ya
kuchukia rushwa?
Nionyeshe marafiki zake na mimi nitakuambia
kama Lowassa ana dhamira ya kweli ya kupiga
vita rushwa na ufisadi. Niliposikiliza akisema
atapiga vita ufisadi, rushwa na atahakikisha
rasilimali za nchi hii zinawanufaisha Watanzania
na nilipowangalia marafiki zake ni nani, nilitambua
anachokifanya ni usanii. Hana dhamira ya kweli
na anachokisema.
Lowassa hafai kuwa Rais.
 
Mnajaza seva bure, mtuambia magu ana mipango gani kuondoa nchi kwenye umaskini mkubwa, na ana nini cha kufanya kwenye
1.elimu
2.afya
3.viwanda
na atareform vipi taasisi kama takukuru, ewura nk
la sivyo ni kujaza seva tu
 
magufuli ni kimsingi ni mtendaji sio mwanasiasa vuta2 subira
 
MAGUFURI: kasimamia miundombinu mpaka sasa wafanya biashara wanauwakika wa kusafiri na mizigo yao kwa muda muafaka pasipo kuaribika kwa bidhaa zao. FAIDA
LOWASA: kashindwa kuleta mvua ya kutengenezwa alipokuwa Waziri Mkuu Kama alivyoomba pesa na kupewa akailetea hasara taifa la sh.152 mil. kwa siku na mvua haikuonekana. HASARA

MAGUFURI: Alipokuwa Waziri wa ujenzi nyumba na makazi aliweza kufukuza wapangaji waliokuwa na madeni sugu na hata kuliletea shirika la nyumba la Taiga, ila alipokamata wizara hiyo aliweza kulifanya shirika hilo kuweza kujitegemea na hata kuwa na uwezo wa kujenga nyumba za kutosha na kuuzia watanzania.FAIDA
LOWASA: alikuwa Waziri wa maji aliipa serikali hasara kubwa kwa kushindwa kufikisha maji mji wa kahama na shinyanga kama malengo yalivyokuwa kwa kula pesa nyingi Mpaka Leo wakazi wa shinyanga wamebakia kuona mabomba yasiyo na maji. HASARA.

MAGUFURI: Ameweza kuwawajibisha makandarasi feki waliolitesa taifa hili kwa miaka mingi mpaka sasa kufanya wakandarasi kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii kwa kuogopa mkono wa magufuri na Dora kwa ujumla mpaka sasa watu mnauwakika wa kufika makwenu bila kulala njiani kwa Barabara bora na madaraja. FAIDA
LOWASA: Amezidi kuumiza watanzania kwa kampuni yake inayoendelea kulipwa kila unit moja kwenye umeme mpaka kusababisha watanzania kushindwa kuwa na umeme kutokana na gharama kuwa kubwa na kusababisha uchumi kuyumba mpaka Leo. HASARA.

UKAWA hauwezi kunitumia kwa kuwa na uchu wa madaraka wakati watanzania wanahitaji kiongozi wa kweli asie mfanyabiashara na mkwepa kodi mkubwa kama mliemsimamisha hadi kuwapa upendeleo wafanyabiashara wakubwa kupewa msamaha wa kodi na kuwaumiza wafanyabiashara wadogo wadogo. CCM ndicho chama chenye viongozi bora mpaka ukawa wakashindwa kumtafuta mbadara wakaamua kuja kutafuta makapi CCM. Inawezekana vipi MTU mliemtuhumu tena kwa ushahidi Leo mnampaka mafuta nakusema msafi kisa kwa uwezo wa pesa zake
Ngoja kwanza ajifunze itikadi za Chadema kama DR. SLAA alivyokipigania chama can chadema na kutupwa kama kuku asiethaminika mwende mkatumiwe ila MUNGU atalisimamia taifa hili na kutupa kiongozi ataetuvusha.
WAALIMU kunadalili ya kuendelea kuwa na maisha magumu mpaka mwisho wa uzee wetu kwani mmelia kwa miaka mingi MUNGU amesikia kilio chenu na kuwapa kiongozi mwalimu, mkewe mwalimu ila Sie ndo wakwanza kumpinga kwa vishindo. Nataka kujuta kuwa mwalimu na kuwapongezq wafanya biashara wenye mshikamano wa kwe
 
CCM ing'oke kwanza madarakani, mengine baadae!

