Upinzani Zimbabwe wataka serikali ya mpito

Upinzani Zimbabwe wataka serikali ya mpito

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa ametoa wito jana wa kuundwa serikali ya mpito kutatua hali mbaya ya kiuchumi na mzozo wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo.

Upungufu wa fedha za kigeni katika wiki za hivi karibuni umezusha mzozo mkubwa wa kiuchumi ambapo upatikanaji wa mafuta , chakula na madawa unapungua.

Hatua ya kwanza ni kwa nchi hii kuingia katika njia ya mjadala wa kisiasa, amesema chamisa mwenye umri wa miaka 40, kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change MDC, ambaye amedai kwamba ameshinda uchaguzi wa rais wa hapo Julai 30.

Chamisa ambaye alishindwa na rais wa sasa Emmerson Mnangagwa , amesema amekutana na viongozi wa kidini ambao wanataka mjadala wa kisiasa kati ya upinzani na rais.

DW swahili
 
Kweli viongozi wa kidini nchi zingine wana nguvu sana ya ushawishi sana na wanaheshimika. Ila hapa bongo. Wamenywea sana
 
Back
Top Bottom