Upo sahihi rais wangu lakini uharaka wa nini?

Upo sahihi rais wangu lakini uharaka wa nini?

Mzururaji

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
1,558
Reaction score
1,274
UPO SAHIHI RAIS WANGU, LAKINI UHARAKA WA NINI?

_Na Mzururaji wa Gairo Morogoro_

Domo la bibi kizee hudaiwa hunuka lakini mate yake hutibu baadhi ya magonjwa kijijini kwetu!!Sahau ubaya wa baniani na tuanze sasa kutambua umuhimu wa viatu vyake.

Hakuna shaka kuhusu ubabe wa rais wetu wa awamu ya 5. Ni mbabe ndio lakini mbona kama subira ni faida. Ingawa tulikosa ubabe hatukua na mtu wa mwisho ambaye sauti yake ikisikika hufunga mjadala! Yaani kama baba katika familia

LAZIMA TUHAMIE DODOMA TUPENDE TUSIPENDE

Jana tar 30/7/2016 mh rais amenukuliwa akisema atakapo hamisha serikali kwenda Dodoma kutekeleza ile ndoto ya siku nyingi ya serikali kuhamia Dodoma atauza majengo ya serikali

Mimi mtembea hovyo naungana na wazo la msingi la KUHAMIA DODOMA lakini naona hapana haina haraka kiasi hiko kuuza hayo majengo, kwanini iwe haraka kiasi natamani kusiwe na uharaka wa kuuza haya majengo.

Wasiwasi wangu umejikita hasa katika kumbukumbu ya uuzwaji wa nyumba za serikali wakati wa awamu ya tatu.

Mh, raisi ulikuwa Waziri mwenye zamana kuna nyumba ziliuzwa bei ndogo sana kuliko bei ya kiwanja chenyewe hii ikazua lawama nyingi sana kwa wadau mpaka Leo na kuonekana kuwa lile wazo halikuwa la busara hata kidogo.

Mh, zile nyumba zingewezwa kupangishwa kwa watumishi wa serikali lingekuwa jambo jema sana kuliko uamzi ule wa wakati ule wa wakuziuza.

Naona kuuza majengo ya serikali kwa sasa hapana tusubiri kwanza kwa sababu zifuatazo;'-

Mosi, badala ya kuyauza natamani tuyabadilishie matumizi mengine kwa mfano mengine yawe mahospital kupunguza msongamano wa wagonjwa mengine yageuzwe hata mabweni kwa ajili ya kupunguza adha kwa watoto wanao soma shule za kata hasa mabinti ambao kila siku wanakumbana na changamoto ambazo zinawarudisha nyuma kitaaluma. Pia hata hosteli kwa wanachuo kama UDSM "vipanga" ambao kila siku wana lalamika uhaba wa hostel.

Pili yarudishe katika halmashauri husika ambapo hayo majengo yapo ili hizo halmashauri wayapangie majukumu mapya kuliko kuyauza naamini halmashauri zetu bado zina uhaba wa majengo ya kutosha hivyo haya majengo yakirudishwa halmashauri utakuwa ume rahisisha upatikani Wa huduma serikalini.

Siamini kama wizara zote zikiamia Dodoma kwa vitengo vyote Dodoma itatosha kama itatosha ufanisi utakuwa mdogo sana kwani watumishi wengi watarundikana sana, hapa natolea mfano wa halmashauri ya wilaya mpya ya Buhigwe ambayo imemegwa kutoka kasulu watumishi wote wamerundikwa kwenye darasa moja na kupelekea baadhi ya kazi kufanyika kasulu. Nataka kujenga hoja kuwa majengo hayana uharaka kiasi hiko wa kuyauza

Endapo serikali mkiyauza ipo siku mtayahitaji na ikiwezekana mtayapangisha wenyewe tena kwa gharama waswahili husema muda ni muamuzi mzuri endapo tukiyauza hayo majengo ipo siku tutayahitaji hata kama sio kipindi chako ipo siku raisi ajaye atayahitaji hayo majengo hivyo kupelekea kuonekana uamzi wa kuyauza haukuwa wa msingi sana na utakuja kuonekana tulikurupuka.

Hivyo ingawa kwa wakati huu utaonekana wa msingi hapa ntatolea mfano wa nyumba ambazo ziliuzwa chini yako zilionekana hazikuwa na maana yoyote kipindi kile lakini kwa sababu ya muda uamuzi ule ukaonekana ulikuwa wa hovyo kuwahii kufanywa kwani mahitaji ya nyumba kwa watumishi unaonekana mpaka kesho.

Mh rais kama majengo haya yakiuzwa siamini kama yatauzwa bei ya kuridhisha haya yatauzwa bei ya kutupwa kama zilizo fanyika wakati wa uuzaji baadhi wa nyumba za serikali kwani wewe mweshiwa raisi naamini hauto husika katika upangaji wa bei wa hayo majengo bali kutakuwa na bodi ambayo itahusika na uuzaji huu hapa ndo utajikuta pale BOT yakiuzwa bei ambayo hata mimi Mzurulaji naweza imudu lakini sitopata hiyo nafasi.

Mwisho kabisa Mhe, rais kama utaona inafaa kuendelea kuyauzai hayo majengo naomba nikili wazi yale majengo pacha ya BOT nayatamani mniuzie yaani nina interest nayo naapa kwelikweli yani nayatamani.

By Mzururaji wa Gairo Morogoro
 
Sikiliza Mzururaji umetoa maelezo mazuri na marefu sana, sema kwa kifupi tu kuwa wananchi hatukubaliani na Wazo la kuuza majengo ya Serikali, kwanza hata sababu iliyotolewa haingii akilini eti ili watumishi wote wahamie dodoma, hivi kweli inaingia akilini kuuza majengo ya Serikali kwa sababu hiyo, labda kama alikuwa anatania
 
Mzururaji umetema point hatari, mimi naamini mji wa Dodoma hauna accomodation ya kupokea wizara zote na watumishi wake kwa sasa hv pili kunaswala miundo mbinu. Halafu kumbuka kuna balozi kadha wakadha ambazo nazo zina watumishi na zinahitaji maofisi huko Dodoma.
Kweli swala lakuhamia Dodoma ni la msingi lakini sio lakukurupuka na kuanza kuuza majengo ambayo yamechukua muda na rasilimali nyingi mno kuyafikisha hapo yalipo.
Mh. Raisi atulie Dodoma tutaenda taratibu walisiokwamba tusipo enda kesho tunaingia hasara kubwa, kama ninayoona tutaingia tukikurupuka.
 
Very constructive idea by Mzururaji, kudos! Ingawa watakuja watu wa mihemko na kuanza kukuona wewe unampinga rais na ni mpinzani .

Vv
 
Nani wa kumfunga paka kengele brother akiamu kaamua kweli kweli ila akipitia huu Uzi wenda akabadiri mawazo ya kuuza
 
Hivi nyumba za serikali sio goverment security? Au wana maana mengine kiuchumi kama kucontrol infation kulinda thamani ya shilingi kucontrol money circulation, kufinance big project kama hiyo ya kuhamia dodoma, nawaza tu mwenye ujuzi wa mambo hayo atujuze vizuri.
 
Back
Top Bottom