Hii agenda tushaikataa kwa vile haitatutofautisha watanzania na Walibya maana walibya walipokuwa wakiulizwa sababu halisi za kumuondoa Gadafi na mkakati wa mbele utakuwaje, walisema "TUNATAKA AONDOKE TU TUMEMCHOKA, YA BAADAYE TUTAPANGA BAADA YA YEYE KUONDOKA". Kinachoendelea Libya sote tunakijua.
 
hii agenda tushaikataa kwa vile haitatutofautisha watanzania na walibya maana walibya walipokuwa wakiulizwa sababu halisi za kumuondoa gadafi na mkakati wa mbele utakuwaje, walisema "tunataka aondoke tu tumemchoka, ya baadaye tutapanga baada ya yeye kuondoka". Kinachoendelea libya sote tunakijua.

true ht dk na prof wanalikubali hili
 
SIKU Edward Lowassa alipotangaza rasmi
kugombea urais wa Tanzania nilibahatika
kumsikiliza na nilishuhudia umati mkubwa
wa watu waliofurika kumsikiliza. Ni kweli
yalikuwa ni mafuriko ya watu. Sijui kama
walikwenda kwa hiari yao au walilipwa ili
waende kwenye mkutano huo.
Hilo sijui wala si ajenda yangu kwenye
makala hii. Jambo ambalo ninataka
wasomaji wa makala hii walizingatie ni
aina ya watu waliokuwepo kwenye mafuriko hayo,
kwani ndege wenye manyoa yanayofanana ndiyo
wanaoruka pamoja.
Tumeona utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Rais
aliyeingia kwa hamasa kubwa akibeba matumaini
na matamanio ya mamilioni ya Watanzania .
Utawala wa Kikwete ulikuja na kila ahadi za
kurudisha utukufu wa Taifa. Lakini Kikwete
atakapoondoka mwezi wa kumi mwaka huu, Je
atakuwa amefanikiwa kurudisha heshima ya taifa
letu?
Na wakati wa mchakato wa kugombea urais,
Watanzania wengi walimuunga mkono Kikwete
hadi baadhi ya viongozi wa dini walifikia kusema
alikuwa chaguo la Mungu. Walisema sauti ya
wengi ni sauti ya Mungu! Leo ukisema kwamba
Kikwete alikuwa chaguo la Mungu, sijui kama
Watanzania wengi watakubaliana na wewe. Sijui.
Rais Kikwete alitengeneza mtandao uliomsaidia
kuingia Ikulu. Lowassa ametengeneza mtandao
unaomsaidia aingie Ikulu. Isipokuwa katika
maelezo yake Lowassa, amejitahidi kujitofautisha
na Kikwete na hasa aliposema suala la urafiki
wao lisihusishwe katika azma yake ya kuomba
nafasi ya kuwa rais.
Anawataka Watanzania wampime kama yeye
binafsi na wasilihusishe suala la urafiki wao. Sijui
kwa nini kwa sasa Lowassa anajitenga na
Kikwete. Lakini Watanzania wanakumbuka
Lowassa aliwahi kusema urafiki wao si wa
kukutana barabarani.
Kwa kuwa Lowassa anaomba nafasi ya nyeti ya
urais ni muhimu Watanzania wajiridhishe bila
shaka yoyote Lowassa ni nani. Na je anaweza
kukabiliana na changamoto zinazolikabili Taifa
letu hasa ufisadi, rushwa na kuporomoka kwa
maadili.
Mwalimu Nyerere katika kitabu chake, Nyufa, cha
mwaka 1995, alisema: “Sasa Tanzania inanuka
rushwa… tunataka kiongozi anayejua hivyo,
ambaye atasema rushwa kwangu mwiko,
mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa
na… watoa rushwa watamjua hivyo. Lakini
hatutaki aishie hapo tu, maana haitoshi wewe
mwenyewe uwe mwaminifu… Unaweza ukawa
wewe mwaminifu kabisa kabisa, lakini una
shinikizo la ndugu zako, jamaa zako na marafiki
zako.
“Kwa hiyo si inatosha wewe kuwa mwaminifu tu,
lakini uwe na uwezo wa kuwaambia jamaa zako
kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia
tena. Unawaambia jamaa na rafiki zako kwa
dhati kabisa… Ikulu ni mahali patakatifu, mimi
sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja
kupageuza pango la walanguzi na hakuna serikali
yoyote duniani inayoongozwa bila miiko”.
Zipo taarifa zinazoeleza kwamba fedha nyingi
zimetumika katika kufanya maandalizi ya
mkutano wa Arusha uliosababisha mafuriko ya
watu. Aidha, ndugu Lowassa mara kadhaa
amekiri kwamba marafiki zake ndio
wanaomchangia kufanikisha safari yake ya
matumaini.
Hivyo fedha nyingi anazochangia kwenye
harambee kwenye misikiti na makanisani nyingine
anatoa yeye na nyingine anachangiwa na hawa
marafiki zake ambao wengi wao ni wafanya
biashara matajiri na wengi wao ni wale
waliotajwa kwenye kashfa za ufisadi na tuhuma
mbalimbali.
Hawa marafiki zake Lowassa wamesaidia sana
kumjua Lowassa ni nani, kwani wahenga
walisema, “Nionyeshe marafiki zako na mimi
nitakuambia wewe ni nani au wewe una tabia
gani”.
Hawa marafiki zake na Lowassa wanaweza
kuwasababisha Watanzania wamtilie shaka
Lowassa kama anaweza kuwa safi na kustahili
kupewa dhamana ya kuongoza nchi. Naomba
niwakumbushe kauli ya Mwalimu Nyerere kuhusu
mmoja wa wagombea urais kwenye NEC Dodoma
mwaka 1995, “Hapa hatuchagui mtu maarufu,
tunachagua mtu safi na huyu si safi”.
“Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe
nae chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu.
Hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini
mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa
ugoni, Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike”.
“Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba si
kweli. Lakini Kaisari bado akamwacha, akasema
mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na
sisi hapa mgombea wetu hapaswi hata
kutuhumiwa wakati wapo wengine wasafi ambao
hawana tuhuma.
“Kama mtamteua huyu mimi sitapiga kampeni.
Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu
nimwombee kura. Hapana kabisa . Huyu najua si
msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa
mgombea wetu”.
Aidha, mtakumbuka pia kuwa mwaka 1995, kundi
la Vijana lilimtaka Lowassa ateuliwe kugombea
urais wa Tanzania. Hata hivyo, ilitolewa kauli
kuwa Lowassa alikuwa na tuhuma za rushwa,
kujilimbikizia mali na kupungukiwa na maadili,
kinyume na katiba ya CCM na kanuni za chama
hicho.
Kamati Kuu ilipopeleka mapendekezo ya
kutompendekeza kugombea urais, Lowassa
alitetewa kwa makelele, kihuni, bila kufuata
taratibu za kikao cha NEC Dodoma. Kundi moja
lilikuwa limejiandaa kumpitisha kwa hoja ya
nguvu na si kwa nguvu ya hoja.
Waliyatetea maelezo ya Kamati Kuu, lakini
waliyakataa yale ya nyongeza aliyoyatoa
Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi (Rais wa wakati
huo) ambaye alielezea tuhuma hizo zilizokuwa
zinamkabili Lowassa. Hivyo, naomba kusisitiza
kwamba Lowassa hakuwa chaguo la CCM katika
uchaguzi wa mwaka 1995.
Katika kikao hicho cha Kamati Kuu, Mwalimu
Nyerere aliamua kusaidia kikao kwa kutoa
maelezo ya nyongeza. Aliwauliza wajumbe wa
NEC maswali, kwamba wao ni wahuni au ni
viongozi wa CCM? Ikiwa wao ni viongozi wa
CCM, je, hivyo ndivyo wanavyopaswa kumtafuta
mgombea wa urais, kwa makelele?
Kama Watanzania wangewaona walivyokuwa
wanafanya katika kikao hicho, je, wangeamini
kuwa wao ni viongozi kweli? (Wajumbe walibaki
kimya). Kisha Mwalimu aliendelea kusisitiza
maelezo aliyoyatoa Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi
akisema: “Mwinyi amemstahi sana Lowassa”.
Hakuwaambia wajumbe wa NEC baadhi ya
tuhuma mbaya kabisa kuhusu Lowassa.
Ikiwa NEC inachoombwa ni kuchagua kati ya
wenye tuhuma za rushwa kuchaguliwa kwa nafasi
ya urais, na wale wasioitaka, basi huu ni wakati
muafaka kwao kuipeleka hoja hiyo mbele ya
Watanzania waiamue kwa kuwa ndani ya NEC
hakuna mwenye uwezo wa kumfukuza mwenzie,
wote ni wajumbe sawa kwa mujibu wa katiba ya
CCM”.
Hatimaye kikao cha NEC kiliondoa jina la
Lowassa, kikawateua Benjamin William Mkapa,
Cleopa David Msuya na Jakaya Mrisho Kikwete
kuwa wagombea. Majina yao yaliwasilishwa
kwenye Mkutano Mkuu ambao ndio uliopaswa
kumchagua miongoni mwao kuwa mgombea urais
wa CCM.
Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM, wagombea hao
watatu walijinadi kwa wajumbe. Kikwete
alipokuwa akijinadi aliwaeleza wajumbe kwamba
endapo wangempitisha kugombea na akashinda,
angemteua Lowassa kuwa Waziri Mkuu wake.
Lakini hapa pia tujiulize, pamoja na maelezo ya
Mwalimu Nyerere na Kamati Kuu kuondoa jina la
Lowassa kwa nini bado Kikwete alidiriki kumtaka
Lowassa awe Waziri wake Mkuu?
Hapa kwa akili za kawaida inaonekana dhahiri
kuwa Kikwete na Lowassa ni marafiki wakubwa.
Lowassa Alisha sema urafiki wao si wa kukutana
barabarani. Nionyeshe rafiki yako na mimi
nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani au
nitakuambia tabia yako.
Hata hivyo Kikwete hakuchaguliwa kuwa
mgombea urais. Historia hii inatoa mfano hai wa
jinsi matatizo yanayolikumba taifa letu
yalivyoanza.
Ni dhahiri kabisa kuwa watu walewale,
wakiongozwa na tamaa zilezile za kuwa matajiri
na kutaka urais kwa gharama yoyote hata
kuhonga au kutumia fedha, ndio wanaolisumbua
taifa letu mpaka sasa.
Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba, wale
wanaoomba nafasi ya urais hawapaswi
kutuhumiwa kwa jambo lolote. Hawapaswi
kutiliwa mashaka kuhusu uadilifu wao.
Wanapaswa kuaminiwa kuhusu dhamira yao ya
kupiga vita ufisadi na rushwa.
Na wagombea hawa tunaweza kuwajua kutokana
na hulka au tabia za marafiki zao. Katika
mafuriko ya Arusha, baadhi ya walioshiriki
mkutano huo walitajwa. Hawa walitajwa kuwa ni
marafiki wa Lowassa. Wengine walikuwa
wamevaa nguo zilizoandikwa “Marafiki wa
Lowassa”.
Baadhi ya marafiki wa Lowassa ni pamoja na
Rostam Aziz, Andrew Chenge, Anna Tibaijuka,
Cyril Chami, Ezekiel Mayige, David Matayo, Nazir
Karamagi na kadhalika.
Baadhi ya marafiki hawa wa Lowassa wengi wao
ni wale ambao ama walijiuzuru kwa kupatikana
na tuhuma za ufisadi, au wengi wao
waliondolewa kwenye nyadhifa zao kwa kashfa za
kutokuwa waadilifu.
Na wengi wao ni wafanyabiashara na matajiri.
Tunapoliangalia kundi la watu wanaomuunga
mkono Lowassa, tunaweza kujua Lowassa ni
nani. Tukiliangalia kundi linalomuunga mkono
Lowasssa tunaweza kujua kama Lowassa akiingia
Ikulu atapambana na rushwa na ufisadi au
ataenda kufanya biashara.
Je, marafiki wa Lowassa anaowataja na
walioonekana kwenye mafuriko ya Arusha
wanakerwa na rushwa na ufisadi kwa dhati?.
Ndege wenye manyoya yanayofanana ndio
wanaoruka pamoja.
Watanzania tukumbuke kwamba utumishi wa
umma ni dhamana na fursa adhimu kwa ajili ya
kulinda na kutetea maslahi ya wananchi wote.
Haya ni maneno aliyoyasema Rais Barack Obama
baada ya kula kiapo cha kuongoza Marekani.
Inawapasa wale wanaopata nafasi za
kuchaguliwa wafahamu kwamba wamepewa
dhamana ya kuwatumikia wananchi na si nafasi
ya kujitajirisha au kumnufaisha ndugu au
marafiki. Kutokana na kumomonyoka kwa maadili
na moyo wa uzalendo nchini, uongozi umegeuzwa
kuwa nafasi ya kujitajirisha. Urais, uimekuwa
fursa ya uwekezaji, na wala si fursa ya
kuwatumikia wananchi.
Ukweli kwamba kuna matajiri au watu
wanaotumia pesa kumiliki siasa na uongozi katika
nchi yetu, ni jambo lililo wazi. Zipo taarifa
kwamba baadhi ya watu wanaokwenda kwenye
mikutano ya watia nia ya urais mfano waliofurika
Arusha walinunuliwa waende kwenye mkutano,
walilipwa wapige kelele “Rais, Rais”.
Matumizi makubwa ya fedha yalionekana katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Baada ya
kutangazwa mshindi wa kiti cha urais katika
uchaguzi huo, Kikwete, alizindua Bunge Desemba
30, 2005 alidhibitisha hili alisema: “Yameanza
mawazo kuwa uongozi unaweza kununuliwa kwa
fedha.
“Tusipokuwa waangalifu, nchi yetu inaweza
kuwekwa rehani kwa watu wenye fedha za
kununua uongozi au wanaoweza kupata fedha za
kufanya hivyo, maana unaweza kufadhiliwa na
mtu ili ununue uongozi, ni vema sasa
tulishughulikie suala hili”.
Kuna mawazo kwamba sasa Tanzania inahitaji
Rais tajiri. Ninapenda niwakumbushe wosia
alilowahi kuutoa Mwalim Nyerere wakati wa uhai
wake juu ya hatari ya watu wachache wenye pesa
kujaribu kutafuta uongozi kwa manufaa yao.
Alisema: “Tanzania halijawa taifa imara sana na
adilifu kiasi cha kuruhusu matajiri kuingia kwenye
uongozi wa nchi kama ilivyo Marekani na Ulaya.
Wakati huo bado uko mbali sana na tukitaka
kuuvuta kwa kamba huko ndiko kuliingiza taifa
letu changa kwenye kiwango cha ufisadi”.
Mgombea mmoja wa urais amesema bado
anasaka utajiri na anaomba aende Ikulu. Je Ikulu
kuna biashara gani itakayompatia utajiri? Na wale
wanaomuunga mkono atawalipaje akienda Ikulu?
Nchi kuwekwa rehani kwa matajiri ni jambo la
hatari sana, kwa maana serikali itaongozwa na
matajiri na haitawajibika kwa wananchi. Hili
limeanza kujitokeza. Demokrasia itakoma na
udikteta utatawala.
Jambo linalojitokeza hapa na ambalo ni matokeo
ya matumizi makubwa ya fedha na rushwa
kwenye chaguzi, ni kupatikana kwa viongozi
ambao hawakuchaguliwa na wananchi bali
walinunua uongozi au waliotoa rushwa
kushawishi wapiga kura wawape uongozi.
Serikali inayopatikana kwa rushwa haiwajibiki
kwa wananchi. Hutumikishwa na matajiri
walionunua uongozi na waliotoa rushwa. Serikali
hiyo huwaabudu matajiri walioiweka madarakani,
haiwezi kufanya maamuzi yenye maslahi kwa
wananchi.
Serikali hiyo hulinda maslahi ya watu wachache,
haiwezi kuchukua hatua dhidi ya ufisadi. Baadhi
ya maamuzi ambayo yamekuwa yakitolewa na
utawala wa awamu ya nne, ripoti ya hivi karibuni
ya Ikulu ya TOKOMEZA na ESCROW ni ushahidi
wa ninachokieleza.
Tuwe makini na wagombea wanaotumia fedha
nyingi na wanaopewa fedha nyingi na marafiki
zao katika mchakato wa kutafuta nafasi za
kuchaguliwa urais, ubunge na udiwani.
Tumejifunza katika utawala wa awamu ya nne.
Tusirudie makosa.
Ningependa kusisitiza, Watanzania tunatakiwa
tuichukie rushwa ya aina yoyote. Rushwa ni
dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti.
Rushwa hupofusha macho na moyo. Taifa
linaoendekeza rushwa ni taifa ambalo watu wake
ni sawa na vipofu na wafu.
Vipofu ambao hawaoni madhara ya rushwa na
mioyo yao imekufa. Rushwa inapotolewa na
kupokelewa kwa shangwe makanisani na
misikitini na wagombea wa vyama vya siasa ni
ushahidi wa jambo hili.
Tanzania ina nafasi ya kuwa Taifa
linaloheshimika kama tutaichukia rushwa na
kukataa kuipokea au kuitoa. Mfalme Suileman
aliwahi kusema; “haki huinua taifa bali dhambi na
uovu ni aibu ya watu wote”. Rushwa ni dhambi
na ni aibu kwa watanzania wote.
Tanzania imepoteza heshima kwa sababu ya
rushwa. Pia napenda kusisistiza, Kwenye nchi
ambapo rushwa imetawala sauti ya wengi si sauti
ya Mungu. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu
kwenye nchi ambapo haki, usawa na upendo
vinatamalaki.
Mafuriko ya watu kule Arusha kama walilipwa ili
waende kwenye mkutano sauti yao si sauti ya
Mungu. Na, Je Lowassa ana dhamira ya kweli ya
kuchukia rushwa?
Nionyeshe marafiki zake na mimi nitakuambia
kama Lowassa ana dhamira ya kweli ya kupiga
vita rushwa na ufisadi. Niliposikiliza akisema
atapiga vita ufisadi, rushwa na atahakikisha
rasilimali za nchi hii zinawanufaisha Watanzania
na nilipowangalia marafiki zake ni nani, nilitambua
anachokifanya ni usanii. Hana dhamira ya kweli
na anachokisema.
Lowassa hafai kuwa Rais.

Hii sio gazeti ni novel 😳😳😳
 
nyie mpeni magufuli, lakini lowasa ndo raisi ajaye.

unaringa na ka kura kako kamoja, hukuona nyomi zile dar,mbeya,arusha,mwanza na visiwani.
mtanyooka.
 
Bora kuchagua "wezi" walioko UKAWA kuliko kuichagua tena CCM.

CCM iondoke kwanza, haya mengine tutayerekebisha mbele kwa mbele!

VIVA UKAWA, VIVA CHADEMA, VIVA LOWASSA...

Nchi imeitikaje!!!!
 
bora kuchagua "wezi" walioko ukawa kuliko kuichagua tena ccm.

Ccm iondoke kwanza, haya mengine tutayerekebisha mbele kwa mbele!

Viva ukawa, viva chadema, viva lowassa...

Nchi imeitikaje!!!!

alipo upo.....

Njaa mbaya sana.
 
Back
Top Bottom